Posted by Esta Malibiche on MEI 23,2018 IN NEWS
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos
Makala,makabidhiano hayo yamefanyika leo hii katika kijiji cha Sadani
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.PICHA NA ESTA MALIBICHE
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akivalishwa skafu na mmoja wa watoto chipukizi ,ishara ya kukaribishwa Mkoani Iringa wakati wakitokea Mkoani Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala,makabidhiano hayo yamefanyika leo hii katika kijiji cha Sadani Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akimkaribisha Kiongozi wa
Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2018
Charle Francis Kabeho.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akimkaribisha mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Charle Francis Kabeho.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu akisalimianana Mkimbiza Mwenge kitaifa. |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2018 Charle Francis Kabeho. |
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asiah Abdalah akisalimianana Mkimbiza Mwenge kitaifa. |
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri David Willium akisalimiana na mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa. |
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa
Charle Francis Kabeho.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akisalimiana na Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa akipokea Mwenge wa Uhuru.
Mkuu wa wilaya ya KiloloAsiah Abdala akipokea Mwenge wa Uhuru
Kamanda wa Jeshoi la Zima moto Mkoa wa Iringa akipokea Mwenge wa Uhuru
NA ESTA
MALIBICHE
IRINGA
MWENGE wa Uhuru
2018 umewasili leo Mkoani Iringa na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina
Masenza katika kijiji cha Sadani kilicgopo
Haslmashauri ya Wilaya ya Mufindi , ukitokea Mkoani Mbeya,ambapo unatarajia
kuzindua,kukagua na kutembelea miradi 39 ya Maendeleo yenye thamani ya Bill 24.1
Miradi
itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru nipamoja na Elimu, Afya,Maji,Maliasili,Kilimo,Viwanda,Uvuvi
na mradi wa Rushwa.
‘Mwenge wa Uhuru
mwaka huu 2018 umebeba kauli mbiu isemayo “Elimu ni ufunguo wa Maisha; Wekeza Sasa kwa
Maendeleo ya Taifa letu.” Kauli mbiu hii
inawahamasisha wananchi hususani wa Mkoa wa Iringa kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto
shule ili mkoa wetu na Taifa kwa ujumla upate wataalam wa kutosha ili taifa letu liweze kupiga hatua kubwa ya
maendeleo kwa kuwatumia wataalamu wetu wa ndani’Alisema Masenza na kuongeza
kuwa
Pamoja na Kauli Mbiu tajwa hapo juu Mwenge wa Uhuru
katika Mkoa wetu utaendelea kuwahamasisha wananchi kuhusu Mapambano dhidi ya
Rushwa, VVU/UKIMWI, Matumizi ya Dawa za Kulevya na Mapambano dhidi
ya Malaria.
Akizungumzia hali ya maambukizi ya ukimwi alisema
kuwa,Mkoa wa Iringa ni wa pili kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya
virusi vya ukimwi Nchini kutokana na utafiti wa mwaka 2016\2017 unaonyesha kuwa
kiwango cha maambukizi kimeongezeka na kufikia asilimia 11.3 ikilinganishwa na
kiwango cha TAIFA ASILIMI 4.7Kutokana na hali hiyo Mkoa kwa kushirikiana na
wadau tunaendelea kutekeleza mkakati wa kupambana na Ukimwi.
0 maoni:
Chapisha Maoni