Alhamisi, 24 Agosti 2017

MAVUNDE AZINDUA PROGRAMU YA KUKUZA UJUZI KWA VIJANA MTWARA


Posted by Esta Malibiche on AuGust 24,20¹7 IN NEWS
Naibu Wazi:i  ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,kazi ,vijana na Ajira Anthony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya utambuzi wa ujuzi ,uliofanyika Mkoani Mtwara leo.










Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Anthony Mavunde  leo amezindua Mafunzo ya utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi kwa vijana TAMBUZI WA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI kwa Vijana 847 kutoka Mikoa ya Mtwara, 847 kutoka mikoa ya Mtwara,Lindi, Morogoro, Pwani, na Dar es Salaam yaliyozinduliwa Mkoani Mtwara. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, amewataka Vijana kuutumia ujuzi watakaoupata kupitia mafunzo hayo ili waweze kujiajiri na kuajiri Vijana wengine na pia kutumia ujuzi huo kushiriki katika Uchumi wa Viwanda.

Mavunde aliwataka Vijana waliopata fursa ya kuingia kwenye Mafunzo Haya, kutumia vizuri fursa hii kwa kuwa WAAMINIFU na KUWAJIBIKA ipasavyo ili kujenga msingi wa mafanikio.

Mafunzo haya yanatolewa na Serikali kupitia Fedha za walipa KODI, hivyo mhakikishe fursa hii vyema ili iongeze thamani katika shughuli zenu,Serikali ya Mhe John Pombe Magufuli imedhamiria kuwekeza kwa vijana kwa kuwajengea UJUZI vijana na KUWAWEZESHA  ili waweze kushiriki katika Uchumi wa Nchi yao"Alisema Mavunde

Vijana washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Serikali ya awamu ya Tano kwa kuthamini VIPAJI vyao vya ufundi kwa kuwaongezea Ujuzi na kuwarasimisha kwa kuwapatia vyeti vya Mafunzo ya Ufundi pasipo wao kupitia vyuo vya Ufundi katika utaratibu wa kawaida wa masomo.










0 maoni:

Chapisha Maoni