Jumanne, 22 Mei 2018

RC IRINGA AMINA MASENZA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUULAKI MWENGE WA UHURU UNAOTARAJIA KUWASILI KESHO MKOANI IRINGA.

Poated by Esta Malibiche ON MEI 22,2018 IN NEWS

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza jana vyombo vya Habari ofisini kwake kuhusu   ujio wa Mwenge wa Uhuru,unaotarajia kuwasili kesho Mei 23 Mkoani Iringa.

NA ESTA MALIBICHE
IRINGA
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka wananachi Mkkan hapa kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa uhuru unaotarajia kuwasili Mkoani Iringa Mei 23,2018 ukitokea Mkoani Mbeya.
Wananachi wote bila kujali itikadi zao,wametakiwa kujitokeza katika viwanja vya makabidhiano ya mwenge wa uhuru,Kwenye miradi ya maendeleo ambayo Mwenge wa Uhuru utatembelea pamoja na maeneo ambayo ujumbe wa mwenge wa uhuru utatolewa.
Akizungumza na vyombo vya Habari jana ofisini kwake alisema kuwa mwenge wa uhuru utakaugua miradi ya maendeleo 40 yenye thamani ya Bill 24.
Katika Gharama hizo wananchi wamechangia kiasi cha  Tsh 1,251,610,850.00,Seriksali kuu imechangia kiasi cha Tsh.8,638,969,449.40,Halmashauri zimechangia kiasi cha Tsh.253,564,461.00 na wadau wa Maendeleo wameweza kuchangia kiasi cha Tsh.14,283,215,936.00.
 Masenza alisema kuwa Mwenge wa uhuru utapita katika Halmashauri zote 5 zilizopo Mkoani hapa huku ukiimza shughuli za mradi ya Maendeleo,ambapo Mei 23 utakuwa Wilaya ya Mufindi,Mei 24 Iringa vijjini,Mei 25 utakuwa Wilaya ya Kilolo,Mei 26,Mwenge wa Uhuru utakuwa Wilaya ya Iringa Mjini na Mei 27 utakuwa katika halmashauri ya Mji wa Mafinga na baada ya kuhitimisha mbIo zake mkoani Iringa utkabidhiwa katIka Mkoa wa Njombe.
‘Ndugu wandishi wa Habri Miradi itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru  ni kutoka  sekta ya  Elimu ya Elimu miradi [10],Afya mieadi [7],Maji miradi[4],Maliasili mradi[ 1],Kilimo miradi [5],Viwanda miradi [2],Uvuvi mradi [1] na mapambano dhidi ya  Rushwa miradi [4]’’Alisema Masenza na kuongeza kuwa
Alisema kuwa Mwenge wa uhuru utatoa ujumbea maalum wa mwaka 2018 na ujumbe wa kudumu katika maeneo yote ambako utakimbizwa,ambapo ujumbe maalumu wa mwenge wa uhuru 1018 unasema ‘Elimu ni ufunguo wa Maisha;Wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.
‘’Ujumbe huu unalenga kutilia makazo umuhimu wa uwekezaji katika elimu unaofanywa na Searikali pamoja na wananchi kiwa ni mkakati madhubuti kupiga vita dhidi ya umasikini na kujenga taifa lenye maendeleo ya vwanda’’Alisema Masenza n akuongeza kuwa
Pamoja na kutoa ujumbe mahususi,mwenge wa uhuru utaendelea kuhimiza mapambano dhdi ya Ukimwi chni ya kaul mbiu isemayo’Mwananchi jitambue;pima Afya sasa’’

0 maoni:

Chapisha Maoni