MASHINDANO ya mbio za magari yanatarajia kufanyika mkoani Iringa kuanzia jumamosi April 22-23 mwaka
huu,ambapo madereva 20 wanatarajia kushiriki mashindano hayo yatakayopambwa na
ngoma mbalimbali.
Akizungumza na wandishi wa habari
jana,Mwenyekiti wa Club za mbio za magari mkoa wa Iringa Hamid Mbata alisema
kufanyika kwa mashindano hayo kutaibua fursa nyingi mkoani hapa ikiwa nipamoja
na kuongeza kipato katika sekta ya utalii na wafanyabiashara kutokana na
wageni kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi watakaoshiriki na kushuhudia
mashindano hayo.
"" Kwa siku mbili hizo
Mkoa wetu wa Iringautanyenyuka kiuchumi kwa wafanyabiashara na katika sekta ya
utalii kutokana na vivutio vingi vizuri vilivyopo lakini havitambuliki kutokana
na kutotangazwa,kupitia mashindano haya tutautangaza mkoa wa Iringa na vivutio
vilivyopo pia wageni watakaoshiriki na kushuhudia watapata nafasi ya kutembelea
vivutio vilivyopo na hivyo kuliingizia Taifa
pato."""Alisema Mbata.
Mbata alisema kuwa umbali wa km 302
zitatumika katika mashindano hayo na washindi watatu watakaopatikana watapewa
zawadi ya vikombe kuanzia mshindi wa kwanza hadi wa tatu miaka.
"" Zaidi ya miaka kumi
iiliyopita ndipo tulipopata nafasi ya kushiriki madhindano haya ya mbio za
magari,ninapenda kuwaahidi wananchibwa mkoa wa Iringa na watanzania kwabujumla
kuwa tumejipanga vuzuri kuhakikisha tunafanya vizuri""Alisema Mbata.
Mbata aliwataka wananchi mkoani
Iringa na nje ya mkoa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano hayo huku
wakiwataadhari ya kukaa mbali na barabara zitakazotumika kutokana na mwendo
kasi wa mashindano hayo.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa
usalama barabarani mkoa wa Iringa Stive Nyandongo aliwataka washiriki
kuzingatia swala la usalama barabarani huku wakizingatia kanuni na kutii
sheria zake zilizowekwa.
Nyandongo akisema washiriki
wanapaswa kuweka usalama wao kwanza wakati wote watakaokuwa wanaendesha magari
hayo na usalama wa raia watakaoshuhudia mashindano hayo ili kujiepusha na
madhara yanayoweza kutokea kutokana na kutozingatia swala zima la usalama barabarani.
"Sisi kama polisi tumejipanga
vizuri katika kusimamia mashindano haya na kuhakikisha tunaimarisha ulinzi na
zoezi hili linamalizika kwa Amani bila kutokea vurugu za aina yeyote.Tunawaomba
wananchi ambao wanashi katika barabara zitakazotumika katika mashindano haya
wachukue tahadhari wao na mifugo yao sababu magari yatakuwa yanaendeshwa kwa
mwendo kasi.Mifugo na watoto wadogo wasiwepo barabarani,waendesha
pikipiki(bodaboda)nao wawe makini au wasitumie kwa muda barabara zitakazotumika
katika mbio hizo.""" Alisema Nyandongo
Awali mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akizungumzia mashindano hayo
aliwataka wananchi kuwa waangalifu kwa maeneo yatakayotumika kutipita mbio
hizo.
""" Pamoja na kuyapokea mashindano kwa mikono miwili
lakini yanahatari kubwa kwa watoto waliochini ya miaka 15.Ninawaomba wazazi
mhakikishe mnawalinda watoto ili wasipate madhara sababu ya magari ya
mashindano hayo kutembea kwa mwendo kasi."""Alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuunyenyua mkoa wa Iringa na
kutangaza vivutio vilivyopo ili mashindano ya mbio za magari kwa Afrika na
dunia yaje kufanyika mkoani Iringa.
"Ombi kwa wananchi wa mkoa wa Iringa,wajitokeze kwa wingi kushuhudia
mashindano hayo huku wakiwa na taadhari ya kukaa mbali na barabara
zitakazotumika.""" Alisema Kasesela
0 maoni:
Chapisha Maoni