Posted by Esta Malibiche on APRIL 26,2017 IN NEWS
Na Esta Malibiche
Kilolo
HALMASHAURI ya wilaya ya Kilolo Mkoani
Iringa,katika kutekeleza kauli mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2017
inayosema 'Shiriki uchumi wa viwanda kwa Maendeleo ya Nchi yetu imeadhimia
kuongeza viwanda vidogo vidogo ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kipato cha
kati ifikapo 2025.
Akisoma risala ya utii jana kwa Mh.Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Katibu tawala wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Yusuph
Msawanga alisema kuwa,kutokana na Serikali ya awamu ya tano kudhamiria Tanzania
iwe Nchi ya viwanda Halmashauri hiyo imetenga maeneo yenye ukubwa
wa ekari17,819.91 katika eneo la Lundamatwe,Ilula,Luhanga.Dabaga na Luganga
kibaoni kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.
Msawanga alisema kuwa kwa sasa
wilaya hiyo inajumla ya viwanda 17 vinavyojihusisha na shuguli mbalimbali
zikiwemo usindikaji wa mbao,ukamuaji wa mafuta ya alizeti,usindikaji wa Jam na
juisi, pamoja na kiwanda cha usindikaji Maji ya kunywa.
‘’’Mh.Rais sisi wananchi wa wilaya ya Kilolo
tunakupongeza kwa wewe pamoja na Serikali ya awamu ya Tano kwa kuliongoza Taifa
kwa Amani, Upendo, Utulivu na Mshikamano wa Taifa.Pia tunakupongeza katika kuhakikisha vijana wanashiriki katika uchumi wa
viwanda,kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali,kusimamia utendaji kazi katika
utumishi wa umma,kutekeleza mapambano dhidi ya Rushwa,Madawa ya kulevya,Malaria pamboja na Maambukizi ya vvu\ukimwi’’’’Alisema
Msawanga.
Akizungumzia
uimarishaji na uwezeshaji wa vikundi vya vijana na wanawake katika
uzalishaji mali alisema wilaya hiyo ina jumla ya vikundi 89, vya vijana
vinavyojihusisha na uzalishaji mali vyenye idadi ya wanachama 2,507.Pia vikundi
nane vimetoa ajira kwa vijana 73.
Aidha alisema Mwenge wa uhuru mwaka 2017
wilayani kilolo umezidua ,kuweka mawe ya msingi na kukagua miradi ya Maendeleo katika sekta ya Afya,
Elimu,Kilimo,Maji,Maendeleo ya Jamii,Mazingira na Taasisi ya kuzuwia na
kupambana na Rushwa Takukuru,jumla ya ikiwa na thamani ya Bill.2,055,857,050.00
,
Aliongeza kuwa katika utekelezaji wa kauli
mbiu za kudumu Mapambano dhidi ya vvu\ukimwi kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo wilaya imetekeleza kwa kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi
dhidi ya ukimwi katika kata zote 24 ikiwemo upimaji wa hiari,matumizi sahihi ya
kondomu pamoja na kuwahamasisha kutumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi na
matunzo kwa wanaoishi na vvu.
Mheshimiwa Rais,Mapambano dhidi ya dawa za
kulevya kipindi cha kuanzia julai2016 hadi April 2017 wilaya imetekeleza kauli mbiu isemayo ‘Tuwajali
na kuwasikiliza watoto na Vijana’kwa
kuendesha misako ya kubaini waingizaji,watumiaji ,wauzaji na wasambazaji wa
coceini kwa,Mandrax,Heroine na pombe zilizohifadhiwa kwenye viroba,wamiliki wa
mashamba ya bhangi ambapo jumla ya kilogram 23 na gram 60 za bhangi kavu,puli 1
na kete 266 viliakamtwa na kesi zipo mahakamani.’’’Alisema Msawanga.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa
uhuru kitaifa,Amour Hamad Amour akizungumza wanafunzi wa shule ya sekondari Ilula,alisema kuwa ili Taifa liweze kuwa na viongozi wazuri
wenye kuleta Maendeleo lazima wananfunzi ambao ni viongozi wajao wajitume kwa
juhudi zote na kufanya bidii katika
masomo yao.
Vitendo vya Rushwa vimeenea katika Taasisi
mbalimbali Nchini,tumieni Elimu mnayoipata kukemea vitendo hivyo,muwaheshimu
wazazi,Viongozi,walimu,pamoja na kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo yenu ya
baadae’’’’Alisema Amour.
Nae mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah
akizungumzia Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria wilayani humo alisema kuwa,
ugonjwa wa malaria umekuwa ni miongoni mwa
magonjwa yanayoongoza kwa kuathiri watu wengi wilayani,hivyo kutokana na
kauli mbiu yam bio za mwenge wa uhuru 2017 inayosema ‘shiriki kutokomeza
Malaria kabisa kwa Manufaa ya Jamii’’aliahidi kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi juu ya usafi wa Mazingira ili wawezekujikinga
na ugonjwa wa Malaria.
Bi.Asia
Abdalah aliipongeza Serikali ya awamu ya Tano
kwa kuunga mkoano juhudi zinazofanywa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanazania Dkt.John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kukusanya mapato kwa
kila ngazi na kufanya matumizi yenye tija kwa Jamii na Taifa kwa ujumla.
‘’’Hii
imeuthibitishia umma wa Watanzania kwamba,wewe ni kiongozi Mzalendo mwenye azma
ya kweli ya kuwaunganisha Watanzania dhidi ya Mapambano ya Rushwa,mapambano
dhidi ya dwa za kulevya,Mapamabano dhidi ya Ukimwi na Malaria.Tunakuhakikishia
kwamba tutaendelea kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali,viongozi wa dini
na wadu wa Maendeleo katika kuhakikisha kuwa,kazi iliyop mbele yetu ni
kuhamasisha,kufanyakazi kwa juhudi na maarifa,ili kutimiza kauli mbiu ya
Serikali ya awamu ya Tano ya HAPA KAZI TU.
0 maoni:
Chapisha Maoni