Alhamisi, 24 Mei 2018

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI 9 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILL.1 KATIKA HALMASHAURI YA IRINGA


Posted by Esta Malibiche on MEI 24,2018 IN NEWS
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaiafa Charles Francis Kabeho akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa shule ya Sekondari Tanangozi.PICHA NA ESTA MALIBICHE.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaiafa Charles Francis Kabeho akizindua Zahanati ya Muwimbi iliyopo kata ya Ulete  Halmadauri ya Iringa Vijijini.





Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa   Charlse Francis Kabeho    akikabidhi Chandarua chenye dawa kwa mama mja mzito wa kijiji cha Muwimbi,ikiwa ni mpango wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa wananchi wake. Kushoto kwqke ni Mkuu wa Wilaya ya Iringq Richard Kasesela na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilayanya Iringa Vijijini.PICHA NA ESTA MALIBICHE.



Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa   Charlse Francis Kabeho akikata utepe katika Zahanati ya Muwimbi.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wananchi wa Muwimbi.





NA ESTA MALIBICHE
IRINGA

MWENGE wa Uhuru umeipitia miradi 9 yenye thamani ya Bill.1,063. katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambapo miradi 6  imezinduliwa,miaradi 2 imekaguliwa na mrradi 1 umekewa jiwe la Msingi.
Miradi iliyotembelewa na Mwenge wa uhuru nipamoja na Zahanati iliyopo katika kijiji cha Muwimbi,Mradi wa maji uliopo katika kijiji cha Igingilanyi pamoja na Shamba darasa la Korosho lililopo katika shule ya Sekondari Isimani.Pia Mwenge wa uhuru umezindua klub ya mapambano dhidi ya Rushwa na Dawa za kulevya katika shule ya sekondari Kiwere,umeweka jiwe la Masingi katika shule ya Sekondari  Tanangozi na umakagua ukarabati wa barabara ya Ifunda_Kiponzero yenye urefu wa km 14.
Akizungumza  na wananchi wa Kijiji cha Muwimbi kilichopo Halmashauri ya Iringa mara baada ya  kuzindua zahanati na kugawa vyandarua kwa akina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano,Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Charlse Francis Kabeho aliwataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya vyandarua vinavyotolewa na serikali ili kujikinga na ugonjwa wa homa ya maralia.
Kibeho alisema kuwa  serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John  Magufuli itaendelea kujenga miradi zaidi ili wananchi waweze kupata huduma za kijamii ziweze kiurahisi.
"Lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuona wananchi wanaendelea kupatiwa huduma mbali mbali ikiwemo Afya,Elimu na nyinginezo. Pia ninawaomba kila mmoja wenu awe  mlinzi wa miradi hii,tusiruhusu watu wasiopenda maendeleo kuharibu miradi yetu" "Alisema Kibeho

Alisema pamoja na ushiriki wa wananchi katika uchangiaji wa nguvu zao katika miradi hiyo bado wanawajibu wa kulinda miradi hiyo na kuwafichua wahujumu wa miradi iliyojengwa.

0 maoni:

Chapisha Maoni