Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumatatu, 31 Julai 2017

MAJALIWA ZUNGUMZA NA WATUMISHI WA MANISPAA YA MBEYA

Posted by Esta Malibiche on JULY 31,2017 IN NEWS

PMO_6985
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafisi wa Manispaa ya Mbeya kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya Julai 31, 2017.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Kulia ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson
PMO_7002
Baadhi ya Watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya julai 31, 2017
PMO_7007
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa TAKUKURU wa Mkokoa wa Mbeya, Mhandisi Emmanuel Kyabo taarifa zinaoonyesha ubadhirifu uliofanywa na baadhi ya watendaji katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa jijini Mbeya ili afanye uchunguzi wa kina  na kumshauri Waziri Mkuu hatua zinazostahili kuchukuliwa kwa wanatakaobainika kuwa wamefanya makokosa. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Aagiza kukamatwa kwa viongozi 12 wa Jiji la Mbeya kwa kusabaisha hasara ya Bilioni 63

Posted by Esta MALIBICHE ON july 31,2017 IN NEWS   

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iwakamate watendaji 12 wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakiwamo aliyekuwa mstahiki meya Athanas Kapuga.

Amesema pia wakamatwe, wakurugenzi watatu, kaimu mkurugenzi, wahasibu wawili na wajumbe wa bodi wanne kwa kuisababishia hasara jiji hilo kiasi cha Sh63 bilioni katika ujenzi wa Soko la Mwanjelwa.

Amewataka makamanda wa Takukuru kuanzia leo wawakamate watuhumiwa hao na kwamba anatuma timu kutoka ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya kuandaa mashtaka hayo ambapo itatua Mbeya  Jumatano.

UZINDUZI WA BARAZA LA WAZALISHAJI WAFANYIKA ZANZIBAR.

Posted by Esta Malibiche on JULY 31,2017 IN NEWS

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akiangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Wafanyabishara wa Zanzibar katika Uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Unguja.
Katibu wa Baraza la Wazalishaji Zanzibar Madam Cheherezade Chukh akitoa hotuba ya makaribisho katika uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Unguja.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazalishaji Zanzibar Ahmed Yussuf Baalawy akizungumza machache katika uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Unguja.
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara  Wenyeviwanda,Kilimo na Utalii (ZNCCIA)Taufiq Tourky akitoa hotuba na kumkaribisha Mgeni Rasmi katika  Uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Unguja .
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika  uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Unguja.
Mgeni Rasmi Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace  Malindi mjini Unguja.

PICHA NA-YUSSUF SIMAI ALI/MAELEZO ZANZIBAR.

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AHIMIZA WAKUU WA YUO VYA MAENDELEO YA JAMII KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI NA TARATIBU KATIKA UTENDAJI KAZI.

Posted by Esta Malibiche on JULY 31,2017 IN NEWS

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na washiriki wa mkutano wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
 Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni Mwenyekiti wa mafunzo (kulia) Bw. Paschal Mahinyika akiwatambulisha washiriki wa mafunzo ya kudhibiti viashiria hatarishi kabla ya kukaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
  Washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinavyosimsmiwa na Wizara wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa uendeshaji wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
 Watendaji kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kutoka kulia ni Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu Bibi Deodata Makani , katikati ni Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi Bibi Martha chuma na kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bibi Lightness Mchome wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) katika  ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.   
 Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu kwa kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Deodata Makani akitoa somo juu ya masuala ya kuzingatia kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni mwenyekiti wa mafunzo Bw. Paschal Mahinyika(kulia) wakati wa mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo vya maendeleo ya Jamii yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwasilisha mada kuhusu uaandaaji mzuri wa Bajeti kwa Wakuu wa Vyuo vua Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo hao yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati waliokaa)akiwa akiwa na wakufunzi wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakati wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi mahala pa kazi yaliyofanyikakatika Ukumbi wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo leo 31.7.2017. Picha na Erasto Ching’oro WAMJW
Na Erasto Ching’oro WAMJW.

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kazi katika kuendesha vyuo wanavyovisimamia.

Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao  kuhusu udhibiti wa viashiria hatarishi vya utendaji na utawala ikiwa ni pamoja na  kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha katika utendaji wao wakazi wa kila siku ili kuepuka hoja za ukaguzi wa fedha.

Amesisitiza kuwa wakuu wa vyuo ni watumishi wa Umma na wanapaswa kuzingatia weledi mahala pa kazi kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zote za utumishi wa Umma katika kutimiza majukumu yao.

“Niwatake Wakuu wa Vyuo mliopo hapa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika kundesha vyuo mnavyoviongoza tuondokane na dosari katika suala la udhibiti wa Fedha katika matumizi” alisema Bibi Sihaba.
Aidha, Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga, amesema kuwa mara baada ya mafunzo haya maalum, Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini vitaweza kufuta hoja zote za ukaguzi mahala pa kazi kutokana na kufanya kazi kwa kufuata maadili, maarifa na miongozo na weledi unaotakiwa katika uendeshaji wa vyuo.

Aidha Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wakuu wa vyuo kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu yao mahala pa kazi, kuimarisha mawasiliano katika uwajibikaji wa pamoja kwa kuimarisha mifumo ya utendaji kazi katika vyuo vya maendeleo ya jamii.
Mafunzo haya yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na kushirikisha vyuo vya Buhare, Uyole, Rungemba, Ruaha, Mabughai, Monduli na Mlale.

WANANCHI MONDULI KUNUFAIKA NA MAJI

Posted by Esta Mlibiche on JULY 31,2017 IN NEWS

IMG_20170730_113056
Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim (kushoto) na Andrew Chung ambaye ni mbunifu wa mtambo wa kusafisha maji wakionyesha mtambo huo kwenye uzinduzi wake kwenye kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha 
IMG_20170730_113923
Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim (kushoto) na mchungaji wa kanisa la Enyora Daniel Vengei wakiwa kwenye uzinduzi wake katika kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha. 
IMG_20170730_133855
Wananchi wa kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha wakishuhudia uzinduzi  wa mtambo wa kusafisha maji na kuyachuja uliofanywa na kampuni ya Korea ya Smart Vision.
………………………….
Zaidi ya kaya 700 za wananchi wa Kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha, waliokuwa wanatumia maji ya kwenye bwana wanatarajia kunufaika na mradi wa kusafisha maji na kuchuja maji kuwa safi uliozinduliwa Kijiji hapo. 

Awali, wananchi hao walikuwa wanatumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kupika, kufua, kuoga na kunywa maji hayo ya bwawa ambayo pia yalikuwa yanatumiwa na mifugo ya eneo hilo. 

Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim akizungumza jana kwenye uzinduzi wa mradi alisema lengo ni jamii ya eneo hilo kunufaika na maji safi na salama yanayochujwa kupitia ubunifu wao. 

Kim alisema kwa kuanza kuwanufaisha wananchi wa eneo hilo, wanatarajia kugawa majiko rafiki ya mazingira 22 na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji ya bwawa kuwa safi na salama 22 kwa kaya 22 zitakazowanufaisha zaidi ya watu 220. 

 Alisema Smart Vision kupitia uwekezaji wa Korea Trade-Investment Promotion Agency. (KOTRA) jamii ya eneo hilo itanufaika na na mradi huo wenye lengo la kuondokana na matumizi ya maji yasiyo safi wala salama ambayo yanasababisha magonjwa ya tumbo. 

“Jamii ya eneo hili kupitia mchungaji wa kanisa la Enyorata Daniel Vengei, walileta maombi kwetu kuwa wanatatizo la maji, hospitali na shule, ndipo tukaona tuanze kutatua hili suala la maji ndipo tukaleta mitambo hii ya kuchuja na kusafisha maji,” alisema Kim. 

She said goal of project, Smart Vision head about maasai water problem in Korea. Smart Vision developed water purifier to help maasai people overcome water problem.

Kim said now Smart Vision a Korean Environmental company launches water project ina Tanzania, hopes to expand project to other parts of Tanzania where there is lack of drinking water.

“This project was aided financially bya KOTRA (Korea Trade-Investiment Promotion Agency) who supports international business of Korean companies, specifically, the KOTRA branc in Dar es salaam gave Smart Vision immense support in order to help people suffering from lack of drinking water though the water purification project,” said Kim.

She said people who helped with project is Director of Smart Vision Seo-Young Kim, Manager of Smart Vision, Hyun-Jung Chung and Purifier developer and volunteer, Andrew Chung.

Mkazi wa Kitongoji cha Emairete Rose Lemomo alisema alisema awali walikuwa wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama lakini kupitia mradi huo wataondokana na maradhi ya tumbo yaliyokuwa yakiwakabili hasa watoto. 

Lemomo aliwashukuru wote waliohusika na kufanikisha mradi huo, kwani hivi sasa watakuwa wanachota maji bwawani na kuyachuja na kuyasafisha kupitia mitambo hiyo. 

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Irmorijo, Mirishi Songoyo alishukuru shirika la Smart Vision kwa kufanikisha mradi huo wa maendeleo ambao utainufaisha jamii ya eneo hilo walioteseka kwa muda mrefu juu ya suala la maji. 

“Tunawaomba wananchi watakaofikiwa na mradi huu kuhakikisha wanawasaidia na wale ambao bado wanasubiri kupatiwa majiko na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji,” alisema Songoyo.  

Mwalimu wa shule ya msingi Irmorijo, Stephen Laizer aliwataka wananchi wote waliofanikiwa kupatiwa mradi huo kuhakikisha wanautunza ili kunufaika nao kwa muda mrefu kwani wameteseka kwa miaka mingi kwenye tatizo la maji. 

“Wageni wanapokuja kwenu inawabidi kuwashukuru hata kama hawajaacha chochote ila hawa wametuletea teknolojia ya maji, wanaweza kutufanyia mengine mazuri,” alisema Laizer. 

BARAZA LA MADIWANI MJI WA KIBAHA LAADHIMIA MKUU WA IDARA YA MAZINGIRA NA MAJI WAWAJIBISHWE

Posted by Esta Mlaibiche on JULY 31,2017 IN NEWS

IMG_20170727_125010
Mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka akieleza maadhimio ya baraza la mji huo yaliyotolewa kwenye baraza la madiwani
IMG-20170731-WA0052 IMG-20170731-WA0053
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Lucy Kimoi akizungumza jambo katika baraza la madiwani la Mji huo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
BARAZA la madiwani la halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Pwani ,limeadhimia mkuu wa idara ya mazingira Tumaini Kaila na wa idara ya maji Grace Lyimo wachukuliwe hatua na mamlaka za ajira zao endapo watabainika kuzembea kusimama majukumu yao  .
Akielezea maadhimio ya madiwani hao ,mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka ,alisema baraza hilo pia limemkataa mkuu huyo wa idara ya mazingira kutokana kukosa ushirikiano na kushindwa kusimamia hali ya usafi ya mji huo ambayo hairidhishi .
Aidha limeitaka mamlaka husika ya ajira yake imchukulie hatua stahiki kwa mujibu wa ajira yake. 
Koka alisema wameshindwa kumvumilia mkuu huyo wa idara ya mazingira kwani huwezi kufanyakazi pasipo kuwa na mahusiano mazuri na madiwani wala watendaji wengine .
“Maeneo mengi na ya wazi hayapo katika usafi hivyo na hili nalo tumeshapiga kelele ,tumeshauri ,hashauriki ,ni bora mamlaka husika imuwajibishe .” alisema Koka .
Hata hivyo ,madiwani hao wameelekeza wakandarasi washauri na wasimamizi wa miradi ya maji wachukuliwe hatua zile zinazostahiki kwa kushindwa kusimamia miradi hiyo na kusababisha hasara ya mil.132 .
Walitaka  wakandarasi hao wachukuliwe hatua kwa kulingana na mikataba yao.
Koka alibainisha kwamba ,waajiriwa wa halmashauri waliosimamia miradi ya maji wakiongozwa na Grace Lyimo ,mamlaka zao zinazowasimamia ziangalie hatua za kuwachukulia endapo watabainika kufanya uzembe .
Katika hatua nyingine ,mbunge huyo aliishauri halmashauri na watendaji kukamilisha miradi mbalimbali ambayo ni viporo ikiwemo zahanati na majengo ya madarasa .
Koka alisema miradi hiyo ambayo haijakamilika ikamilishwe kabla ya kuanza mipya  ya aina ile ile .
Alielezea kuwa ,haina budi fedha zinazoingizwa na serikali ikakamilisha miradi lengwa kwa maslahi ya jamii kuliko kuishia kati huku mwaka wa fedha mwingine inaanzishwa miradi mingine hivyo kusababisha kuwa na mlundika wa miradi ya zamani .
Wakati huo huo ,Koka alisema kwa mujibu wa sheria 0.03 ya mauzo au huduma kwa viwanda au kampuni hulipia kodi ya mapato kutokana na bidhaa wanazozalisha .
Alisema licha ya kulipia mapato kisheria lakini inapaswa halmashauri ikaangalia namna ya kukusanya asilimia kiasi ya mapato kwenye viwanda na makampuni yanayozunguka mji huo kwa ajili ya kujiongezea mapato .
“Kila anaetoa huduma inatakiwa halmashauri imfikie ili inufaike na wadau wake”alisema Koka .
Nae diwani wa kata ya Tumbi ,Hemed Chanyika alisema kwa kushindwa kupeleka taarifa za kata za maji imechangia kukosa zaidi ya sh mil 100 ambazo wahisani walitakiwa kuchangia kuleta Maji mjini Kibaha .
Awali akiibua hoja hiyo ya miradi ya maji kusuasua alisema wakandarasi na watendaji husika wa idara hiyo watafutiwe kazi nyingine .
Chanyika alielezea wananchi wanataka kuona majibu na matokeo ya miradi inayotekelezwa na serikali na wahisani hivyo kama haisimamiwi kikamilifu inakatisha tamaa .
” Miradi ya nyuma tumeshapata hasara yenye zaidi ya mil. 132  na kutoletwa taarifa za kata tumekosa mil.100 ambazo tungewezeshwa na wahisani”alisisitiza Chanyika.
Diwani wa viti maalum mjini humo, Selina Wilson ,alizungumzia changamoto ya kusuasua kwa fedha zinatengwa kwa ajili ya vijana na wanawake .
Alisema katika halmashauri hiyo fedha hizo hazitolewi zote na zinawekwa kidogo .
Selina alieleza ,kwa mwaka 2015/2016 kati milioni 306 zilizotengwa lakini zilizopelekwa kwenye vikundi ni milioni 49 pekee,na zilizobaki milioni 256.
Alisema kwa 2016/2017 zimetengwa milioni 391 zilitolewa hadi sasa ni milioni 174.
Selina aliomba halmashauri hiyo itupie macho makundi hayo kwa kuyawezesha kupitia fedha zao zote zinazotengwa bila kuyabania .
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mji wa Kibaha,Maulid Bundala alisema licha ya miradi ya maji kudorora na miradi ya barabara iangaliwe .
Bundala alisema wakandarasi wa miradi ya miundombinu ya barabara wasimamiwe ili ijengwe kwa viwango vinavyotakiwa na kumalizwa kwa wakati.

UNCDF YAWEZESHA UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA BWAWA LA KALEMAWE

Posted by Esta Malibiche on JULY 31,2017 IN BIASHARA

SERIKALI ya Tanzania, imeshukuru Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) kwa kuwezesha watanzania kupambana na umaskini kupitia miradi wanayoidhamini au kuitafutia fedha.
Kwa miongo miwili UNCDF imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) katika mpango wa kupeleka madaraka kwa umma na shughuli za maendeleo ya kiuchumi .
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Aisha Amour kwenye ufunguzi wa kongamano la siku 2 la Wadau wa Ufugaji Samaki Kibiashara Bwawa la Kalemawe lililoko wilaya ya Same mwishoni mwa wiki.
“Tunafurahishwa kwa namna ya pekee na UNCDF kwa jitihada zake zinazoendeshwa kupitia katika Mpango wa Ufadhili Miradi ya kiuchumi (LFI),” alisema Iyombe na kuongeza:
“Tunapokutana hapa tunapewa fursa na kufunuliwa uzoefu wa ushiriki wa UNCDF katika miradi mbalimbali, safari hii tukishuhudia hatua yake ya kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro.”
 Meneja wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo kuhusu mradi wa ufugaji samaki katika shamba hilo kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi ya mafunzo juu ya ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo lililopo wilaya ya Bagamoyo. Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Mh. Naghenjwa Kaboyoka na Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Staki pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (wa pili kulia).
Pamoja na kushukuru kwa hatua mbalimbali zilizofikiwa na taasisi hiyo katika kusaidia watanzania, aliwataka wakazi wa Same kuhakikisha kwamba mradi huo ulioundiwa kampuni ili kwenda kibiashara unafanikiwa na kuwa mfano kwa wengine.
Halmashauri ya wilaya ya Same, na jamii inayozunguka bwawa la Kalemawe wanashirikiana na UNCDF kuboresha miundo mbinu ya bwawa hilo na kuwezesha uwapo wa uwekezaji kwa kuanzisha kampuni.
Kampuni hiyo iliyosajiliwa ya Kalemawe Dam Investment Limited katika mpango maalum (SPV) inamilikiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Same, halmashauri ya vijiji sita, wakala wa serikali, watu binafsi pamoja na makundi ya kijamii.
Kuwapo kwa kampuni hiyo ni juhudi zinazofanywa za kuwezesha uhusiano mahsusi wa kibiashara unaohusisha ubia wa Serikali, Binafsi na jamii (PPCP) kwa kutoa umiliki linganifu mpaka katika ngazi za chini za mamlaka za kijiji, ambazo kimsingi ndizo wamiliki wa maliasili muhimu ya ardhi kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya Mwaka 1999.
Viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) wakiwa kwenye ziara fupi ya mafunzo kuhusu ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba la ufugaji samaki la Ruvu lililopo wilaya ya Bagamoyo.
Mradi huo wa Ufugaji wa Samaki Kibiashara wa Bwawa la Kalemawe ni zao la ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Same, Kata za Ndungu na Kalemawe, asasi zisizo za kiserikali na wadau wa maendeleo walioazimia kukarabati na kufufua bwawa hilo na mfumo wake wa kilimo cha umwagiliaji.
UNCDF kwa kushirikiana na wabia wake waitwao Mikono Tayari (ambao ni kundi linaloundwa na washirika kutoka Tanzania na Norway) ni wataalamu katika mradi hu wa ufugaji samaki kwa pamoja na SPV ya Same na washirika wake.
Katika kongamano hilo Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Staki amesema wilaya yake ipo tayari kutekeleza mradi huo ambao una manufaa makubwa si tu kwa watu wa Kalemawe na vijiji vinavyozunguka bali pia na halmashauri ya wilaya ya Same.
Meneja wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo kuhusu vyakula vinavyotumika kulisha samaki wanaofugwa kwenye shamba hilo kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi ya mafunzo juu ya ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo lililopo wilaya ya Bagamoyo.
Akishiriki katika mjadala aliwataka wanakalemawe kutambua umuhimu wa mradi huo na kwamba hicho ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa watu binafsi na jamii kwa ujumla.
Mradi huo ambao ni sehemu ya programu kubwa ya kubadili watu wenye makazi kuzunguka bwawa hilo umelenga katika siku za usoni kuzalisha samaki na vifaranga vyake.
Ili kuwa na uelewa mkubwa wa kufanya biashara hiyo ya samaki, madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa za vijiji vinavyotengeneza kampuni hiyo ya Kalemawe walitembelea shamba la samaki Ruvu ambapo waliona shughuli mbalimbali zinazoendelea katika shamba hilo ili iwe mfano kwao
Pamoja na kuuza samaki shamba hilo ambalo lipo kilomita 20 kutoka Bagamoyo na kilomita 13 hivi kutoka Mlandizi linafuga samaki aina ya sato na hutotolesha vifaranga laki moja kila wiki kwa kulingana na oda zilizopo.
Ziara ya mafunzo ikiendelea katika shamba la kufuga samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamoyo. Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki (wa pili kushoto) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (katikati) pamoja na ujumbe ulioambatana nao kwenye mafunzo hayo ukitazama jambo katika shamba hilo.
Mmoja wa viongozi katika mradi huo Khumbo Kanthenga alisema kwamba mradi huo ambao bado unapanuliwa kufikia mabwawa sitini kwa sasa umelenga kutoa vifaranga kwa mujibu wa oda na pia kuuza samaki ambao wapo tayari kuingia sokoni samaki hao wanafikia gramu 350 na kuendelea.
Naye Mbunge wa Same Mashariki, Naghenjwa Kaboyoka ambaye alikuwapo katika kongamano hilo alielezea haja ya wananchi wengi kutambua mipaka yao na kuhakikisha kwamba dhamira safi iliyopo ya kufufua bwawa hilo na kubadilisha maisha ya wananchi inafikiwa.
Wakifunga Kongamano hilo UNCDF ili shukuru ushirikiano mkubwa wa karibu ambao umeonyeshwa na washiriki wa warsha hii ya wadau kuanzia serikali kuu, mkoa, willaya na viongozi wa vijiji sita vinavyohusika na utekelezaji wa mradi na pia iliahidi kua mashirika mengine ya umoja wa mataifa watashirikishwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa mradi huu na miradi mingine mbalimbali katika eneo hili la bwawa la samaki.
Eneo ambalo linaandaliwa kwa ajili ya bwawa la kufugia samaki katika shamba la kufugia samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamayo.
Wafanyakazi wa shamba la kufugia samaki la Ruvu wakitega nyavu kwa ajili ya kuonyesha samaki katika moja ya mabwawa kwenye shamba hilo wakati wa ziara hiyo fupi ya mafunzo.
Mmoja wa wafanyakazi wa shamba hilo akiwa ameshikilia samaki aina Sato wanaofugwa kwenye shamba hilo.
Meneja wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (tisheti nyekundu) akitoa maelezo katika chumba maalum cha kutotolea vifaranga vya samaki kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliokuwa kwenye ziara fupi ya kupata elimu juu ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo lililopo wilaya ya Bagamoyo.
Mshauri wa Shamba la Samaki la Ruvu, Per Gjoede akitazama mabwawa ya samaki katika shamba la kufugia samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Shamba la Samaki la Ruvu, Daudi Makobole (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki (kulia) pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (kushoto), Mshauri wa Shamba la Samaki la Ruvu, Per Gjoede (wa pili kushoto) baada ya kuhitimisha ziara fupi ya mafunzo katika shamba hilo.
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini, Peter Malika akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour akizungumza wakati ufunguzi wa warsha ya siku mbilli ya wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki.
Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Staki akitoa salamu kwa wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe wakati wa warsha hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia uwekezaji katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF), Imanuel Muro akisimamia majadiliano kuhusu wa kampuni ya bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji samaki kibiashara katika bwawa hilo iliyoandaliwa na UNCDF na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkiurugenzi Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dr. Charles Mhina akitoa maoni kwenye warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kijiji cha Misufini kata ya Ngungu wilaya ya Same, Omari Mganga akiwasilisha maoni wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mgandu kata ya Bendera wilaya ya Same, Merina Mhando akichangia maoni katika warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Mawasiliano na Ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini, Jacqueline Namfua-Mwombela na Mshirika wa Programu UNCDF, Andulile Mwabulambo wakifurahi jambo wakati wa warsha hiyo iliyofanyika wmishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni washirki wa warsha ya siku mbili ya mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyoandaliwa na UNCDF na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.


Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.