Posted by Esta Malibiche on JAN 31,2018 IN NEWS
Rotary
Club of Iringa imepanda miti ya matunda zaidi ya 134 katika ya
wasichana ya iringa (Iringa Girls Secondary School) ikiwa mkakati
kabambe wakupanda miti katika shule mbalimbali mkoani hapa.
Zoezi
la upandaji miti katika shule hiyo iliongozwa na rais wa rotary club of
iringa Miraji Vanginothi kwa kushirikiana na MKUU wa Wilaya Iringa
Richard Kasesela.
MKUU
wa Wilaya Iringa Richard Kasesela amesema kama watu watajenga utamaduni
wa kuwaangalia na kuwasaidia watu wengine wataishi kwa furaha katika
maisha yao.
Kasesela
ametoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya
upandaji miti katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa
Girls).
Zoezi
la upandaji miti katika shule hiyo liliandaliwa na Kikundi cha Rotary
Club tawi la Iringa kazi hiyo ikishirikisha wanafunzi wa kidato cha
tano nasita na uongozi wa shule.
"Ngoja
niseme mambo mawili,kwanza ukiwa Rotarian ni kumuungalia mwenzako,hilo
ndo jambo la Msingi,ni jumuiya ya kimatifa na kikibwa ni
kujitolea"alisema Kasesela.
Kasesela
aliwataka wanafunzi wa shule hiyo pamoja na vijana kujenga utamaduni wa
kufanya jambo kwa lengo la kusaidia wengine na kwamba kwa kufanya hivyo
watakuwa wamejijengea uwezo wa kutenda mema.
"Hata
leo tunapanda miti ,hii miti si kw aajili yetu ni kw aajili ya watu
wengine,ndio sababu mi mara nyingi ninasema nivema kila unalofanya
ufanye kwa ajili ya mwingine:
:Umezaliwa
na mtu mwingine,umepokelewa na mtu mwingine,utalelewa na mtu
mwingine,utaolewa na mtu mwingine na utazikwa na mtu mwingine hivyo kila
mtu akifanya kwa ajili ya mtu mwingine nchi yetu na dunia kwa ujumla
itabaki kuwa na amani"alisema.
Awali
akizungumza katika zoezi hilo Rais wa Rotary Club Tawi la Iringa Miraji
Vanginothi aliwashukuru watu waliojitolkea kupanda naa miti katika eneo
la shule hiyo na kuutaka uongozi w ashule na wanafunzi kuitunza kwa
faida yao na kizazi kijacho.
"Tumepanda
miti jukumu lenu ni kuhakikisha mnaitunza kwa aajili ya kizazi
kijacho,miti niu kwa ajili ya kutunza mazingira miti ni kw aajili ya
maatunda"alisema Vanginothi.
Kwa
upande wake Mkuu wa shule ya hiyo Blandina Nkondola alishukuru Rotary
Club tawi la Iringa kwa uamuzi w akupanda miti katika shule hiyo na
kuahidi kuitunza.
"Tunawashukuru
sana kwa msaada wenu wa kijamii,tumefurahishwa na uamzui wenu wa
kizalenda wwenye lengo al kutunz amazingira yetu na tuwahakikishei tu
kwua tutaitunza hii miti"alisema,Nkondola.