Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumanne, 26 Juni 2018

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA UGENI KUTOKA LIWALE MKOANI LINDI

Posted by Esta Malibiche on JUNE 26,2018 IN NEWS
V25A2171
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akisalimiana na Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi kuchauka (kulia) na Ndg. Jivunie Mbunda (aliebebwa) ambae ni mlemavu wa kimo kutoka Liwale Mkoani Lindi walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
V25A2200V25A2186V25A2184
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi kuchauka (kulia) pamoja na wanandoa Ndg. Jivunie Mbunda ambae ni mlemavu wa kimo (kushoto) na Mkewe Ndg. Amina Mbunda wote kutoka Liwale Mkoani Lindi (wa pili kushoto) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
V25A2178
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi kuchauka (kulia) na Wana ndoa Ndg. Amina Mbunda (kushoto) na Mumewe Ndg. Amina Mbunda (aliebebwa) ambae ni mlemavu wa kimo kutoka liwale Mkoani Lindi walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 (PICHA NA OFISI YA BUNGE

DOKTA PHILIP MPANGO AHITIMISHA MJADALA WA BAJETI BUNGENI JIJINI DODOMA

Posted by Esta Malibiche on JUNE 26,2018 IN NEWS
AC3A3525
Baadhi ya wadau wakifuatilia kwa makini mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, kabla ya Waziri mtoa hoja Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) hajahitimisha hoja hiyo ya Bajeti, Bungeni, Dodoma.
AC3A3548
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), naMwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, wakizungumza jambo kabla ya kuhitimishwa kwa hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma.
AC3A3581
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifuatilia hoja za Mawaziri wakati wa kuhitimisha hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni, Dodoma.
AC3A3682
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kuhitimishwa kwa hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma, ambapo alizitaka Halmashauri kuendelea kubuni miradi ya kimkakati ili kujiongezea kipato.
AC3A3788
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihitimisha hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni, Dodoma, ambapo ameahidi kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma kwa ufanisi na kuwatahadharisha wabadhilifu wa fedha za umma kuwa ni sawa na kula sumu.
AC3A3824
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), na Waziri wa Madini, Mhe. Anjellah Kairuki (Mb), wakijadili jambo muda mfupi baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma.
AC3A3832
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu (katikati), akipeana mkono na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge, katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma baada ya kuhitimishwa kwa hoza za Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19, ambapo mtoa hoja  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) aliwapongeza wabunge wengi kwa kutoa hoja zenye kujenga ili kuboresha Bajeti hiyo, kulia ni Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi.
AC3A3846
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akipongezwa na Mbunge wa Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza kwa hitimisho zuri la Hoja ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa kusisitiza weledi katika usimamizi wa fedha za umma.
AC3A3854
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akipongezwa na Mbunge wa Kwimba Mhe. Mansoor Sharif, baada ya kuhitimisha ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mipango madhubuti ya kufikia uchumi wa kati.

AC3A3862
NaibuWaziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akipongezwa na Mhe. George Simbachawene (Mb) (kushoto) na Waziri wa Habari,  Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, kwa kujibu hoja za wabunge kwa ufasaha wakati wa kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni, Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango

DK. KIGWANGALLA AFUNGUA WARSHA YA KITAIFA YA WADAU WANAOPINGA VITENDO VYA UHALIFU DHIDI WANYAMAPORI NA MISITU NCHINI

Posted by Esta Malibiche on JUNE 26,2018 IN NEWS
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. Warsha hiyo imelenga kujadili na kuainisha mahitaji na vipaombele vya sekta ya mahakama na mashtaka ya kudhibiti uhalifu huo.  
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Iddi Mfunda (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga (wa pili kulia) na Mkuu wa ofisi wa Shirika la Ufuatiliaji wa Wanyamapori (TRAFFIC), Julie Thomson (kulia) wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa warsha ya siku moja ya wadau wanaopinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. 
 Baadhi ya wadau wa kitaifa walioshiriki hafla hiyo wakiimba wimbo wa Taifa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. Warsha hiyo imelenga kujadili na kuainisha mahitaji na vipaombele vya sekta ya mahakama na mashtaka ya kudhibiti uhalifu huo. 
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini. (Picha na Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii)

WAZIRI MKUU AONGOZA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA MKOANI IRINGA

Posted by Esta Malibiche on JUNE 26,2018 IN KITAIFA.
PMO_0711
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wananchi, kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani, uwanja wa Kichangani Mkoani Iringa Juni 26, 2018.
PMO_0375

PMO_0378
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia tumbo la Juma Desail, kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani, ambaye alipata tatizo la kupasukiwa na kete ya dawa za kulevya tumboni na kunusurika kifo wakati akisafirisha, kwenye Kiwanja cha Kichangani Mkoani Iringa Juni 26, 2018.
PMO_0393
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya picha iliyochorwa na waathirika wa dawa za kulevya, kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Kichangani Mkoani Iringa Juni 26, 2018. Kutoka kushoto ni  Juma Desail, Said Bandawe, Nuru Saleh, Karim Banji,
PMO_0420
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wanao hamasisha mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya mashuleni, kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani, uwanja wa Kichangani Mkoani Iringa Juni 26, 2018. Kutoka kushoto ni  Salha Said, Regina Simon, Ramadhan Said, Asia Mohamed
PMO_0470
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia chupa ambayo hutumika kusafirishia dawa za kulevya, kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani, kwenye uwanja wa Kichangani Mkoani Iringa Juni 26, 2018. Kushoto ni RCO Iringa Deusdedit Kasindo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha dawa za kulevya wa Mkoa wa Iringa Simon Kitana.


Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza na kushoto ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama.
IMG_1161
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.
IMG_1063
IMG_1085
IMG_1095
IMG_1107
IMG_1117
IMG_1167
Baadhi ya wananchi pamoja na wadau wa kupambana na dawa za kulevya wakipita kwa bashasha mbele ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.
IMG_1011
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Sheria Edwin Kakolaki alipotembelea banda la mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevyawakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.

PMO_0681
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mmoja wa waathirika wa dawa za kulevya Christina Joseph, kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani, katika Kiwanja cha Kichangani Mkoani Iringa Juni 26, 2018. kutoka kushoto ni Mbunge wa Biharamulo Oscar Rwegasira Mukasa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
PMO_0688
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wanao hamasisha mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya mashuleni, kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani, uwanja wa Kichangani Mkoani Iringa Juni 26, 2018. Kutoka kushoto ni  Asia Mohamed, Regina Simon, Salha Said, Ramadhan Said.PMO_0746
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wananchi, kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupambana na Dawa za Kulevya Duniani, uwanja wa Kichangani Mkoani Iringa Juni 26, 2018. Kutoka kushoto ni  Asia Mohamed, Regina Simon, Salha Said, Ramadhan Said.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
………………

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kumewezesha kukamatwa kwa wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wakitamba kwamba hawawezi kuguswa.
“Sasa hivi dawa zinakamatwa kwelikweli na wale wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliokuwa wakijiita vigogo na kutamba kuwa hawakamatwi na hata wakikamatwa wanaachiwa, wameanza kuikimbia nchi,” amesema. 
Ameyasema hayo leo (Jumanne, Juni 26, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika uwanja wa Gangilonga, mkoani Iringa. 
Waziri Mkuu amesema Serikali baada ya kuanzisha Mamlaka hiyo, iliiwezesha kwa kuipatia rasilimali fedha, watendaji na vitendea kazi na tayari mafanikio yameanza kuonekana.
Amesema kila mmoja anapaswa kuliona suala hilo la dawa za kulevya kama jambo hatari kwa mustakabali wa Taifa letu na akasisitiza kuwa watu wasioneane haya katika vita hiyo kwa kuwataja wahusika kwa sababu huuzwa katika mitaa yao na wauzaji wanawafahamu. 
“Nawasihi viongozi wa siasa, dini pamoja na vyombo vya habari, tuendelee kukemea kwa nguvu zote matumizi na biashara ya dawa za kulevya,” amesema.
Waziri Mkuu amesema matumizi ya dawa za kulevya yapo zaidi kwenye miji mikubwa hasa ya Dar es Salaam, Arusha, Tanga na Mwanza, pia kasi ya kuenea kwa matumizi hayo kwenye miji midogo nayo ni kubwa hasa katika mikoa ya Iringa, Dodoma na Mbeya na Morogoro. 
Wakati huohuo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama amesema tatizo la dawa za kulevya limeiathiri duniia na watu wengi wameathirika na janga hilo ikiwemo jinsia na rika zote. 
Amesemabiashara ya dawa za kulevya imesababisha madhara makubwa mbalimbali nchini yakiwemo ya kiafya, kijamii, kiuchumi, kimazingira, kisiasa na kiusalama. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni“tujenge maisha yetu, jamii yetu na utu wetu bila dawa za kulevya

“Zipo dalili kwamba, endapo biashara hii itaachwa iendelee, athari zaidi zitajitokeza ikiwemo kuingiliwa kwa misingi ya kiutawala na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kwa manufaa  yao  binafsi,” amesisitiza.

Awali,  mmoja wa waathirika wa dawa hizo Bi. Reja Chawe ambaye alitumia dawa hizo kwa muda wa miaka 15 na alianza kutumia akiwa kidato cha pili, alisema alianza akiwa kidato cha pili baada ya kushawishiwa na rafiki yake wa kiume na alianza kwa kutumia bangi. 
Bi Reja alisema kwa sasa ameacha ila anaumia sana akiona vijana wenzake wanaitumia dawa hizo kwa sababu yeye alipata matatizo makubwa wakati akitumia dawa hizo ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ambazo ni za kujidhalilisha.
“Nilikuwa naitwa majina mabaya, nililala makaburini na nilifanya kazi ya kuchimba makaburi ya watoto wachanga na kuwazika. Mimi nilikuwa napitisha hata mwezi bila ya kuoga, pia nilikuwa naiba. Sikupenda, ila mkumbo tu, nawaomba vijana wenzangu waachane na dawa za kulevya,” amesema.
Muathirika mwingine, Bi. Christine Mponzi ambaye bado anatumia dawa ameiomba Serikali imsaidie ili aweze kuachana na dawa hizo ambazo alianza kutumia miaka 25 iliyopita na sasa anasikia maumivu ila anashindwa kuacha kutumia dawa hizo.
Alisema dawa hizo zimesababisha atengane na familia yake, ambapo watoto wake wawili nao wamemkataa kutokana na hali aliyokuwa nayo.” Dawa za kulevya ni hatari mimi nilikuwa mzuri na nilikuwa na mume wangu na watoto wamenikataa kwa sababu mama yao wananiona sina hadhi. Nilianza kufanya biashara kabla ya kutumia,”. 
Tayari Serikali imesikia kilio chake, baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista kumkabidhi kwa muendeshaji wa nyumba za upataji nafuu (sober house) ili aanze kupatiwa matibabu.

Jumamosi, 23 Juni 2018

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA RODRICK MPOGOLO AWATUNUKU VYETI VYA KUHITIMU WANACHAMA 281 KUTOKA UMOJA WA VIJANA CCM VYUO NA VYUO VIKUU MKOANI IRINGA LEO HII

Posted by Esta Malibiche on JUNE 23,2018 IN SIASA


Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg Rodrick Mpogolo akizungumza na Wahitimu Makada wa CCM Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga,yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Siasa ni kilimo Mkoani Iringa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Mwl Raymond Mwangwala akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapindui Mkoa wa Iringa Ndg.Albert Chalamila akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo 


 katibu wa chama cha Mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa Christopher Magala akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo 

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.


 Wahitimu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa Wakiimba nyimbo Mbali mbali za Chama mara baada ya Mgeni rasmi kuzungungumza katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC) Bi Theresia Mtewele akiongoza meza kuu kuimba nyimbo Mbali mbali za Chama mara baada ya Mgeni rasmi kuzungungumza katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.

Viongozi na wahitimu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa wakiburudika kwa pamoja kwa nyimbo Mbali mbali za Chama mara baada ya Mgeni rasmikuzungungumza katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.


Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg.Rodrick Mpogolo akimkabidhi cheti cha pongezi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndg.Kenani kiongosi katika sherehe ya Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo



 Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg.Rodrick Mpogolo akitoa vyeti kwa wahitimu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogolo akipokea baadhi ya bendera na jezi za chadema wakati akimkaribisha ndg Godfrey Maiko aliojiunga rasmi na CCM Leo  katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogolo akimvisha kofia ya CCM ndg Godfrey Maiko aliojiunga rasmi na CCM Leo  katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza akipeana Mkono na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini Ndg Damalo aliporejesha kadi ya Chadema na Kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi Leo katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogoro akifurahi pamoja na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini Ndg Damalo aliporejesha kadi ya Chadema na Kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi Leo katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogoro akizungumza  mara baada ya kumpokea Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini Ndg Damalo aliporejesha kadi ya Chadema na Kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi Leo katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo kulia ni Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl Raymond Mwangwala.


PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI CCM BLOG