Posted by Esta Malibiche on MAY 2,2018 IN KITAIFA
NA
ESTA MALIBICHE
KILOLO
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli amemuagiza waziri wa
ujenzi, uchukuzi na mawasilino mhandisi Makame
Mbarawa kwa kushirikiana na wakala wa barabara nchini (Tanroad) pamoja na
wakala barabara mijini na vijijini (TARURA) kuanza ujenzi wa barabara ya Iringa-Kilolo kwa kiwango
cha lami yenye urefu wa Km.35.
Rais Magufuli amesema hayo jana wakati akiwahutubia
wananachi wa wilaya hiyo Mkoani hapa mara
baada ya kuweka jiwe la msingi katika hospitali ya wilaya ya Kilolo iliyopo
mkoani Iringa inayoendelea kujengwa.
“Nafahamu kwamba mnahitaji barabara ya lami na bahati
nzuri barabara hii nimenza kujenga kidogokidogo tangu enzi za Venance Mwamoto,serikali
hii imetekengeza barabara nyingi sana katika nchi hii na bahati nzuri nimekuwa
waziri wa ujenzi miaka 17 lakini kwa heshima ya pekee tutazijenga taratibu.”alisema
Dk.Magufulina kuongeza:
“Mna haki ya kuniomba barabara ya lami,Ninachoomba
barabara hii ikikamilika muitunze msipakie mizigo mikubwa ili iweze kudumu kwa
muda mrefu,inawezekana haikuwapo kwenye bajeti ya mwaka huu lakini jungu kuu
haliskosi ukoko.”alisema Dk.magufuli.
Pia Rais Dk. Magufuli ameziagiza halmashauri zote
nchini kuanzisha mifuko ya dawa na kuhakikisha fedha zinazoingia kwenye mifuko hiyo
zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwamo kununua madawa,vifaa tiba na
vitendea kazi vingine.
Alisema kuwa
katika bajeti ya mwaka huu serikali imetenga takribani Bilioni 50 ambazo
zitatumika kwa ajili ya kununulia vifaa tiba hospitalini.
Alisema kuwa hospitali hiyo itakuwa na vitendea kazi
vyote mara baada ya kukamilika huku akiagiza wakala wa majengo Tanzania (TBA) kufanya kazi
usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo haraka iwezekanavyo kwa lengo la
kutoa huduma kwa wananchi wa kilolo ili kupunguza vifo vitokanavyo na kina mama
na watoto.
Rais Magufuli aliwahakikishia wananchi hao kuwaletea
watumishi wa idara ya afya pindi hospitali hiyo ikikamilika atawaletea
watumishi wa afya ili waweze kutoa huduma nzuri.
Naye waziri nchi ofisi ya rais tawala mikoa na serikali
za mitaa Seleman Jaffo amesema kuwa katika bajeti ya mwaka huu serikali
imetenga Bilioni 105 kwa ajili ya kujenga hospitali mpya 67.
Waziri Jaffo alisema kuwa tangu uhuru kulikuwa na vituo
vya afya 515, vilivyokuwa na hadhi vilikuwa 115 peke yake lakini kwa sasa serikali
inajenga vituo 208 kwa mara moja vinafanyiwa ujenzi mkubwa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Kilolo Aloyce kwezi alisema kuwa ujenzi huo utagharimu Sh.Bilioni 4.2
ambayo itajenga majengo saba lakini majengo matano yapo hatua za mwisho lakini
majengo ya kuhifadhia maiti na upasuaji yapo hatua za mwanzo.
“Tuliwasilisha andiko kwa katibu mkuu wizara ya fedha lenye
thamani ya Bilioni 4.2 lakini hadi sasa serikali imetoa Bilioni 2.28 ambayo
ndiyo tuliojenga nayo majengo haya.”alisema Kwezi.
Kwezi aliomba serikali kuwajengea wodi za watoto na kina mama na waototo ambazo zitagharimu
kiasi cha Bilioni 4.6.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa mkoa
wa Iringa ulipokea sh.Bilioni 26 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo
ikiwamo Elimu,maji,afya,kilimo na barabara.
Awali
waziri wa ardhi,nyumba na makazi Wiliam Lukuvi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la
Isimani mkoani Iringa alionekana kutoridhishwa na baadhi ya wananchi wa wilaya
hiyo kuuza ardhi kinyemela
0 maoni:
Chapisha Maoni