Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Alhamisi, 31 Agosti 2017

BANDARI KAVU YA KWALA –VIGWAZA KUANZA KUTUMIKA JANUARI MWAKANI

Posted by Esta Malibiche on August 31,2017 IN NEWS
1
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akifafanua jambo wakati akikagua mchoro wa Bandari kavu ya Kwala –Vigwaza Mkoani Pwani.
2
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Eng. Charles Salu Ogare anayesimamia ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza  Mkoani Pwani.
3
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Eng. Deusdedit Kakoko akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa bandari kavu ya Kwala –Vigwaza Mkoani Pwani.
4
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa mwenye kofia ya njano akiwa katika majukumu ya ukaguzi wa ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza inayojengwa mkoani Pwani.
5
Muonekano wa bandari kavu inayojengwa na mkandarasi Suma-KJT katika eneo la Kwala-Vigwaza inayotarajiwa kuanza kutumika Januari mwakani ikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Imetolewa na Kitengo cha  Mawasiliano Serikalini , Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
……………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala Vigwaza Mkoani Pwani na kumtaka mkandarasi Suma JKT kuongeza kasi na kuzingatia ubora.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo ameiagiza Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuhakikisha wanaunganisha kwa haraka ili reli na barabara zinazoingia katika bandari kavu hiyo zinakamilika na hivyo kuiwezesha bandari kavu hiyo kuanza kutumika ifikapo Januari mwakani.
“TPA, TRL na TANROADS uzuri wote mko kwenye wizara moja shirikianeni na hakikisheni kilomita 15 za barabara inayoingia kwenye bandari kavu hii na kilomita moja ya reli zinajengwa haraka,” Amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko kuhakikisha ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza unazingatia ubora na viwango vilivyopo katika mkataba ili kuiwezesha kuhudumia zaidi ya makontena milioni moja kwa mwaka na hivyo kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
“Hakikisheni eneo la bandari kavu linakuwa na maegesho ya kutosha, taa, maji ya uhakika, gari la zimamoto, uzio na mashine ya ukaguzi wa mizigo scanneritakayowezesha kupima kila mzigo unaopandishwa na kushushwa katika eneo hili,” amesisitiza Profesa Mbarawa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Kakoko amesema TPA imejipanga kuhakikisha ujenzi huo unatumia gharama nafuu na mifumo yote ya teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA inakuwepo katika bandari hiyo ili kuiwezesaha kufanya kazi kisasa na kwa ufanisi zaidi.
“Tukifanikiwa kuhamia hapa mzigo uliokuwa unasafirishwa kwa siku saba sasa utatumia siku tatu kufika Mwanza hali itakayovutia wasafirishaji wengi kutumia bandari ya Dar es Salaam na hivyo kukuza uchumi wa nchi na kuibua fursa za ajira,” amesema Eng. Kakoko.
Bandari Kavu ya Kwala –Vigwaza inayojengwa na Mkandarasi SUMA JKT ambapo takribani kiasi cha shilingi bilioni 9 kinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo ili kuboresha huduma za usafirishaji katika bandari ya Dar es Saalaam ambapo zaidi ya hekta 500 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo ambapo kwa kuanza hekta 120 sawa asilimia 24 zinajengwa katika awamu ya kwanza.

MWIGULU AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI UREJESHAJI WA WAKIMBIZI WA BURUNDI WALIO TAYARI KUREJEA NCHINI KWAO

Posted by Esta Malibiche on August 31,2017 IN NEWS
PIX 1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 2..
Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi,Pascal Barandagiye, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi, ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 3.
Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi  Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,Chansa Kapaya, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MANGULA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA CPC LEO

Posted by Esta Malibiche on August 31,2017 IN SIASA
Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula akimkaribisha Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole. (Picha na Bashir Nkoromo).

  Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philipo Mangula (kulia) akiongoza mazungumzo  baina yake na Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017.
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ujenzi ya IDCPC Kanda ya Afrika,  Wang Heming 
akipigapicha mandhari ya eneo kitakakojengwa Chuo Kikuu cha Viongozi wa Siasa cha Mwalimu 
Nyerere, Kibaha mkoa wa Pwani, alipotembelea eneo hilo, jana, Agosti 30, 2017. Kushoto ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinza. (PICHA NA BASHIR NKOROMO).

TAARIFA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA KUHUSU KUBADILISHA FEDHA

Posted by Esta Malibiche on August 31.2017 IN NEWS


bot
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kupuuza taarifa zinazozunguka katika mitandao ya kijamii kwamba kutakuwa na ‘mabadilisho ya fedha zote za zamani kuanzia tarehe 04/09/2017 hadi tarehe 01/12/2017’.
Taarifa hizo ni za uongo na hazijatolewa na Benki Kuu ya Tanzania. Wananchi mnaombwa kuendelea na taratibu zenu za kawaida za kufanya miamala yenu mbalimbali kwa kutumia fedha zetu kama kawaida.
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania inawaasa watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia vizuri nyenzo hiyo ya kupashana habari na kuacha kuzusha uongo ambao unaleta usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.
Imetolewa na:
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
Barua pepe: info@bot.go.tz
Simu: +255 22 2233167

Jumatatu, 28 Agosti 2017

MKUU WA WILAYA YA IKUNGI MKOANI SINGIDA AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU 69

Posted by Esta Malibiche on August 29,2017  IN MICHEZO


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji J. Mtaturu akionyesha moja ya mipira aliyoigawa kwa timu shiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama "IKUNGI ELIMU CUP 2017"


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji J. Mtaturu akifungua mipira aliyoigawa kwa timu zote shiriki za mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama "IKUNGI ELIMU CUP 2017"

Baadhi za jezi zilizotolewa kwa ajili ya timu zote shiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama "IKUNGI ELIMU CUP 2017" 
 
Na Mathias canal, Singida

Takribani timu 69 zinazoshiriki mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama “IKUNGI ELIMU CUP 2017”zimekabiziwa jezi pamoja na mipira kwa ajili ya utimilifu wa kuwa na vifaa vya michezo kwenye mashindano hayo jambo ambalo limeibua hisia chanya kwa kila timu kutaka kuibuka mshindi.

Akitoa vifaa hivyo vya michezo kwa ajili ya ushiriki wa timu hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa Ofisi yake kwa ushirikiano mkubwa na wadau wa elimu na wananchi kwa ujumla wamechangia vifaa hivyo vya michezo ikiwa ni sehemu ya kuongeza chachu ya hamasa katika mashindano na kufikisha zaidi ujumbe wa umuhimu wa waanchi kuchangia mfuko wa elimu.

Mashindano hayo yanayoshadihishwa na kauli mbiu isemayo CHANGIA, BORESHA ELIMU IKUNGI yanafanyika katika vijiji vyote 101 ambapo katika Jimbo la Singida Magharibi lenye kata 15 kila Kata itatoa timu mbili na Jimbo la Singida Mashariki lenye Kata 13 kila kata itatoa timu tatu hivyo kuwa na timu 69 zitakazopambana na kupatikana timu tatu bora.

Mhe Mtaturu alisema kuwa kunzishwa kwa mashindano hayo ni kusudio la kuifanya jamii kujihusisha na shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na serikali, kuibua vipaji vya michezo katika Wilaya ili kukuza ajira na kufanya vijana waachane na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Sababu zingine ni Kuunganisha jamii kuwa kitu kimoja hatimaye vijana na wananchi kuimarisha upendo, ajira na afya sambamba na kudumisha amani na mshikamano.

Mashindano hayo yanataraji kufika ukomo Septemba 19, 2017 huku zawadi zikitaraji kutolewa kwa washindi watano ambapo mshindi wa kwanza atapatiwa zawadi ya Kombe, Seti ya jezi, Mipira miwili na kitita cha shilingi 1,000,000/= , na mshindi wa pili atapatiwa Seti ya jezi, Mipira miwili na shilingi 750,000/=.

Mshindi wa tatu atapatiwa Mipira miwili na shilingi 450,000/= , Mshindi wa nne atapatiwa Mpira mmoja na Shilingi 200,000/= huku mshindi wa tano akipatiwa Mpira mmoja na Shilingi 100,000/=.

Aidha, kutakuwa na zawadi zingine kwa timu yenye nidhamu, Zawadi ya mfungaji bora, Zawadi ya Kipa bora, Zawadi ya mchezaji bora, huku wachezaji wengine 30 wakichaguliwa kuingia kambini kufundishwa mbinu za uchezaji bora.

Katika taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Mhe Dkt Rehema Nchimbi, alisema kuwa Idara ya elimu katika Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa nyumba za walimu, Upungufu wa Walimu, Maabara ya Masomo ya sayansi kwa shule za sekondari, pamoja na vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

Hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa ushirikiano na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo walianzisha mfuko wa elimu wilaya kwa mujibu wa sheria ndogo ya Halmashauri Wilaya ya Ikungi ya mwaka 2014 ambayo ilitolewa katika tangazo la serikali Na. 222 la tarehe 11 Julai, 2014 ili kuweza kukabiliana na changamoto za elimu ambazo zinaathiri mafanikio ya elimu katika Wilaya hiyo.

Kuanzishwa kwa mfuko wa elimu kumepelekea pia kufunguliwa kwa akaunti ya mfuko katika Benki ya NMB tawi la Ikungi kwa jina la Mfuko wa Elimu wa Wilaya ya Ikungi (Ikungi District Education Funds) akaunti Namba 52510000554.

Hata hivyo Mhe Mtaturu alitoa Rai kwa wadau wa elimu kuchangia mfuko wa elimu ili kukuza ufanisi wa elimu katika Wilaya hiyo ambao kwa kiasi kikubwa unategemea zaidi upatikanaji wa rasilimali fedha na nguvu kazi kutoka kwa wadau, wananchi, Taasisi, Mashirika, Makampuni mbalimbali yaliyopo ndani na nje ya nchi.

MKUTANO MKUU WA 17 WA SHIRIKISHO LA MASISTA WAKATOLIKI NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI (ACWECA).

Posted by Esta Malibiche on August 29,2017 IN NEWS

Na Pascal Mwanache

Mkutano huo umefunguliwa Agosti 26, 2017 kwa Misa Takatifu iliyoongozwa na Rais wa Baraza la Kipapa la Maisha ya waliowekwa wakfu Mwadhama Joao Kardinali Braz de Aviz kutoka Vatikani.

Katika Misa Takatifu ya ufunguzi wa mkutano huo Kardinali Joao amewaasa watawa wanaounda shirikisho hilo kutomezwa na tama ya fedha katika utume wao na badala yake wajikite katika kutoa huduma bila kutegemeamalipo ya hapa duniani.

Mkutano huo wa unatarajiwa kufanyika hadi Septemba 2, 2017 katika kituo cha mikutano cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Kurasini jijini Dar es salaam.

Umoja huo unaundwa na nchi 9 ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi, Zambia, Ethiopia, Sudani ya Kusini, Sudani na Eritrea. Baadhi ya wageni waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo ni pamoja na Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda Mhashamu Renatus Nkwande, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa, na Balozi wa Papa nchini Askofu Mkuu Marek SolczyÅ„ski.






















PITIA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO AUGUST 29,2017

Posted by Esta Malibiche on August 29,2017 IN KITAIFA