Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Alhamisi, 29 Machi 2018

RAIS WA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA AWATAKA WAAMINI KUUISHI UKRISTO WAO KWA KUTENDA MATENDO MEMA.

Posted by EstaMalibiche on March 29,2018 IN NEWS

 Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akiadhimisha Sadaka ya Misa takatifu ya Alhamis Kuu katika Parokia ya Mkwawa Jimboni Iringa.
Katika Homilia yake amewataka waamini kuwa wanyenyekevu kama Yesu Kristo alivyokuwa mtii hata akafa msalabani.

Baba Askofu amesema kuwa mama Kanisa anafundisha kwamba, Kristo Yesu aliwapenda watu wake upeo na alipokuwa anakaribia “Saa yake” ili kutoka hapa ulimwenguni na kurudi kwa Baba yake wa mbinguni.

Wapendwa wana familia ya Mungu Siku ile ya Alhamisi kuu, walipokuwa wakila, Yesu aliwaosha mitume wake miguu yao na kuwapatia Amri ya upendo inayomwilishwa katika huduma ya upendo, hasa kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.Akataka pia kuwapatia amana ya upendo huu na kuendelea kubaki kati yao na kuendelea kuwashirikisha Fumbo la Pasaka, aliweka Sakramenti ya Ekarissti Takatifu, kielelezo cha sadaka, shukrani, kumbu kumbu endelevu na uwepo wake kati yao katika alama ya Mkate na Divai.PICHA NA ESTA MALIBICHE

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akiadhimisha Sadaka ya Misa takatifu ya Alhamis Kuu katika Parokia ya Mkwawa Jimboni Iringa.

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akiadhimisha Sadaka ya Misa takatifu ya Alhamis Kuu katika Parokia ya Mkwawa Jimboni Iringa.
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akiwaosha miguu waamini.


Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akiwaosha miguu waamini.
Waamini wa parokia ya Mkwawa jimbo katoliki la Iringa wakiwa katika misa takatifu ya Aalhamis kuu iliyoongizwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.
Waamini wa parokia ya Mkwawa jimbo katoliki la Iringa wakiwa katika misa takatifu ya Aalhamis kuu iliyoongizwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.
Waamini wa parokia ya Mkwawa jimbo katoliki la Iringa wakiwa katika misa takatifu ya Aalhamis kuu iliyoongizwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.
Wanakwaya na wamini wa parokia ya Mkwawa jimbo katoliki la Iringa wakiwa katika misa takatifu ya Aalhamis kuu iliyoongizwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.
Wanakwaya na waamini wa parokia ya Mkwawa jimbo katoliki la Iringa wakiwa katika misa takatifu ya Aalhamis kuu iliyoongizwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.

RC MAKONDA ATOA ZAWADI KWA WAJAWAZITO WATAKAOJIFUNGUA PASAKA

Posted by Esta Malibiche on March 29,2018 IN NEWS
IMG-20180329-WA0113
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametoa zawadi ya vifaa tiba vya Mama mzazi kwaajili ya kujifungulia (Delivery Packs) 200 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi million 20 Kama zawadi yake ya sikukuu ya pasaka kwa kinamama watakaojifungua kwenye msimu huu wa pasaka.
Gharama ya mfuko mmoja (package) ya Vifaa hivyo vya kisasa ni Shilingi laki Moja ambapo ndani yake kuna Mashuka, Vitambaa, Dawa, Mabomba ya Sindano, Pamba, Kibanio cha kitovu, Nyuzi, pedi za kinamama, Dawa ya kuzuia upotevu wa damu, Nyembe na Gloves ambapo vitatolewa Bure kwa Mama mzazi atakaejifungua msimu huu wa pasaka kwenye vituo vya Afya na zahanati zilizopo kwenye Wilaya Tano za Mkoa huo.
IMG-20180329-WA0112
RC Makonda ametoa vifaa hivyo baada ya kubaini changamoto ya baadhi ya kinamama kushindwa kumudu gharama ya vifaa vya kujifungulia na kujikuta wanatumia kanga au nguo jambo ambalo ni hatari kiafya kwa mama na mtoto. 
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya RC Makonda kwa waganga wakuu wa halmashauri na wasimamizi wa vituo na Zahanati, Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Dr. Grace Maghembe amesema vifaa hivyo vitasaidia pia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
 IMG-20180329-WA0108
Vifaa hivi vinapatikana Bure kwenye Hospitali zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwa Msimu huu wa Pasaka hivyo kwa wewe Mama unaetaka kujifungua fika Hospitalini vifaa vyako utavikuta.
KUTOA NI MOYO, SIO UTAJIRI.

JOSEPH MWAGALA ATATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA SEKONDARI REGINA PACIS MUFINDI, AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI 100 KWA AJILI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA

Posted by Esta Malibiche on March 29,2018 IN NEWS


Na Esta Malibiche

Mufindi

SHULE ya  sekondari ya wasichana ya Regina Pacis inamilikiwa na kanisa katoliki parokia ya Kibaoni jimbo katoliki la Iringa tayari imeanza ujenzi wa vyumba nane vya madarasa ambapo mdau wa maendeleo mkoani Iringa,Josepht Mwagala amekabidhi mifuko 100 ya saruji  yenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni 1.3 kwa ajili ya kukamilisha  ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Awali shule hiyo  iliyopo katika kata ya Kibaoni wilayani humo,  ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya miundombinu ya madarasa lakini kwa sasa yameanza kwa muundo wa ghorofa ambavyo vitawezesha watoto wa kike wa kidato cha tano kuanza masomo shuleni hapo mwaka huu 2018.

Akizungumza jana wakati wa kukabidhi msaada huo Mwagala alisema kuwa ametekeleza ahadi yake aliyotoa wakati wa mahafi ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana na kujionea mradi mkubwa wa maendeleo wa ujenzi wa shule hiyo pamoja na changamoto zake na ndio maana ameamua kufanya hivyo.

“Nimeamua kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt.John Magufuli kwa kuboresha miundombinu na hii ni sehemu tu ya msaada wangu,nimevutiwa na miradi ya elimu inayotekelezwa katika kijiji hiki , niseme tu hiyo ni sehemu ya msaada lakini pale nitakapoona ninakitu cha kufanya hapa nitaendelea kuwasaidia kadri ya uwezo wangu.”alisema Mwagala

Pamoja na masaada huo pia ameahidi kuwa atahakikisha anajichanga kadri ya uwezo wake kuhakikisha anasaidia kutatua kero ya maji inayoikabili parokia na shule hiyo kwa sababu kwa kuwa msaada huo pia utawasaidia wananchi wa kijiji hicho na vijiji vya jirani.

Akipokea mifuko ya saruji hiyo  mkuu wa shule  hiyo ambae ni paroko wa parokia ya Kibaoni padre  Cesco Muyinga alimshukuru  Mwagala kwa kutoa msaada huo na kutoa wito kwa wadau wengine hususani wenye uwezo kujenga utamaduni wa kusaidia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo wanayotoka kama sehemu ya kurejesha fadhili kwa jamii waliowaacha katika maeneo hayo.

Padre Muyinga alisema msaada huo umefika wakati mwafaka kwa kuwa majengo ya shule hiyo yanatarajia kuanza kutumika wakati wowote kuanzia sasa.

" Kimsingi umetusaidia sana,kwani tangu uje kwenye mahafali yetu na kuona changamoto aliahidi kusaidia utatuzi wa tatizo la maji jambo ambalo unaendeleo nalo na sasa mifuko ya Saruji"alisema Padre Muyinga


Padre Muyinga aliongeza kuwa atahakikisha mradi huo wa ujenzi wa vyumba vya madarsa sita unaojengwa kwa muundo wa ghorofa unakamilika kwa wakati,ambapo ametenga kila siku ya Jumatano kuwa siku ya kuwaombea wafadhili na watu mbalimbali wanaojitolea kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.

Nao baadhi ya wananchi wa kata hiyo akiwamo Maria Sanga na Jackson Kikoti alisema kuwa kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto ya maji huku mdau huyo akiahidi kutatua changamoto ya maji siku za karibuni.

Kikoti alisema kuwa wananchi hao hususani kina mama wanatembea umbali mrefu kutafuta maji jambo ambalo linaweza kuhatarisha familiya zao.


Jumatano, 28 Machi 2018

MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE MACHI 29,2018

Posted by Esta Malibiche on March 29,2018 IN KITAIFA




































MKUU WA MKOA WA IRINGA AMINA MASENZA AWAPONGEZA RDO KWA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI MUFINDI NA KILOLO

Posted by Esta Malibiche on March 28,2018 IN NEWS


 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi. 
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimtusha ndoo ya maji mmoja ya wananchi walihudhulia uzinduzi wa mradi maji ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania 
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali wakibadilisha mawazo juu ya mradi huo ambao umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)
 Hapa ndio tank kubwa la mradi wa maji unaofadhiliwa nashirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania na 
umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100) 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.

 Na Fredy Mgunda,Iringa.
 
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania kwa kufanikisha kupatikana kwa maji katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Kilolo na Mufindi ambayo itakuwa njia moja wapo ya kuchochea maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Nandala’ Masenza alisema kuwa amefurahishwa na mfumo ambao unatumiwa na shirika hilo kwa kutoa huduma ya maji kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika.

“Mradi wowote ule ukiwa na ushirikiano mkubwa na wananchi mara nyingi wananchi wanautunza mradi huo kwa kuudhamini na kuulinda,hivyo nawapongeza RDO kwa kufanya maamuzi sahihi ya kubuni mradi huo pamoja na wananchi” alisema Masenza

Masenza alisema kuwa mradi huo wa maji utatoa huduma kwa wananchi wengi na taasisi binafsi nyingi hivyo wananchi wanatakiwa kuutunza na kuudhamini ili udumu kwa muda mrefu na kuondoa tatizo la maji ambalo limekuwa kero ya muda mrefu.

Nimesikia kwenye risala yenu kuwa mradi huu utahudumia kata zifuatazo Ifwagi,Mdabulo,Ihanu,Luhunga,Mtitu na Kising’a na vijiji vitakavyopata huduma hiyo ni Igonongo,Ludilo,Kidete,Ikanga,Nandala,Ibwanzi,Isipii,Mkonge,Lulanzi,Luhindo,Barabara mbili na Isele hivyo ukiangala utagundua kuwa mradi huu ni mkubwa na upaswi kupuuzwa kwa maendeleo kwa wananchi wa maeneo ambayo mradi huo umepita.

“Jamani wananchi ambao mmepata bahati ya kupitiwa na mradio huu mkubwa wa maji mnapaswa kuulinda na kuudhamini kwa kuwa ni mmoja ya mradi mkubwa ambao unapunguza adha ya upatikanaji wa maji ambayo hapo awali ilikuwa kero kubwa” alisema Masenza

Kwa upande mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali alisema kuwa mradi huo umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100) ambao ndani yake kuna pesa zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya kusaidia kupata huduma ya maji.

“Sisi kama RDO ambao ndio wafadhili namba moja wa mradio huu wa maji tumechangia kiasi cha shilingi milioni themenini na sita,laki nane ishirini na moja elfu (86,821,000) na wananchi walichanga kiasi cha shilingi milioni nane,laki sita themenini na mbili na mia moja (8,682,100)” alisema Filipatali

Filipatali  alisema kuwa mradi huo wa maji  utazaliza ujazo wa lita 776  kwa vijiji vyote ambazo vinatumia huduma hiyo ya maji na pia wananchi watakao pata huduma hiyo ni 10,874 kwa vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi huo na jumla ya taasisi 18 nazo zitanufaika na huduma hiyo.

“Mkuu wa mkoa sasa ukiangalia kwa ujumla ndio utagundua kuwa ni mradi ambao utakuwa unakomba wananchi wengi waliokuwa wanapata tabu juu ya kupata maji hivyo naomba pia nisisitize wananchi kuutunza na kuchangia kwa malipo kidogo kwa ajili ya ukarabati wa mashine na mitambo mingie inayosukuma maji hayo ili isihalibike” alisema Filipatali

Filipatali alisema kuwa mradi huo unakabiliwa na changamoto zifuatazo baadhi ya watumiaji maji kutochangia, viongozi kutotimiza majukumu yao kama kutohudhuria mikutano ya mapato na matumizi,watumiaji maji kutotilia mkazo elimu wanayopewa na wataalamu wa maji,siasa kuingia mfumo mzima wa mradi huu na baadhi ya serikali za vijiji kuchukulia mapato ya miradi ya maji kama sehemu ya mapato ya serikali  kitu ambacho sio kweli mfano kjiji cha Lidilo

“Hizi changamoto zimekuwa kero sana kwenye miradi ambayo imekuwa inatekelezwa kwenye maeneo husika hivyo niwaombe viongozi wa kiasa wawe wa kwanza kutoa elimu juu ya miradi ambayo inafaida na kutatua changamoto za wananchi kwenye maeneo yao” Filipatali

Jumapili, 25 Machi 2018

PITIA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO MARCH 26,2018

Posted by Esta  Malibiche on March 26,2018 IN KITAIFA