Jumatano, 16 Mei 2018

DC MOFUGA ATOA AGIZO KWA MKURUGENZI WA MBULU

Posted by Esta Malibiche On MEI 16,2018 IN NEWS

 Mkuu wa wilaya ya mbulu chelestino s mofuga leo 16/5/2018 amesikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Tumati kuhusu mwenyekiti wao wa Chadema ndugu Ezekiel martin ambaye wamemkataa kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo, kuwaweka rumande wananchi mwanaume na mwanamke chumba kimoja, kukataa kuwasikiliza kero wananchi, kuwatoza faini  bila risiti . 

Mkuu wa wilaya amesikiliza malalamiko ya wananchi ambao wamekataa kuongozwa na m/kiti huyo. Mkuu wa wilaya amevunja serikali ya kijiji cha Tumati baada ya kukosa sifa kwa tuhuma ambazo zimedumu tangu 2015 hadi leo. 

Wakati  huo uuo alimwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Hudson Kamoga kuitisha  uchaguzj wa kijiji
 Pia mkuu huyo alikemea vikali viongozi ambao hawatumikii wananchi kikamilifu, kwamba waige mfano wa mh Rais wetu Dkt john pombe magufuli ambaye anawajali sana watanzania.




0 maoni:

Chapisha Maoni