Jumatatu, 21 Agosti 2017

ALPHONCE MUYINGA:VIJANA WAFICHUENI VIONGOZI WAZEMBE

Posted by Esta Malibiche on August 21,2017  IN SIASA

Katibu wa umoja wa vijana ccm Iringa mjini,Alphonce Patrick Muyinga akizungumza na vijana wa uvccm  kutoka kata zilizopo Manispaa ya Iringa.

KATIBU wa jumuiya ya umoja wa vijana ccm wilaya ya Iringa Mjini ndg: Alphonce Patrick Muyinga,amewataka vijana kutoa ushirikiano  kwa kuwafichua viongozi wazembe watakaodiliki kukwamisha shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na serikali.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na vijana katika kata mbalimbali zilizopo Manispaa ya Iringa,wakati akitoa semina kwa viongozi wapya ili waweze kujua majukumu yao kwa mujibu wa kanuni ya uvccm.
Muyinga alisema kuwa,kijana ndio Mpelelezi na askali wa chama pia Kijana ni sehemu kubwa katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuwataka kuwa mstari wa Mbele kupaza sauti zao pale wanapoona maovu kuanzia serikali za mitaa na kutowafumbia macho watendaji wazembe watakao diriki kukwamisha utekelezaji wa Ilani ya Ccm.
"" Nawaomba vijana wenzangu tusimfumbie macho kiongozi yeyote atakae leta uzembe kwa makusudi,maana ujinga wa mtu mmoja ukiachwa unaweza kuisababishia Serikali hasara ukizingatia ni serikali inayoongozwa na chama cha Mapinduzi ccm.Kwa hiyo vijana wote tunapaswa kuwa mstari wa mbele kuonyesha uzalendo wetu kwa kukitetea Taifa letu na  chama chetu cha Mapinduzi""Alisema Muyinga na kuongeza kuwa
Vijana ndiyo dhamana ya Ccm,kwahiyo vijana tunatakiwa  tuwe mstari wa mbele kusema ukweli na kulinda rasilimali zetu pia Katibu Muyinga akasema kwa Kijana yoyote atakae kuwa na taharifa ya siri kuhusu Mtendaji yoyote wa serikali ndani ya Wilaya ya Iringa mjini anae kiuka miiko na maadili ya Uongozi wa uma  na kukumbatia ufisadi unaweza nipa kwa njia ya siri kwa kupiga Namba 0743799726. Pia ninawasihi tuisome katiba ya chama chetu na kanuni zake ili tusiyumbe na tusimame kwenye ukweli daima fitina iwe mwiko na tusome  katiba ya Nchi yetu.
Aidha katibu huyo aliwahamasisha vijana kujiunga katika vikundi mbalimbali ili waweze kunufaika na fursa ya mikopo inayotolewa na serikali,ambapo kila kila Halmashauri imetenga %5 kwa ajili ya vijana na ili waweze kujikwamua kimaisha.
Hata hivyo katibu huyo alihitimisha kwa kusema kuwa moja ya majukumu ya vijana ni kujitoa katika  Shughuli mbalimbali za maendeleo, za kijamii ususani zile za kujitolea,hivyo aliwataka vijana wa chama cha Mapinduzi ccm Iringa mjini kujitoa kwa hali na mali pale wanapohitajika kujitolea katika shughuli za maendeleo.














0 maoni:

Chapisha Maoni