Jumapili, 13 Mei 2018

MWENGE WA UHURU KUKIMBIZWA MKOANI IRINGA

Posted by Esta Malibiche on MEI 13,2018 IN NEWS



Mwenge wa Uhuru unatarajia kuwasili Mkoani Iringa Mei 23,2018 hadi 27 ukitokea Mkoani Mbeya,ambao utapokelewa katika kijiji cha  Sadan,Wilayani Mufindi kupitia Madibila.

Akitoa taarifa ya awali kuhusu kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru Mkoani Iringa,Mratibu wa mbio za Mwenge Mkoa wa Iringa,ambae pia ni Ofisa wa Vijana Mkoa,Atilio Mganwa alisema kuwa  Mwenge wa Uhuru utakimhizwa katika Halmashauri zote tano za Mkoa wa Iringa.

Mganwa aliwataka vijana Mkoani hapa  kushiriki  kikamilifu  katika maadhimisho hayo kwa madai ya kuwa na ujumumbe mahususi kwao.

"Ukiacha kazi ya kufungua  miradi mbalimbali,Mwenge wa Uhuru una ujumbe kwa vijana na wanafunzi  unaosema" Elimu ni ufunguo  wa maisha ;Wekeza sasa kwa maendeleo ya taifa letu"Alisema Mganwa.
Aidha alisema kuwa mara baada ya kuhitimisha mbio zake Mkoani Iringa,Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa Mkoani Njombe Mei 28 asubuhi katika kijiji cha Idofi,Mpakani mwa Mkoa wa Njombe na Iringa. 

0 maoni:

Chapisha Maoni