Ijumaa, 25 Agosti 2017

MKUU WA WILAYA YA MBULU AGAWA VITABU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI VYENYE THAMANI YA MIL.830.

Posted by Esta Malibiche on August 25,2017 IN NEWS

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mkoani Arusha Chekestino Mofuga akizungumza na walimu wa shule za Msingi wa Wilaya hiyo, waliofika ofisini kwake kuchukua vitabu.

 Mkuu Wa wilaya ya Mbulu chelestino s Mofuga Leo 25/8/2017 akiongea na walimu Wa wilaya hiyo waliofika kuchukua vitabu vya shule za msingi na sekondari . 
Mofuga amesema jumla ya Shule 180 za Msingi na Sekondari zitanufaika na Vitabu hivyo,ambapo,Shule za msingi  ni 150 na sekondari ni 36.
"Tani 22 ya vitabu vyenye thamani ya Tsh.830 MIL.nimevipokea kutoka mashirika rafiki ya children na bookaid international kwa kushirikiana na wabunge wa Mbulu ambao ni wadau wa Maendeleo hasa katika sekta ya Elimu nitahakikisha kila shule iliyopo wilayani kwangu inapata vitabu ili wanafunzi waweze kuvitumia katika madomo na hatimae Mbulu iweze kupiga hatua katika Elimu ikiwemo ongezeko la ufahuru"Alisema Mofuga.
Aidha Mofuga aliwashukuru wambunge wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu ambao ni.Zacharias paulo Isaay na Fratei masaay Kwa kuchangia kiasi Tsh.11 Mill.






0 maoni:

Chapisha Maoni