Posted by Esta Malibiche On APRIL 24,2017 IN NEWS
Na Esta
Malibiche
Iringa
Mwenge wa
uhuru umezindua miradi 7 ya Maendeleo yenye thamani ya Bill..3,597,714,040.00
katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa.
Akisoma
risala ya utii wa Mwenge wa uhuru 2017 kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Mufindi Riziki Shemdoe alisema kuwa Miradi
iliyozinduliwa,kukaguliwa na kuwekewa jiwe la Msingi nipamja na barabara iliyopo kata ya Maduma,Mradi
wa Maji ,Shamba la mahindi yalitolimwa nawanafunzi wa shule yaMsingi Maduma kwa ajili ya chakula cha mchana,ujenzi wa kituo cha Afya Maduma,Club
ya kupambana na Rushwa katika shule ya sekondari ya wasichana Mufindi,pamoja na
kiwanda cha kuchakata Mbao kilichopo Nyololo.
‘’’Mheshimiwa Rais, Wananchi wa Halmashauri ya
wilaya ya Mufindi,wametekeleza miradi ya Maendeleo ambayo baadhi yake
imefunguliwa,kuwekewa jiwe la msingi,kuzinduliwa na kukaguliwa na kiongozi wa
mbio za Mwenge wa uhuru 2017.Jumla ya miradi 7 imepitiwa na Mwenge wa
uhuru,ambapo jumla ya gharama ya miradi yote ni Tsh. 3,597,714,040.00.Alisema
Shemdoe
‘’’Mheshimiwa
Rais,Halmashauri ya wilaya imechangia tsh.48,000,000,00,Serikali kuu imechangia
Tsh.265,884,040.00,Wananchi wamechangia Tsh.103,137,000.00 pamoja na wadau na
wahisanimbalimbali Tsh.3,181,00,000.00,vile vile wananchi na wadau mbalimbali
wamechangia fedha taslimu kiasi cha
Tsh.18,639,300 ikiwa nipamoja na vitu
halisi na nguvu zao kwa ajili ya
kufanikisha mbio za Mwenge wa uhuru mwa huu 2017.Pia kiasi cha Tsh.5880,800.00
Zimeelekezwa katika miradi ya maendeleo
ya wananchi’’Alisema Shemdoe
Aidha
akizungumzia swala la uwezeshwaji kwa vijana wilayani humo alisema kuwa, jumala ya vijana 4225
wamejiunga na vyama vya kilimo 6 vilivyopo kwenye ngazi ya kata kupitia skimu
za Mgololo, Igomaa,Ikweha,Mkonge block Tea Farm,Sawala block Tea na Mtambula
AMOCOS.
‘’Mheshimwa
Rais,kutokana na Takwimu za sense ya
Taifa ya mwaka 2012,Halmashauri ya Mufindi inakadiliwa kuwa na jumla ya vijana 148,450[Me 76,298 na Ke 72,152]
ambao ni nguvu kazi ya Taifa sawa na
asilimia 53 ya wakazi wote,hadi sasa vijana 2,118 wamenufaika na mikopo yenye
thamani ya Tsh. 2,102,469,121 kuroka Tanzania Agricultural Development BANK
[TADB] na hali ya marejesho imefikia Tsh. 1,759,832,761 sawa na asilimia 83.70’’’Alisema Shemdoe.
Alisema kuwa
ili kuendelea kujenga uwezo wa mfuko wa maendeleo ya vijana,Halmashauri imenga
fedha kiasi cha Tsh.169,316,500.00 sawa na asilimia 5 ya mapato ya ndani kwa
mwaka huu wa fedha 201|2017 hadi kufikia
Aprili 2017 jumla ya Tsh. 150,00,00.00 zimekopeshwa kwa vikundi vya vijana sawa
na asilimia 88.6 ya kiasi kilichotengwa,ambapo zaidi ya vijana 1,206 wakiwa
katika vikundi wamenufaika.
Kwa upande
wake kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Amour Hamad Amour akizungumza na wananchi wa wilaya ya Mufindi
mara baada ya kupokea Risala ya utii
katika mkesha wa mbio za mwenge uliofanyika kwenye viwanja vya NYololo
aliwasihi wananchi kuunga mkono kwa vitendo juhudi zinazofanywa na serikali ya
awamu ya Tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kuanya kazi kwa bidii ili
Taifa liweze kusonga mbele kiuchumi.
Amour
alisema kuwa serikali imedhamilia
kuanzisha viwanda vidogovidogo,vya kati na viwanda vikubwa kwa kutumia
rasilimali zinazopatikana hapa nchini,ambavyo vitasaidia kuongeza thamani ya
mazao yanayozalishwa, hususani rasilimali zina zopatikana na kilimo,ufugaji na uvuvi na hatimae
kuongeza ajira kwa watanzania.
‘’Kauli mbiu ya Mwenge wa uhuru ya mwaka huu
2017 inasema ‘Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya ya Nchi
Yetu’Hivyo basi Mheshimwa Rais anataka
Taifa liondokane na uvivu ndiyo maana anahamasisha kila mwanmanchi ashiriki
katika kukuza chumi wa viwanda kwa kuwataka wawekezaji kuanzisha viwanda vitakavyotumia malighafi
zilizopo nchini’’’Alisema Amour.
Aidha
aliwasihi wananchi ku dumisha
Umoja ,Amani,Upendo pamoja na mshikamano kama ulivyoasisiwa na
baba wa Taifa na kusema kuwa ili Taifa liweze kusonga mbele kimaendeleo na
kupiga hatua kiuchumi Amani inatakiwa kuwepo.
0 maoni:
Chapisha Maoni