Posted by Esta Malibiche on APRIL 20,2017 IN NEWS
Katibu
mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa
ameambatana na Ofisa Mtendaji mkuu Dawasco,mhandisi, Cyprian Luhemeja
katika ziara ya kutembelea Mtambo Ruvu juu uliopo mkoani Pwani.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ametembelea Tenki la Maji la
terminal lilipo karibu na chuo kikuu cha ardhi ambalo linapokea maji
kutoka mtambo wa Ruvu na chini.
Pia
ametembelea tenki kubwa jipya la Maji lilipo Kibamba Luguruni ambalo
linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu na ametembelea Ofisi za Dawasco
Mkoa wa Kibaha na kumalizia ziara yake kwa kutembelea mtambo wa
kuzalishia Maji wa Ruvu juu ambapo umeanza kuzalisha maji mapya leo.
Mkurugenzi
wa Huduma za Ufundi wa DAWASA, mhandisi Romanus Mwangingo, akitoa
maelezo mafupi kwa Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa
Kitila Mkumbo kuhusu tenki jipya la Maji lilipo Kibamba Luguruni ambalo
linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu mara baada ya kufanya ziara ya
kutembelea Mtambo huo wa uzalishaji Maji wa Ruvu juu uliopo Mlandizi,
mkoani Pwani. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
Ofisa
Mtendaji mkuu Dawasco, mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo mafupi
kwa Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo
katika ziara ya kutembelea Mtambo Ruvu juu uliopo mkoani Pwani.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa katika
picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza
na watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji leo jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakimsilikiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo
Moja ya mitambo ya maji katika eneo la Ruvu Juu kama inavyoonekana.
Sehemu ya mtambo wa kusafirishia maji.
0 maoni:
Chapisha Maoni