Jumanne, 15 Agosti 2017

DC MOFUGA:WAHAZABE HAKIKISHENI MNAWAPELEKA WATOTO SHULE

Posted by Esta Malibiche on August 15,2017 IN NEWS

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mkoani Arusha Chelestino Mofuga akizungumza na wananchi wa kabila la wahazabe katika mkutano uliofanyika katika kitongoji cha Umbea ikiwa ni moja ya ziara aliyoifanya leo hii kwa lengo la kusikiliza kero zinazowakabili.

Mkuu Wa wilaya ya mbulu chelestino s mofuga leo tarehe 15/8/2017 amefanya mkutano na wahazabe kusikiliza kero zao katika kijiji cha Dumang kitongoji cha umbea. 

Wahazabe wamemwambia mkuu wa wilaya kuwa uhalibifu wa mazingira unaofanywa na wafugaji na wakulima una hatarisha maisha yao, kwani ni vigumu kupata asali na matunda. Pia wamelalamika kuhusu huduma za afya na maji kuwa ni tatizo kubwa katika eneo hilo. 

Mofuga alimwagiza mkurugenzi kutuma wataalamu kusimamia mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kulinda mazingira hayo. Pia kuwasogezea huduma ya maji na afya katika kata ya Eshkesh ili kunusuru maisha yao ambapo kaimu mkurugenzi matia amesema halmashauri imetenga milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati. 

Wahazabe wamemwambia mkuu wa wilaya kwamba wanaomba serikali iwape nafasi ya kuwashirikisha katika ngazi za maamuzi mbalimbali na mkuu wa wilaya amewahimiza kuanza kugombea nafasi za uongozi kuanzia vijiji, kata hadi ubunge na kuwasihi jamii hiyo wakijitokeza   wawachague.

Aliwapongeza vijana wa kihazabe waliofika vyuo vikuu, na kuwataka wahazabe wote Wahakikishe wanawapeleka watoto wao shule.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya alipokea zawadi ya shanga,kwa niaba ya waziri mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa wakimsihi amfikishie huku wakimuomba waziri mkuu awatembelee.

Pia mkuu wa wilaya amepokea zawadi ya kitabu cha maisha ya wahazabe kutoka kwa mtafiti aliyeishi na wahazabe zaidi ya miaka 20 ndg Daud Beroff ,na amemhakikishia mkuu wa wilaya kuwa hela kusomesha wahazabe ipo ya kutosha inayotokana na kuuza kitabu hicho na mavuno ya hewa ukaa kutoka bonde hilo.










0 maoni:

Chapisha Maoni