Posted by Esta Malibiche on APRIL 27,2017 IN NEWS
RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kitaifa, huku
kilio kikubwa cha vyama vya wafanyakazi kikiwa kukosekana kwa mikataba ya hali
bora kazini.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirikisho la
Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Taifa lilipaswa kuwa na waajiriwa
milioni 3.7 katika sekta iliyo rasmi, lakini waliopo ni 650,000 pekee, hali
inayoashiria kutokuwa na mikataba.
Katibu Mkuu wa Tucta, Yahaya Msigwa
alisema hayo jana mjini Moshi ikiwa ni maandalizi ya Mei Mosi itakayofanyika
Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).
“Tayari tumemwandikia Rais Dk Magufuli
kumuomba awe mgeni rasmi, kimsingi sherehe zote kitaifa mgeni rasmi ni
yeye...tunazo ajenda za kumpa Rais, lakini moja ya mambo ambayo ni kero ni hili
la mikataba ya hali bora kazini, wafanyakazi wengi wanafanya kazi kama vibarua
na hawajui haki zao,” alieleza Msigwa.
Alitolea mfano wa watumishi wa mashambani
pekee nchini Kenya ni zaidi ya 700,000 na Afrika Kusini ni zaidi ya milioni
moja na kwamba ipo haja kwa waajiri Tanzania kutafakari upya suala la maslahi
ya wafanyakazi wao na rais anapaswa kulisemea hilo.
Aidha, Katibu Mkuu huyo wa Tucta alitaka
waajiri kuruhusu kuundwa kwa mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi ili kutoa
fursa kwa wafanyakazi kukutana na kujadili maslahi yao lakini pia kufanya kazi
kwa tija zaidi.
Katika hatua nyingine, Msigwa alisema
Tucta inaunga mkono kampeni ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kupambana na
wafanyakazi hewa sanjari na mpango wa kupunguza matumizi ya serikali.
“Pamoja na nia njema ya serikali katika
kupambana na wafanyakazi hewa, lakini tunaomba haki itendeke na isitokee
mfanyakazi ameonewa kwa namna yoyote ile kwani huko ni kuwakatisha tamaa
wafanyakazi waadilifu na waaminifu,” alieleza.
Maadhimisho ya Mei Mosi yatahusisha pia
kujengwa kwa mabanda ya kuoneshwa kwa shughuli mbalimbali za kisekta nchini