Jumanne, 1 Agosti 2017

KATIBU WA UMOJA WA VIJANA CCM MKOA WA IRINGA JEMSI MGEGO AANZA ZIARA YA SIKU 9 KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO MANISPAA YA IRINGA

Posted by Esta Malibiche on August 1,2017 IN SIASA


Katibu wa umoja wa vijana ccm Mkoa wa Iringa Jemsi Mgego akizungumza na wananchi wa kata ya Ilala ,ikiwa ni moja ya ziara yake ya siku tisa aliyoianza leo hii.Katika ziara hiyo aliambatana na katibu wa umoja wa ccm Iringa mjini Patrick Muyinga.
 Akizungumza  na wananchi wa kata ya Ilala na Mkwawa kwa nyakati tofauti,Mgego alisema kuwa lengo la ziara hiyo niKuangalia Uhai wa Chama na jumuiya,
 kukagua zoezi zima la Uchaguzi wa Chama na jumuiya,
,Kukagua na Kushiriki shuguli za maendeleo (Utekelezaji wa Ilani)
kusikiliza kero za Vijana, Wanaccm na wananchi kwa Ujumla

"" Katika ziara hii Nitakutana na =Viongozi wa Chama na serikali
Viongozi wa Jumuiya zote UVCCM, UWT na WAZAZI,Wanaccm wote na wananchi kwa ujumla"""Alisema Mgego ""
Alisema kuwa katika ziara hiyo ataweza kutembelea viradi ya serikali na ya chama, pamoja na kushiriki shuguli za maendeleo.
Aidha alitoa wito kwa viijana, Wanachama wa CCM na wanachi kwa ujumla wajitokeze kwa wingi kutoa kero zao na chanagamoto zinazowakabili katika maeneo wanayoishi ili ziweze kutatuliwa.

Katibu wa umoja wavijana ccm Jemsi Mgego akipokea Taarifa ya tekelezaji shughuli za maendeleo kutoka kwa Afisa Mtendaji wa kata ya Mkwawa Manispa ya Iringa.


Katibu wa umoja wa vijana ccm Mkoa wa Iringa Jemsi Mgego akiwa na katibu wa Uvccm Iringa Mjini Patrick Muyinga wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa chama na Serikal wa kata ya Mkwawa mara bada ya kupokea Taarifa.
Katibu wa umoja wa vijana ccm  Iringa Mjini Patrick Muyinga akizungumza na wananchi wa kata ya Ilala
Katibu wa umoja wa vijana ccm  Iringa Mjini Patrick Muyinga akizungumza na wananchi wa kata ya Ilala

Katibu wa umoja wa vijana Ccm Mkoa wa Iringa Jemsi Mgego na Katibu wa umoja wa Vijana Ccm Iringa Mjini wakiwa katika picha ya pamojq na viongozi wa serikali ,Chama pamoja na vijana wa kata ya Ilala.







0 maoni:

Chapisha Maoni