Alhamisi, 1 Machi 2018

MAVUNDE ATUA KILIMANJARO ASEMA SERIKALI YA AWAMU YA TANO YADHAMIRIA KULINDA HAKI ZA WAFANYAKAZI WANAOPATA MADHARA KAZINI

Posted by EstaMalibiche ON March 2,2018 IN NEWS



SERIKALI ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuhakikisha wafanyakazi wanalindwa na kupata haki zao pindi wanapopatwa na madhara yatokanayo na kazi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amesema mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro leo.

Mheshimiwa Mavunde ameyasema hayo leo *Machi 1, 2018* wakati akiendelea na ziara yake ya kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeleza takwa la kisheria linalowataka waajiri wote katika sekta rasmi,(umma na binafsi), waliopo Tanzania Bara kujisajili na kuchangia kwenye Mfuko huo.
Kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Ikiwa Mwajiri hajajisajilil kwenye Mfuko, atakuwa ametenda kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi na akipatikana na hatia adhabu yake ni kulipa faini isiyozidi *shilingi milioni 50,000,000* (Milioni Hamsini) au kifungo kisichozidi miaka mitano jela au adhabu zote kwa pamoja, alisema Mhe. Mavunde.

Mheshimiwa Mavunde ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anslem Peter na Kaimu Kamishna wa Kazi kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, alibaini Mkoa wa Kilimanjaro wenye jumla ya Waajiri 1,039 ni waajiri 525 tu ndio wamejisajili huku wengine 514 bado hawajajisajili na Mfuko.

“Serikali ilikwishatoa matamko mbalimbali yanayowahimiza waajiri kutekeleza takwa hilo la kisheria, na leo hii hakuna njia nyingine, Waajiri hawa tuliowabaini hapa Mkoani Kilimanjaro naagiza WCF iwapeleke mahakamani haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake.” Alisema.

Alisema sio lengo la serikali kuwatisha au kuwadhalilisha waajiri hao bali nia ni kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa lakini pia kuwaondolea jukumu waajiri la kuwahudumia wafanyakazi wao wanapopatwa na madhara wakiwa kazini.

“Tunataka ninyi wawekezaji, (waajiri), mjielekeze kwenye shughuli zenu za msingi kwa maana ya kufanya uwekezaji na biashara zenu na hili la kumuhudumia mfanyakazi aliyepatwa na madhara kazini lishughulikiwe na serikali.” Alisisitiza.
Tayari Mhe. Mavunde amefanya ziara kama hiyo mkoani Mwanza na Shinyanga na kubainisha kuwa operesheni hiyo ya kuwabaini waajiri wasiotekeleza takwa hilo la kisheria litafanyika nchi nzima, na kuwataka waajiri kufanya hivyo haraka ili wasijikute kwenye matatizo.
“Tumewasambaza maafisa wetu wa WCF mikoani na wanaednelea na utaratibu wa kuwafuikisha mahakamani waajiri wote ambao wameshindwa kufuata sheria






.

0 maoni:

Chapisha Maoni