Posted by EstaMalibiche on Mei 14,2018 in MICHEZO
NA
ESTA MALIBICHE
IRINGA
MSHIRIKI wa
mashindano ya Kimataifa ya bio za magari Kutoka Mkoa wa Iringa,Ahmed Huwel
ameibuka kidedea kunyakua kombe la mbio hizo huku akiwaacha wenzake 18 kutoka
Nchi mbalimbali.
Mashindano
hayo yalianza Mei 12,2018 Mkoani Iringa,ambayo yalihitimishwa jana Mei 13,ambapo nchi nne
zilishiriki ikiwemo,Tanzania,Kenya,Uganda na Zambia,huku Mshiriki kutoka
Tanzania Mkoani Iringa,Ahmed Huwel
akipeperusha Bendera ya Taifa kwa kuibuka mshindi.
Akizungumza
wakati wa kufunga mashindano hayo jana,Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Amina Masenza
alizitaka Nchi zilizoshiriki kuendelea
kutoa ushirikiano katika Nyanja mbalimbali ili kukuza uchumi wan chi.
‘Mashindano haya yasaidie
kujenga urafiki na undugu miongoni mwenu washiriki wa michezo ya ndani na nje
ya Tanzania,yasaidie kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika Mkoa wetu wa
Iringa,yasaidie kuutangaza utamaduni wa Mkoa wa Iringa ndani na nje ya Tanzani,yasaidie
kuimarisha umoja na mshikamano na nchi jirani pia yasaidie kukuza na kuendeleza
biashara mbalimbali katika Mkoa wa Iringa n Tanzania kwa ujumla’Alisema Masenza.
Masenza alisema kuwa Uendelezaji
wa michezo unahitaji uwekezaji mkubwa hivyo ni jukumu la wadau wote wa
maendeleo kuendelea kushikamana ili kuweza kufanikisha kuendeleza michezo
katika Mkoa wa Iringa na Tanzania kwa
ujumla.
‘Kutokana na umuhimu wa
michezo hii na michezo mingine inayochezwa hapa Mkoani Iringa napenda kuchukua
nafasi hii kuwaomba tena wadau mbalimbali wa michezo kuendelea kuchangia
shughuli za michezo hapa nchini hususani katika mkoa wangu wa Iringa ambao una
vipaji vingi vya michezo’Alisema Masenza.
Akishukuru kwa niaba ya
washiriki wa mbio hizo,Ahmed Huwel aliwashukuru washiriki wote kutoka Tanzania
na nje ya Nchi kwa kuonyesha ushirikiano toka mashindano haya yalipoanza.
‘Sisi sote ni washindi
kwasababau tultoka katika Nchi Zetu tukiwa na lengo moja kwa kila mmoja kuibuka
mshindi,lakini tunatakiwa tukubaliane na matokeo yaliyotokea.Huu umoja tulipouonyesha
tunatakiwa tuuendeleza katika mashindano yatakayoendelea’Alisema Huwel;
Ninayofuraha kubwa
kushinda nyumbani na kuipeperusha bendera ya Taifa.Huu ni ushindi wa watanzania
wote na wanairinga kwa ujumla,ninawashukuru sana watanzania kwa kunitia moyo
katika safari yangu hii,pale nilipokuwa nimekata tama mlinipa moyo na hatimae
leo nimeibuka mshindi’Alisema Huwel.
0 maoni:
Chapisha Maoni