Kiongozi wa mbio za mbwenge wa Uhuru kitaifa Amour Hamad Amour akizindua
mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya katika kijiji cha Maduma kata ya
Mbalamaziwa wilayani Mufindi jana.
Na Esta
Malibiche
Iringa
Kiongozi wa
mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour Hamad Amour amewataka viongozi kusimamia kwa ungalifu miradi ya maendeleo
inayotekelezwa iwe na ubora unaotakiwa ,ikamilike kwa wakati na ijengwe kwa
kiwango kinachotakiwa kulingana na kiasi
cha fedha kinachotolewa.
Kauli hiyo
ameitoa jana wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya katika kijiji cha Maduma kata ya Mbalamaziwa, unaojengwa
kwa nguvu za wananchi kwa kushrikiana na serikali ambayo mpaka kukamilika kwake utasaidia kuwahudumia wakazi zaidi ya 6,158 pia itasaidia kupunguza
Msongamano wa wagonjwa katika Hospital ya Wilaya ya Mufindi.
Pamoja na
kweka jiwe la msingi katika zahanati hiyo,aligawa vyandarua 80,kwa watoto
wadogo na akina mama wajawazioto kujikinga na mbu waenezao malaria
alikagua barabara inayoendelea kutengenezwa, alizindua mradi wa maji safi
na salama amoja kukagua shamba la mahindi lenye ulefu hekali 7 lilimwa na wananfunzi wa sshuke ya msingi
Maduma kwa ajili ya chakula cha Mchana.
‘’’Ninaziomba
shule zote Nchini kuiga mfano
huu,ili wanafunzi waweze kupata chakula cha Mchana wawapo shuleni.Mradi huu ni
Mzuri na unahitaji uendelezwe kwa shule zote nchini .Tusiiachie serikali pekee
na wazazi wakati wanafunzi wanaweza kutumia muda kidogo kuazalisha
chakula’’’Alisema Amour
Aidha
kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kitaifa aliweka jiwe la Msingi katika kiwanda
cha Leshe Investment kinachojishugulisha na kuchakata nguzo za umeme kilichopo
Nyololo,alizindua Klabu ya wapinga Rushwa
katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mufindi.
Akisoma
Taarifa ya Mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya kilichopo kata ya Mbalamaziwa
Neema Kyando alisema kuwa, mpaka kukamilika kwa ujenzi huo kutagharimu kiasi cha
Tsh.600,000,000.00,ambapo mpaka sasa majengo ya jengo la mapokezi
[OPD]umefanyika ,ujenzi wa nyumba za watumishi naendelea kufanyika kwa lengo la
watoa huduma katika kituo hichokuwa karibvu na kiutuo cha Afya.
Kyando
alisema Lengo la Mradi huo ni kuboresha huduma za Afya katika kata ya
Mbalamaziwa ikiwa ipamoja na Afya ya mama na Mtoto.
''Ndugu
kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa,Thamani ya Mradi huu mpaka sasa ni
Tsh.148,123,500.00,ambapo ujenzi wa mapokezi ya wagonjwa umegharimu kiasi cha
Tsh.132,580,000.00 ikiwa mchango wa wananchi ni Tsh.32,947,000.00,Halmashauri
ya wilaya Tsh.48,000,000.00,Serikali kuu Tsh.43633,00.00 na
wahisaniTsh.8,000,000.00.Ujenzi wa nyumba za watumishi wa Afya umegharimu jumla
ya Tsh.15,543,500.00 ikiwa mchango wa wananchi ni Tsh.11,543,500.00 na Serikali
kuu Tsh.4,000,000.00 ''Alisema Kyando
Awali mkuu
wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Willium akipokea Mwenge wa uhuru wilayani humo
alisema kuwa ujio wa MWenge wa uhuru wilayani shughuli za Maendeleo kwa kuwaingia kipato wafanyabiashara katika
maeneo ambayo utapita kukagua,kuzindua na kufungua miradi ya Maendeleo.
Jamhuri
aliipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kuunga mkoano juhudi zinazofanywa na
Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania Dkt.John Pombe Magufuli kwa
jitihada zake za kukusanya mapato kwa kila ngazi na kufanya matumizi yenye tija
kwa Jamii na Taifa kwa ujumla.
‘’’Hii
imeuthibitishia umma wa Watanzania kwamba,wewe ni kiongozi Mzalendo mwenye azma
ya kweli ya kuwaunganisha Watanzania dhidi ya Mapambano ya Rushwa,mapambano
dhidi ya dwa za kulevya,Mapamabano dhidi ya Ukimwi na Malaria.Tunakuhakikishia
kwamba tutaendelea kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali,viongozi wa dini
na wadu wa Maendeleo katika kuhakikisha kuwa,kazi iliyop mbele yetu ni
kuhamasisha,kufanyakazi kwa juhudi na maarifa,ili kutimiza mbiu ya Serikali ya
awamu ya Tano ya HAPA KAZI TU
Hata hivyo Taarifa ya ujenzi wa barabara ya Maduma- Tambalang’ombe Patrick Mwihava
alisema Matengenezo ya barabara hiyo ni mkakati wa HALMASHAURI YA WILAYA YA
Mfindi,ambayo imejipanga kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bira za usafiri mna usafirishaji bila matatizo.
Mwihava
alisema barabara hiyo imetengenzwa kwa awamu mbili,ambapo awamu ya kwanza jumla ya kilimota kumi zitafanyiwa
matengenezo kwa kiwango cxa changarawe
na mkandarasi aliyepewa tenda ni kampuni ya M/s Willyfres Enterprise Ltd
wa Iringa kwa gharama ya Tsh.151,781,040.00 na anatarajia kukamilisha kazi hiyo
tarehe 25/5/2017.Pia kwa awamu ya pili itatengenezwa kilomota kumi.
Ndugu
kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Kukamilika kwa ujenzi wa barabara hii
kutaleta mafanikio makubwa katika kuunganisha maeneo ya kata ya maduma ma
Malangali zenye wakazi wapatao 17,828 kwa mujibu wa Sensa ya wanaokwenda kupata huduma katika kituo cha
Afya cha Malangali na kufika katika
Gulio la Tanmbalang’ombe’’’’Alisema
Mwihava.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni