Jumatano, 7 Machi 2018

MAVUNDE AFUNGA KIWANDA SINZA,VIWILI VYATOZWA FAINI AENDELEA KUSISITIZA JUU YA WAAJIRI KUTOA MIKATABA KWA WAFANYAKAZI WAO KWA MUJIBU WA SHERIA

hPosted by Esta Malibiche ON March 8,2018 IN NEWS


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde leo ameendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa sheria mbalimbali za kazi kwa kuagiza kusimama uzalishaji kwa kiwanda cha magunia cha *TASIPA LIMITED* kilichopo Sinza Mkoani Dar wa Salaam kutokana na mazingira hatarishi ya kufanyia kazi sambamba na kuwatoza Faini ya kiasi cha Shilingi *18,000,000* kwa kukiuka *Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 5/2003*

Naibu Waziri Mavunde pia amevitoza faini Kiwanda cha Kutengeneza Nywele  *S.H AFRIQ (T) LTD* -**8,000,000** kilichopo Tabata Segerea na Kiwanda cha Magunia cha *Heng Ji Investment* *Tsh 21,000,000* kilichopo Shekilango Sinza kwa kukiuka Sheria ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi na kutumia nafasi hiyo pia kuagiza wafanyakazi wote wapewe mikataba kwa mujibu wa *sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6/2004* ndani ya siku kumi na nne(14).

Mavunde pia ameendelea kusisitiza Waajiri wote kujiunga na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na kwamba zoezi la kuwabaini waajiri ambao hawajisajili katika Mfuko ni endelevu na kwamba  Mfuko hautabadili msimamo wake juu ya hilo.

0 maoni:

Chapisha Maoni