Posted by Esta Malibiche on MEI 21,2018 IN NEWS
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi
,Vijana na Ajira, ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia chama
cha Mapinduzi CCM, Anthony Mavunde amezitaka Halmashauri Nchini kuhakikisha
zinatekeleza agizo la Waziri Mkuu kwa
Tawala za mikoa juu ya utengwaji wa maeneo mahususi kwa ajili ya shughuli za
kiuchumi za Vijana ili Vijana wengi zaidi wapate fursa za maeneo ya kufanyia
shughuli mbalimbali.
Hayo ameyasema jana mara baada ya kutembelea
Mashamba ya Mboga mboga yaliyopo katika Kijiji cha Kiwele, Halmashauri ya Iringa
Vijijini yanayomilikiwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa GBRI Co. Ltd
Bi. Hadija Jabiri,ambae ni kijana mdogo mwenye umri
wa miaka 27,ikiwa ni moja ya ziara yake ndogo aliyoifanya jana Mkoani Iringa.
Mavunde alimpongeza mjasliamali huyo kutokana
na mafanikio makubwa aliyopata kupitia kilimo cha mbogamboga na kuajiri
takriban ya wafanyakazi 236 ambao bni vijana sambamba na uanzishwaji wa mpango wa
ushikirishwaji wakulima wadogo wadogo(out-growers) ambao wataiuzuia Kampuni
hiyo mazao mbalimbali ya mboga mboga ili aweze kufikia mahitaji ya soko la nje
ambalo linahitaji tani 26 za maharage machanga na njegere change kwa wiki.
.
0 maoni:
Chapisha Maoni