Ijumaa, 25 Agosti 2017

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MWIGULU NCHEMBA ATOA SIKU 7 UNHCR KUKAMILISHA TARATIBU ZA KUWAREJESHA WAKIMBIZI BURUNDI

Posted by Esta Malibiche on August 25,2017 IN NEWS

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akiwahutubia wakimbizi katika kambi ya Nduta wilayani Kibondo Mkoani Kigoma

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba ametoa siku saba kwa shirika la wakimbizi Duniani ( Tanzania) kukamilisha taratibu za kuwarudisha warundi waliomba kwa ridhaa yao kurudi nchinj kwao Burundi.
Waziri Mwigulu amefikia hatua hiyo baada ya kupata taarifa ya watu 8,743 ambao wamejisajili kwa hiari yao kurudi burundi wakiwa katika kambi ya Nduta iliyopo wilayani kibondo mkoa kigoma, lakini wanakwamishwa na shirika la UNHCR ambalo wanasema wanataka kukaa vikao ndio waweze kiwarudisha.
Waziri Mwigulu amesema baada ya siku saba endapo UNHCR watashindwa kuwapeleka kundi la kwanza kwao basi yeye ataongea na waziri wa ulinzi kuomba kwa Amri jeshi mkuu Rais Magufuli magari ya kuwarudisha wakimbizi hao makwao.
Kwa upande wa mkuu wa makazi ya Nduta Peter Bulugu amesema kwasasa wanajumla ya wakimbizi na waomba hifadhi 127,715 na kati ya hiyo watu 8,743 wameomba kurudishwa makwao na kuchelewa kurudishwa kuna pelekea sasa hali ya usalama kuwa si nzuri kwani kunawepo na vitendo vya vurugu za mara kwa mala kutoka kwa wakimbizi hao wanaotaka kuondoka.
Nduta amesema kupunguzwa kwa chakula kumechangia kuongezeka vitendo vya wizi ndani na nje ya kambi (wizi wa mifugo na mazao mashambani wizi wa taa za mitaani kambini (48 kati ya 217 zimeibbiwa) utekaji na ubakaji barabarani umeongezeka sasa.

Moja ya wakimbizi ambaye alikutwa anajiandikisha kurudi kwao amsema ameamua kujiandikisha baada ya kuambiwa kuna usalama kwao lakini pia changamoto wanazo kutana nazo za kupunguzwa kwa chakula walichokuwa wanapata mwanzo mpaka sasa kufikia kula mlo moja kwa siku ameona bora arudi kwenda kuwai muda kilimo.
ndu1
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mmoja wa viongozi wa Shirika linaloshughulikia wakimbizi NHCR katika Kambi ya Nduta Kibondo mkoani Kigoma.
ndu2
Baadhi ya wakimbizi wakijisajili kurejea nchini kwao Burundi.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akiwahutubia wakimbizi katika kambi ya Nduta wilayani Kibondo Mkoani Kigoma
ndu4
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika linaloshughulikia wakimbizi kambi ya Nduta Kibondo mkoani Kigoma 





0 maoni:

Chapisha Maoni