Posted by Esta Malibiche on APRIL 4,2017
Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Faisal Shabhai
akizungumza kwenye viwanja vya shule ya msingi Songambele Mji mdogo wa
Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, alipoahidi wananchi
kuwajengea
vyumba saba vya madarasa.
Mkazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara,Japhary Matimbwa akiushukuru uongozi wa kampuni ya TanzaniteOne
baada ya kuahidi kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani
Manyara,Jackson Sipitieck akiushukuru uongozi wa kampuni ya TanzaniteOne
baada ya kuahidi kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele.
…………….
Kampuni ya TanzaniteOne kujenga
madarasa saba ya shule ya msingi Songambele ya Mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Faisal Juma Shabhai
ameahidi kujenga madarasa saba ya shule ya msingi Songambele ya mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambayo yameweka
ufa.
Tangu mwaka 2013 madarasa hayo yaliweka ufa kutokana na kupitiwa na
mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kwenye eneo hilo.
Kutokana na hali hiyo uongozi wa shule hiyo uliamua
kuyafunga madarasa hayo na ofisi ya walimu, wakihofia kupaata madhara
kutokana na hitilafu hiyo iliyotokana na tatizo hilo.
Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Shabhai alisema yeye
binafsi atajenga madarasa matatu na wakurugenzi wenzake wa kampuni hiyo
Hussein Gonga na Riziwani nao watajenga mengine manne yaliyobakia.
Alisema kampuni hiyo imeamua kujenga madarasa hayo ili
kusaidia jamii inayozunguka maeneo hayo ambayo wao wamewekeza kwenye
madini ya Tanzanite.
“Pamoja na hayo jamii ya eneo hili nanyi mnapaswa kutuunga
mkono kwa kutumia nguvu zenu ikiwemo kubeba majabali, matofali na
kusogeza mchanga ili tushiriki pamoja,” alisema Shabhai.
Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Simanjiro Jackson
Leskar Sipitieck aliipongeza kampuni ya TanzaniteOne kwa kufikia uamuzi
huo kwani utasaidia watoto wa eneo hilo kupata elimu.
“Mwezi huu kutakuwa na baraza la madiwani na kupitia nafasi
hiyo tutatoa shukurani zetu rasmi kwa kutuunga mkono baada ya kujenga
madarasa hayo saba ya shule hiii ya Songambele,” alisema Sipitieck.
0 maoni:
Chapisha Maoni