Jumatatu, 28 Agosti 2017

KARDINALI PENGO AKABIDHI MRADI WA KISIMA KWA SERIKALI

Posted by Esta Malibiche on August 28,2017 IN NEWS

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amemkabidhi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu,kisima cha maji katika kituo cha mafunzo cha watoto (Mahabusu ya watoto) Upanga jijini Dar es salaam. Kardinali Pengo amekabidhi mradi huo uliotokana na michango iliyotolewa na Watoto wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam, ambapo hadi kukamilika kwake mradi huo umetumia jumla ya shilingi Milioni 11,780, 000/=. (Na Pascal Mwanache)
























0 maoni:

Chapisha Maoni