Posted by Esta Malibiche on March 23,2018 in SIASA
Na Esta Malibiche
Iringa
Katibu Mkuu wa UWT Taifa Amina Makilagi,ambae pia ni mjumbe
wa Halmashauri kuu ccm Taifa amevuna wanachama wapya 200 katika kata ya Ifunda Halmashauri ya Iringa
vijijini ambao wamejiunga rasmi jana na umoja huo na kupewa kiapo.
Akizungumza na Uwt Kata ya Ifunda Halmashauri ya Iringa Vijijini mara baada ya kuwapokea Wanachama
hao,Katibu mkuu aliwata
wanachama wapya kutoa ushirikiano kwa ccm pamoja na Serikali yake ikiwa
nipamoja na kuwafichua wale wote wanaokwamisha shughuli za maendeleo
zinazotekelezwa na Serikali ili CCM iendelee kushika hatamu.
Makilagi alisema kuwa chama cha Mapinduzi ni chama ambacho
kimejengwa kimisingi ya kulea jumuhia mbalimbali ambazo zipo ndani ya
chama hicho ndio maana bado kinanguvu katika siasa za hapa nchini hata kimekuwa
mfano kwa nchi nyingine.
Alisema kuwa lengo la ziara hiyo Mkoani Iringa ni kutokana na
Agizo la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Rais John Magufuli kuwataka
vipongozi wa chama hicho na Jumuiya zake, kuacha kufanya kazi kwa mazowea kwa
kukaaa ofisini,bali wawatembelee wanachi kujua changamoto zinazowakabili ili
ziweze kutatuliwa.
“Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi Tanzania ni
moja kati ya jumuiya ambayo ipo ndani ya chama hiki na inakazi zake kwa ajili
ya kukijenga chama na kuleta maendeleo kwa wananchi waliokipa dhamana ya
kuongoza nchi hii” alisema Makilagi
Aidha Makilagi aliwataka wanawake kujifunza kujitegemea ili
waweze kuja kuwaajiri wanaume ambao kwa sasa ndio wamekuwa wakitoa ajira nyingi
kwa wanawake hapa nchini.
“Wanawake wenzangu sasa imefika mwisho wa kuwa tegemezi kwa
wanaume inatakiwa sasa tusimame sisi kama sisi na tuanze kuwaajiri na kulisha
wanaume zenu majumbani kwetu maana tunauwezo wa kufanya kila kazi hizo
inatakiwa tujitume” alisema Makilagi
Alisema kuwa wanawake mkiwa mnataka kufanya biashara zenye
malengo msiogope kwenda kukopa maana siku hizi kuna mikopo ya bei rahisi na
riba yake sio kubwa ambayo itakuwezesha kufanya biashara yako kwa maendeleo
yako.
“Ninawaomba msibweteke,huu ni muda wa kuamka na kuchangamkia fursa zilizopo.Siku hizi Benki
nyingi zinawakopesha wanawake na wanawaamini sana wanawake kwenye kufanya
biasha hivyo nendeni mkakope msiogope maana hizi benk zipo kwa ajiri ya
kusaidia kuinua maisha ya mtanzania” alisema Makilagi
“Jamani kila pesa ukiitumia kwa nidhamu basi utaona faida yake
na itakuletea maendeleo yako na taifa kwa ujumla maana unakuwa umetumia vizuri
pesa kwa maendeleo” alisema Makilagi.
0 maoni:
Chapisha Maoni