Jumatatu, 28 Agosti 2017

ABASIA YA MVIMWA WPATA ABATE MPYA

Posted by Esta Malibiche on August 28,2017 IN NEWS

Na Emanuel Mayunga Sumbawanga

WATAWA wa shirikala Mtakatifu Bernediko wa Abasia ya Roho Mtakatifu Mvimwa  WAMEPATA Abate mpya Padri Pambo Martin Mkorwe OSB.
Akiongoza Ibaada ya Misa Takatifu  kumuombea  Abate Pambo  Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga  Mhashamu Damian Kyaruzi amemuasa Abate Pambo kufuata mfano wa Mt. Pio wa X Papa, anayekumbukwa August 21 ambaye alijitoa kulihudumia Kanisa la Mungu bila kujibakiza.
Akiwashukuru wananchi na waamini wa jimbo la Sumbawanga abate Pambo OSB amemshukuru askofu na waamini kwa mapokezi na kumuombea na kuahidi kufanya kazi kwa moyo kadiri ya matakwa ya Mama Kanisa.
Abate Pambo atasimikwa August 26 mwaka huu katika Makao Makuu ya Shirika Mvimwa Parokiani Kate jimboni Sumbawanga .
Aidha Abate huyo amesema anaongozwa na kauli mbiu  DUC IN ALCUM (Tweka mpaka kilindini)

Historia  fupi Abate Pambo Martin-Angelica Mkorwe OSB

Abate Pambo Martin-Angelica Mkorwe alizaliwa tarehe 15/08/1975 huko Uwemba Mission, katika jimbo la Njombe, kwa baba Martin Mkorwe na Mama Angelica Samligo. Alipata Sakramenti za Ubatizo, Ekaristi Tatakatifu na Kipaimara katika Kanisa la Mtakatifu Rafaeli - Uwemba.
Kuazia mwaka 1983 – 1989 alipata elimu ya msingi katika shule za Myangayanga – Jimbo la Mbinga, Uwemba – Jimbo la Njombe na mwisho Ihalula – Njombe. Mwaka 1990 – 1996, akapata elimu ya sekondari katika Sekondari ya Njombe (NJOSS), na Irambo katika Jimbo la Mbeya.
Mara baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1996, alianza rasmi safari ya maisha ya Kitawa. Tar 11.07.1998, alifunga nadhiri za kwanza Mvimwa Monasterini. Kuanzia mwaka 1998 – 2005alipelekwa masomoni Morogoro kwa ajili ya majiundo ya Falsaka na Tauhidi katika Taasisi ya Wasalvatoriani.
Tarehe 22/08/2004, alifunga nadhiri za Daima – Mvimwa Abasiani. Tarehe 23 Octoba 2004, alipewa  Daraja Takatifu ya Ushemasi na Mhashamu Askofu Telesfor Mkude huko Salvatorian Institute – Morogoro. Tarehe 10/07/2005, alipewa Daraja Takatifu ya Upadri katika Parokia ya Kristo Mfalme - Sumbawanga na Mhashamu Damian Kyaruzi, Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga.
Mara baada ya kupadirishwa, alitumwa kufanya kazi katika Parokia ya Kristo Mfalme Sumbawanga mjini, kama Paroko  Msaidizi. Kuanzia mwaka 2008 – 2013, aliwekwa kuwa Paroko katika Parokia hiyohiyo ya Kristo Mfalme   Sumbawanga, na wakati huohuo alitumikia kama Mkuu wa Idara ya  Liturujia – Jimbo na Padri wa Kiroho wa Gereza la Sumbawanga mjini.
Tarehe 1 Julai 2013, alitumwa Roma kusomea Shahada ya Uzamili katika Sheria za Kanisa, ambako alihitimu mwezi Juni 2016. Tarehe 14/10/2016 Mkutano Mkuu wa XXI wa Shirika, uliyofanyika huko Sankt Ottilien - Ujerumani, ulimchagua Padri Pambo OSB kuwa Katibu wa Shirika la Wabenediktini Wamissionari, na hivyo akahamishia makazi yake huko Ujerumani.
Ametumikia wajibu huo kwa muda wa miezi minane tu, ambapo tarehe 7/6/2017 jamii ya Wamonaki wa Mvimwa walimchagua kuwa Abate wa III wa Abasia ya Roho Mtakatifu Mvimwa.Tarehe 25/8/2017, ameungama Imani na kula kiapo cha Uaminifu kwa Mama Kanisa Mtakatifu na tarehe 26/8/2017, Mhashamu Damian Kyaruzi amempa Baraka ya Uabate huko Abasiani Mvimwa.
Abate Pambo Martin Mkorwe osb ambaye Kauli-mbiu:ni  Motto DUC IN ALCUM (Tweka Mpaka Kilindini) Lk. 5:4 amekuwa ni abate wa tatu katika nyumba ya Abasia ya Roho Mtakatifu Mvimwa akitanguliwa na Abate Mstaafu Denis Ndomba OSB na hayati Abate Basil Ngaponda OSB.

0 maoni:

Chapisha Maoni