Posted by Esta Malibiche on APRIL 20,17 IN NEWS
KAMPUNI ya Makota Forest ya
inayojihusisha na shughuli za Kilimo katika kata
ya Ihimbo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imetoa
msaada wa bati 100 pamoja na madawati 20 kwa ajili ya
kuunga mkono serikali ya wilaya ya Kilolo ya
ujenzi wa vyumba vya madarasa .
Akizungumza leo [jana]
wakati wa kukabidhi msaada huo kwa mkuu
wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah ,Mkurugenzi mtendaji
wa kampuni hiyo Bharat Bhesania alisema kuwa kampuni yake itaendelea
kusaidia shughuli mbali mbali za kimaendeleo katika wilaya
ya Kilolo na maeneo mengine ya mkoa wa Iringa .
Bhesania alisema kuwa
jitihada zinazofanywa na viongozi wa wilaya ya Kilolo na mkoa wa
Iringa katika kuwaletea wananchi maendeleo ni jitihada ambazo
zinapaswa kuungwa mkono na wadau wote wa
maendeleo ndani ya mkoa huo na waliopo nje
ya mkoa .
" Sisi kama
wawekezaji tunaowajibu wa kuunga mkono
shughuli zote za kimaendeleo zinazoendelea katika
maeneo yetu ....nimekuwa nikisaidia shughuli nyingi sana na
sichoki kuendelea kusaidia "Alisema Bhesania
Kwa pande wake Meneja wa
kampuni Gibson Mkuvalwa
alisema kampuni yake inajihusisha na kilimo cha
mahindi na mwaka huu ndipo shamba hili limeanza
ila changamoto kubwa wanayokutana nayo ni kodi kubwa
wanayolipa na kuomba serikali kuweza
kuliangalia hilo.
Mkuvalwa alisema kupitia
kampuni hiyo wameweza kutoa ajira kwa
wananchi wanaozunguka kampuni hiyo na
wamekuwa wakijitolea kutengeneza barabara
na kushiriki kwa nguvu zote kuunga mkono
shughuli za kimaendeleo .
Nae Mkuu wa wilaya ya Kilolo
Asia alisema kuwa kuwa mwekezaji huyo ameanza kufungua rasmi
mlango wa wawekezaji na wadau wa maenbdeleo
Kilolo kuanza kuchangia bati na madawati na
kuwa amepata kufanya ziara ndani ya wilaya
hiyo na nje ya wilaya kwenda kuwaomba wawekezaji
na wadau wa maendeleo waliopo nje ya Kilolo
kusaidia harambee hiyo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na
nyumba za walimu .
Alisema kuwa
msaada huo wa kampuni ya Makota Forest ni mwanzo
wa wadau wengine kujitokeza kusaidia
harambee hiyo na kuwaomba wawekezaji
wengine kujitokeza .
Hezron Nganyagwa ni Diwani
wa kata ya Ihimbowilayani humo nae aliishukuru kampuni hiyo
kwa msaada huo alisema kuwa utasaidia kwa matumizi
ya shule iliyokumbwa na maafa ya kuezuliwa ambayo
wananchi wameanza ujenzi wa kuta .
0 maoni:
Chapisha Maoni