Ijumaa, 11 Mei 2018

WAZIRI WA TAMISEMI SELEMANI JAFO AISHUKURU KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA NA TAMISEMI KWA USIMAMIZI WAKE

Poated by Esta Malibiche on MEI 11,2018 IN NEWS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiongea na wananchi wa Maruku katika Halmashauri ya  wilayani ya Bukoba
Wananchi wa kijiji cha Maruku wakiwa katika mkutano wa uwekaji wa jiwe la msingi kwenye wodi ya wazazi.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na TAMISEMI na  Mbunge wa Jimbo la Bukoba vijijini  Jasson Rweikiza akimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kwa uwekaji wa jiwe la msingi katika wodi ya wazazi Maruku.
Mjumbe wa kamati ya Utawala na TAMISEMI Mhe. Khatib Said Haji akiwahimiza wananchi wa Maruku katika kuhusu kushiriki kwenye maendeleo.


Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Angelina Malembeka akiongea na wananchi wa kijiji cha Maruku Bukoba vijijini.


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na wajumbe wa Kamati ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
................................................................
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo ameimwagia sifa Kamati ya Bunge ya Utawala na TAMISEMI kwa ushauri na usimamizi wake.
Waziri Jafo aliyasema hayo alipokuwa amealikwa na wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba vijijini kuweka jiwe la Msingi katika wodi ya wazazi ya zahanati ya Maruku ambayo inatarajiwa kuwa Kituo cha afya.

Amesema anashukuru kamati hiyo kwa maelekezo, ushauri na usimamizi wake kwa wizara hiyo.

Katika zoezi hilo la uwekaji wa jiwe la msingi, Waziri Jafo ameambatana na Kamati ya Bunge ya TAMISEMI ambayo ipo mkoani Kagera kwa ajili ya kukagua miradi iliyo chini ya Ofisi ya TAMISEMI. 


Naye, Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Bukoba vijijini Mhe. Jasson Rweikiza alimshukuru Waziri Jafo  kwa uchapakazi na usikivu wake katika utekelezaji wa ushauri na  maelekezo ya kamati ya Bunge.


Aidha, wajumbe wa kamati wamewataka wananchi wa Bukoba vijijini kushikamana kwa pamoja na mbunge wao katika ajenda ya kujiletea maendeleo.

0 maoni:

Chapisha Maoni