Posted by Esta Malibiche on MEI 26,2018 IN KITAIFA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake
TANZANIA(TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika
katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndungulile wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama
cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo
Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti
wa TAWLA Bi. Athanasia Soka wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa
Chama cha Wanasheria Wanawake TANZANIA(TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo
Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akihutubia
kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano mkuu wa 28 wa TAWLA .
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Chama
cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kufanya hima maana Serikali
iko katika hatua za mwisho za kuanza kufanya mageuzi makubwa katika eneo
la mazingira ya biashara kama ilivyobainishwa hivi karibuni na Waziri
wa Viwanda na Biashara.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo
wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria
Wanawake Tanzania (TAWLA) unaotanguliwa na mafunzo endelevu ya Sheria.
“Nawapongeza TAWLA kwa namna ya
kipekee sana kwa kutimiza miaka 28 ya uhai wake. Ni miaka 28 ya
mafanikio makubwa sana. Nawapongeza kwa sababu, katika miaka 28 ya uhai
wenu, hamjawahi kuyumba wala kutoka nje ya lengo la kuanzishwa kwenu,
ambalo ni kutumia taaluma ya sheria kuwasaidia wanawake wasio na uwezo
kupata msaada wa kisheria na haki zao.” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesema anatambua
na kuguswa na kazi nzuri inayofanywa na Chama cha Wanasheria Wanawake
(TAWLA) hapa nchini ya kupigania haki za wanawake kwa kutumia taaluma ya
sheria.
Mkutano huo wa mwaka huu ambao
umebeba kauli mbiu ya “Uwekezaji Wenye Tija; Kufungua Fursa kwa Mitaji
ya Sekta Binafsi na Umma Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi”
Makamu wa Rais amewataka Chama Cha
Wanasheria Wanawake wawasaidie wanawake wajasiriamali kujua sheria,
“Sisi kama wanawake kwanza ni kumnyanyua mwanamke, Ukimnyanyua Mwanamke
umeinyanyua Tanzania”
Makamu wa Rais aliwahakikishia
TAWLA kuwa Serikali haina upungufu wa dhamira. “ Serikali yenu inajali
na inao utashi wa kumkomboa mwanamke kiuchumi”
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa
Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano maana maslahi ya TAWLA na ya
Serikali yanakutana katikati katika suala hili.
Akimkaribisha Makamu wa Rais,
Naibu Waziri wa Afya, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine
Ndungulile amewataka TAWLA kutumia maendeleo ya kiteknolojia kujitangaza
ili wanawake wengi zaidi wapate taarifa zao na kuweza kupata msaada wa
kisheria.
Nae, Mwenyekiti wa Chama cha
Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka amesema TAWLA
inapenda kuona mtoto wa kike na mwanamke anaendelea kupewa kipaumbele
katika maendeleo ya Tanzania.
0 maoni:
Chapisha Maoni