Posted by Esta Malibiche on APRIL 4,2017 IN NEWS
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William
akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida Ndugu Andrew W. Massawe
wakati alipofanya ziara Wilaya ya Mufindi
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ndugu Andrew W. Massawe yuko mkoani
Iringa kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu; ambapo pamoja
na mambo mengine anatazamiwa kushuhudia sherehe za uzinduzi wa utoaji Vitambulisho
vya Taifa kwa wananchi wa Wilaya ya Mufindi na kuzinduliwa kwa kampeni ya Usajili
wa wananchi na wageni wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wanaoishi mkoani
humo.
Katika ziara yake; leo
amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, ambaye amemweleza
Mkurugenzi huyo hatua kubwa ambayo Wilaya yake imefikia mpaka sasa katika
kuwasajili wananchi, ambapo takribani asilimia 60 ya wananchi wameshasajiliwa,
kuchukuliwa alama za vidole na baadhi Vitambulisho vyao kuzalishwa, mbali na
kukamilika kwa zoezi la kuwasajiliwa Watumishi wa Umma.
Akiwa Wilayani Mufindi
Mkurugenzi huyo ametembelea na kukagua shughuli katika ofisi ya Usajili na kukagua
vifaa vinavyotumika katika Usajili. Aidha; amefanya mazungumzo na wadau wakubwa
wa NIDA likiwemo Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Mafinga namba 841,
kinachoongozwa na Kanali Hamisi Maiga; ambaye amehakikishia NIDA ushirikiano
zaidi katika kufanikisha zoezi la kuwasajiliwa wananchi.
Mkurugenzi huyo pia
alitembelea Kata za Boma na Upendo na kukutana na watendaji wa Kata hizo pamoja
na kufanya mazungumzo na Diwani wa Kata ya Boma Mhe. Julist Kisoma (Chadema) ambaye
ameishukuru NIDA kwa kufanikisha zoezi la kuwasajili wa wananchi.
Mbali na kukagua shughuli
za Usajili Wilaya ya Mufindi; pia amekutana na Katibu Tawala wa Wilaya ya
Iringa bwana Joseph Meshacky Chitnka ambaye alieleza mikakati ya Wilaya yake
katika kuhakikisha watu wote wanafikiwa kwa wakati kusajiliwa na kupata
Vitambulisho vya Taifa.
Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa ilianza utekelezaji wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa mara ya
kwanza mkoa wa Iringa mwezi Septemba, 2016 kwa kuanza na kuwasajili Watumishi
wa Umma zoezi lililomalizika hivi karibuni na kuanza mikakati ya kuwasajili
wananchi na Wageni.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William
(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndugu
Andrew W. Massawe (katikati kulia), wengine wa kwanza kushoto ni ndugu Alphonce
Malibiche Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na wa
kwanza kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya
Mufindi Ndugu Bernard.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Wilaya
ya Mufindi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA;
Ndugu Andrew W. Massawe
Ndugu George Mushi Afisa Usajili Mkoa wa Iringa (RRO),
akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, kuhusu vifaa vinavyotumika
kwenye usajili wa wananchi alipotembelea ghala la kuhifadhi vifaa wilayani
Mufindi
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA akiwa na Kanali Hamisi
Maiga Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Mafinga namba 841, wakati
alipotembelea kambi hiyo.
Mtendaji wa Kata ya Boma; Joseph Kiwele akitoa taarifa
ya utekelezaji wa zoezi la usajili wananchi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndugu Andrew W. Massawe
akisalimiana na Diwani wa Kata ya Boma Mhe. Julist Kisoma (Chadema).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Andrew W. Massawe
akiweka saini kwenye ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa bwana Joseph
Meshacky Chitinka wakati alipofanya ziara.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
NIDA (Katikati) akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa bwana Joseph Meshacky
Chitinka (katikati kulia). Wengine ni Ndugu Alphonce Malibiche Kaimu Mkurugenzi
Uzalishaji Vitambulisho (wa kwanza kushoto) na
wa kwanza kulia ni ndugu George Mushi, Afisa Usajili Mkoa wa Iringa.
0 maoni:
Chapisha Maoni