Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Ijumaa, 28 Aprili 2017

MIGODI INAYOMILIKIWA NA KAMPUNI YA ACACIA YAWA KIVUTIO KATIKA MAONESHO YA WIKI YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

Posted by Esta Malibiche onAPRIL 28,2017 IN NEWS

Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya mahala pa kazi yanayofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Maonesho haya yanayohusisha kampuni na Taasisi mbalimbali nchini yanaratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakiweka sawa moja ya picha inayoonesha eneo ambalo shughuli za uchimbaji unafanyika.
Afisa Uhakiki na Usalama katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Amina Mohamed akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo katika maeonesho ya wiki ya usalama mahala pa kazi ndani ya viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Afisa Afya katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ,Tumaini Sylivanus akitoa maelezo ya namna wanavyotoa huduma ya Afya kwa wafanyakazi wa Mgodi huo pindi wapatapo matatizo.
Mmoja wa Wakazi wa Kilimanjaro akipewa maelekezo ya namna ya kutumia kifaa maalumu kinachotumika katika zoezi la uzimaji wa moto pindi yatokeapo majanga ya Moto.Nyuma yake ni mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa Viwango wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,Setieli Kimaro akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la modi huo unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Deogratius Nyantabano akitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea banda la mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi yanyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ,Kilimanjaro.
Afisa Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Mustapher Mlewa akieleza jambo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda hilo.
Daktari kutoka Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Dkt Ludovick Silima akitoa maelezo juu ya usalama kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la mgodi huo wakati wa maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi yanayoendelea katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Afisa Mazingira katika Mgodi wa north Mara ,Sara Cyprian akionesha picha na maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi.
Afisa Usalama katika mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Samweli Nansika (aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la mgodi huo.
Mkuu wa Idara ya Usalama na uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ,Emanuel Erasto(katikati) akitoa maelezo namna amavyo wanaweza kumuokoa mtu aliyepata athari iliytokana na kemikali.
Eneo maalumu la kumuogesha mtu aliyepata athari ya kemikali.
Afisa usalama akita huduma ya kumsafisha mtu aliyepata athali ya kemikali akiwa nje ya bafu hilo la kumuogeshea ili na yeye asipate madhara.
Wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi wakionesha namna ambavyo wanaweza msaidia mtu aliyepatwa na janga la Moto.
Kifaa Maalumu kinachotumika katika kubeba mwili wa mtu aliyepata madhara akiwa katika shimo wakati wa uchimbaji wa Dhahabu.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu akitoa maelezo kwa wananchi walitembelea banda hilo namna ambavyo wanaweza kunyanyua Gari pamoja na Mawe yaliyomuangukia mtu wakati akitekeleza majukumu yake kwa kutumia kifaa maalumu kinachojazwa upepo (Air Bag).
Mkuu wa Idara ya Usalama na Uokoaji katika Mgodi wa North Mara ,Emanuel Erasto akitoa maelezo namna wanavyoweza kumukoa mtu aliyepatwa madhara akiwa chini ya mgodi .
Dkt Ludovick Silima akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la Mgodi wa Buzwagi.
Afisa Mahusiano katika Mgodi wa Bulyanhulu akitoa maelezo ya namna Mgodi huo unavyo tekeleza majukumu yake ukitoa kipaumbele katika masuala ya Usalama na Afya kwa watumishi wake.
Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi ,Magesa Magesa akitoa maelezo namna mgodi huo ulivyoshiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo ujengaji wa vyumba vya madarasa,zahanati,maji pamoja na suala la kuhamasisha michezo katika maeneo yanayozunguka mgodi huo.

Na Dixon Buagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA KIBINADAMU KATIKA VYANZO VYA MAJI IRINGA



Posted by Esta Malibiche on APRIL 28,2017 IN NEWS


Na. Dennis Gondwe, Iringa
Serikali mkoani Iringa imepiga marufuku shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji wilayani Iringa ili kunusuru uendelevu wa bonde la mto Ruaha mkuu.
Marufuku hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa kikosi kazi namba tatu cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha mkuu ambaye pia ni Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu baada ya kukagua chanzo cha maji cha Kivalali kilichopo katika kijiji cha Bandabichi wilayani Iringa katika ziara ya kukagua uharibifu wa vyanzo vya maji katika kata ya Ifunda.
Ayubu alisema “kikosi kazi hiki kimeundwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuangalia njia sahihi ya kuhifadhi ikolojia ya vyanzo vyote vya mto Ruaha mkuu. Baada ya kutembelea vyanzo vya maji, ni kweli shughuli za kibinadamu zinafanyika ndani ya hifadhi ya vyanzo hivyi. Naagiza mazao yote yaliyolimwa ndani ya hifadhi ya maji iliwa ni pamoja na vitindi vya ulazi viondolewe”. Alisema kuwa kikosi kazi hicho kilichoundwa na Jamhuri kina lenga maslahi mapana ya Taifa tofauti na matakwa ya mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu wachache.
Wapo baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kuvamia kidogo kidogo maeneo yenye maslahi ya kitaifa na baadae kujimilikisha wakidhani serikali wanaimiliki wao. Tabia hiyo sasa ifike mwisho, lazima kila mwananchi aheshimu na kufuata sheria na taratibu za nchi kwa ustawi wa taifa zima” alisema Wamoja.
Wakati huohuo, Mkurugenzi mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi alishauri eneo lote la mkondo wa maji libainishwe na kupandwa miti ya asili. Alisema kuwa miti hiyo ya asili itasaidia kutambua mipaka ya maeneo ya vyanzo vya maji pamoja na kusaidia uhifadhi wa vyanzo hivyo na kuzuia kuvamiwa kiholela. Alisema kuwa uhifadhi wa vyanzo vya maji utasaidia uendelevu wa shughuli nyingine za kimandeleo kuanzia uhifadhi wa mazingira, wanyama, watumia maji na shughuli za kilimo nchini.

ASILIMIA 60 YA MAJI YANAPOTELEA KWENYE MIFEREJI ISIYOSAKAFIWA


Posted by Esta Malibiche on APRIL 28,2017 IN NEWS


 Na Denis Gondwe
 Iringa
Wastani wa asilimia 60 ya maji yanapotea yanapopita katika mifereji ambayo haijasakafiwa na kuchangia katika upungufu wa maji kwenye mzunguko wake.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu baada ya kikosi kazi namba tatu kukagua mfereji wa asili katika skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi inayohudumia vijiji sita katika kata za Mboliboli na Itunundu katika tarafa ya Pawaga wilayani Iringa jana alipoongoza kikosi kazi cha kunusuru ikolojia ya bonde la mto ruaha.
Ayubu alisema kuwa jitihada zinahitaki kuhifadhi mazingira yanayozunguka skimu ya umwagiliaji ya mkombozi yenye mfereji wa asili. Aidha, amepiga marufuku matumizi ya pampu za kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji kwa sababu hakuna kibali kilichotolewa kwa matumizi ya pampu katika skimu hiyo. “Matumizi ya pampu ni marufuku kuanzia leo. Pampu zote ziondolewe katika skimu hii kwa sababu zipo kinyume na sheria” alisisitiza Ayubu.
Ayubu aliongeza kuwa jamii nzima inategemeana katika uhitaji na matumizi ya maji na kusisitiza umakini katika matumizi yake. “Sote tunategemeana. Maji yakitoka hapa yanaenda kuzalisha umeme bwawa la mtera, yakitoka bwawa la mtera yanaenda kuzalisha umeme Kidatu, yakitoka kidatu yanaenda katika mashamba ya miwa kilombero” alisema Ayubu.
Wakati huohuo, mwenyekiti wa kikosi kazi hicho aliwataka wafugaji wenye mifugo mingi kujipanga kuvuna mifugo yao ili iendane na ukubwa wa ardhi iliyopo. Alisema kuwa wingi wa mifugo hauendani na tija inayotokana na mifugo hiyo zaidi ya kusababisha uharibifu wa mazingira.
Nae wakili wa serikali mkuu Benard Kongola kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) alisema kuwa mwananchi yeyote atakaye kamatwa akijihusisha na shughuli za kilimo ndani ya eneo la mita 60 kutoka ukingo wa mto ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria. Aidha, aliwataka wale wote wanaojishughulisha na kilimo ndani ya eneo hilo kuacha kabla ya zoezi la kuwakamata litakapoanza baada ya wiki moja.

Alhamisi, 27 Aprili 2017

DK MAGUFULI MGENI RASMI MEI MOSI


Posted by Esta Malibiche on APRIL 27,2017 IN NEWS
Tokeo la picha la john magufuli

RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kitaifa, huku kilio kikubwa cha vyama vya wafanyakazi kikiwa kukosekana kwa mikataba ya hali bora kazini.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Taifa lilipaswa kuwa na waajiriwa milioni 3.7 katika sekta iliyo rasmi, lakini waliopo ni 650,000 pekee, hali inayoashiria kutokuwa na mikataba.
Katibu Mkuu wa Tucta, Yahaya Msigwa alisema hayo jana mjini Moshi ikiwa ni maandalizi ya Mei Mosi itakayofanyika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).
“Tayari tumemwandikia Rais Dk Magufuli kumuomba awe mgeni rasmi, kimsingi sherehe zote kitaifa mgeni rasmi ni yeye...tunazo ajenda za kumpa Rais, lakini moja ya mambo ambayo ni kero ni hili la mikataba ya hali bora kazini, wafanyakazi wengi wanafanya kazi kama vibarua na hawajui haki zao,” alieleza Msigwa.
 Alitolea mfano wa watumishi wa mashambani pekee nchini Kenya ni zaidi ya 700,000 na Afrika Kusini ni zaidi ya milioni moja na kwamba ipo haja kwa waajiri Tanzania kutafakari upya suala la maslahi ya wafanyakazi wao na rais anapaswa kulisemea hilo.
 Aidha, Katibu Mkuu huyo wa Tucta alitaka waajiri kuruhusu kuundwa kwa mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kukutana na kujadili maslahi yao lakini pia kufanya kazi kwa tija zaidi.
Katika hatua nyingine, Msigwa alisema Tucta inaunga mkono kampeni ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kupambana na wafanyakazi hewa sanjari na mpango wa kupunguza matumizi ya serikali.
 “Pamoja na nia njema ya serikali katika kupambana na wafanyakazi hewa, lakini tunaomba haki itendeke na isitokee mfanyakazi ameonewa kwa namna yoyote ile kwani huko ni kuwakatisha tamaa wafanyakazi waadilifu na waaminifu,” alieleza.

Maadhimisho ya Mei Mosi yatahusisha pia kujengwa kwa mabanda ya kuoneshwa kwa shughuli mbalimbali za kisekta nchini


TEHAMA YAHAMASISHA WANAFUNZI WA KIKE KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

Posted by Esta Malibiche on APRIL 27,2017 IN NEWS


Maadhmisho ya siku ya wasichana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  TEHAMA kimataifa yamefanyika leo,ambapo Nyanda za juu kusini siku hii imeadhimishwa katika shule ya Sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo Mkoani Iringa. 


Mgeni rasmi  Katika Maadhimisho hayo alikuwa ni Maneja wa TEHAMA kanda ya nyanda  za juu kusini ambae pia ni msimamizi wa mamlaka ya mawasiliano TCRA  Kanda Eng. Lilian Mwangoka.


Akizungumza mapema leo hii na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa Mkoani  hapa,alisema kuwa,lengo la siku hii ni kuwahamasisha na kuchochea wasichana kuchagua masomo ya sayansi na kuelimisha juu ya matumizi sahihi ya TEHAMA.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema kuwa ;Ongeza wigo badili Mtazamo''


Eng. Lilian Mwangoka,akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda katika maadhimisho ya siku ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yaliyoadhimishwa kimataifa leo hii

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakishiriki maadhimisho ya suku ya wasichana na TEHAMA leo hii
Eng Liliani Mwangoka akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliojibu vizuri maswali yanayohusu TEHAMA na kupewa zawadi  za Tisheti na kofia
Wanafunzi walioshinda kujibu Maswali wakiwa katika picha ya pamoja

Eng Liliani Mwangoka akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliojibu vizuri maswali yanayohusu TEHAMA na kupewa zawadi  za Tisheti na kofia

Eng Liliani Mwangoka akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliojibu vizuri maswali yanayohusu TEHAMA na kupewa zawadi  za Tisheti na kofia



Faraja Msigwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ifunda akizungumza na vyombo vya habari[Havipo pichani]mara baada ya maadhimisho hayo.