Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Alhamisi, 31 Mei 2018

DKT. KIJAJI AITAKA BENKI YA ABC KUPELEKA HUDUMA VIJIJINI KUCHOCHEA SEKTA YA KILIMO NA VIWANDA

Posted by Ssta Malibiche on MEI 31,2018 IN BIASHARA
AC3A0399
Baadhi ya waalikwa katika shughuli ya ufunguzi wa tawi jipya la  Benki ya ABC Jijini Dodoma lililofunguliwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
AC3A0402
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge, wakizungumza jambo kabla ya kufungua rasmi tawi la Benki ya ABC Jijini Dodoma.

AC3A0421
Kaimu Mkurugenzi wa tawi la Benki ya ABC Bw. Imani John, akieleza kuhusu lengo la kufungua rasmi tawi jipya la Benki hiyo Jijini Dodoma kuwa ni kuleta karibu huduma za kibenki kwa wananchi wa Jiji hilo.
AC3A0423
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde, akiishukuru Benki ya ABC kwa kuleta huduma za kibenki karibu na wananchi wa Jiji la Dodoma.
AC3A0444
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge, akiwataka wananchi wa Jiji la Dodoma kutumia fursa za huduma za kifedha zilizopo katika Jiji hilo ili kujiendeleza kiuchumi, wakati wa kufungua rasmi tawi jipya la Benki ya ABC Jijini Dodoma.
AC3A0471
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) akifungua rasmi tawi la Benki ya ABC  Jijini Dodoma, kushoto ni  Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde na wapili kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Dkt. Bilinith Mahenge.
AC3A0480
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kulia), akikata utepe kuashilia kufunguliwa rasmi kwa tawi jipya la Benki ya ABC Jijini Dodoma huku akishuhudiwa na Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo Bw. Imani John, Jijini Dodoma.
AC3A0519
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na wafanyakazi wa Benki ya ABC baada ya kufunguliwa rasmi kwa tawi jipya la Benki hiyo Jijini Dodoma.
AC3A0525
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi na wageni waalikwa baada ya kufunguliwa rasmi kwa tawi jipya la Benki hiyo Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango
……………….
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
SERIKALI imelipa madeni ya wakandarasi na watoa huduma mbalimbali yanayofikia zaidi ya shilingi trilioni 1.2 katika mwaka huu wa fedha hatua iliyochangia kuongeza ukwasi wa fedha katika jamii ikiwa ni hatua ya Serikali ya kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakua kwa haraka.
Hayo yamesemwa Jijini Dodoma, na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akifungua rasmi tawi la benki ya ABC, lililoanzisha huduma zake za kibenki mkoani humo tangu Januari mwaka huu.
Alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kuwaongezea uwezo wajasiriamali na wafanyabiashara waliotoa huduma Serikalini ili waongeze mzunguko wa fedha katika uchumi.
Ametoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na Benki hiyo ambayo riba yake haizidi asilimia 17 ili waweze   kuendeleza shughuli  za uzalishaji mali na huduma za jamii kwa kuwekeza katika miradi inayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi.
“Ni matarajio yangu kuwa sehemu kubwa ya mikopo itakayotolewa na Benki yetu ya ABC, itaelekezwa kwenye sekta ya kilimo na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo, vya kati, mifugo, uvuvi na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na misitu” alisema Dkt. Kijaji
Dkt. Kijaji alisisitiza umuhimu wa uwepo wa sekta imara ya fedha itakayochochea ujenzi wa viwanda vitakavyo saidia kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo pamoja na kukuza ajira kwa vijana.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo ya ABC Bw. Imani John, alieleza kuwa Benki yake yenye mtaji wa zaidi ya shilingi bilioni 67 imeendelea na jitihada zake za kupanua huduma zake ili kukidhi mahitaji ya kibenki ya wananchi.
Alisema kuwa benki yake imeanzisha huduma zake katika Jiji la Dodoma kufuatia utafiti uliofanyika hivi karibuni unaoonesha kuwa asilimia 13 pekee ya wakazi wa mkoa huo wanafikiwa na huduma za kipenki, pamoja na uamuzi wa benki hiyo wa kuunga mkono hatua ya Serikali ya kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde, ameishukuru Benki ya ABC kwa kupeleka huduma za kibenki karibu na wananchi wa Jiji la Dodoma na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuchangamkia fursa za mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge, pamoja na kuipongeza Benki ya ABC kwa hatua yake ya kusogeza huduma za kibenki kwa wakazi wa Jiji la Dodoma, amezitaka taasisi nyingine kuwekeza katika sekta hiyo pamoja na huduma nyingine kama vile ujenzi wa Hoteli za kisasa kwa kuwa mkoa huo una fursa nyingi ikiwemo ardhi yenye rutuba.
Benki ya ABC inafanya huduma zake hapa nchini kwa zaidi ya miaka 20 na inamilikiwa na wanahisa  akiwemo TDFC ambaye ni mbia wa ABC Holding Ltd, anayemiliki asilimia 14.7, kati ya asilimia hizo 14.7, asilimia 68 zinamilikiwa na ABC Holding ltd, na asilimia 32 zinamilikiwa na Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Jumatano, 30 Mei 2018

SERIKALI YAAGIZA WAMACHINGA WATENGEWE MAENEO YA KUFANYIA BIASHARA

Posted by Esta Malibiche on MEI  31, 2018 IN NEWS 

 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wamachinga wakati  wa kufungua  Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania- SHIUMA leo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Dodoma, Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wamachinga wakati  wa kufungua  Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania- SHIUMA leo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Dodoma, Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo  akiongea na baadhi ya viongozi wa shirika la umoja wa wamachinga Tanzania – SHIUMA leo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma, Jijini Dodoma.

......................................................
Na Angela Msimbira,
Wakuu wa Wilaya wameagizwa kuzisimamia halmashauri nchini kuhakikisha kuwa zinatenga maeneo maalum ya kufanyia biashara ndogondogo (machinga) ili  waweze kuendesha shughuli zao bila kuvunja sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali. 

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania – SHIUMA uliofanyika leo katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Dodoma, Jijini Dodoma.

Alisema Wakuu wa Wilaya wana wajibu wa kuratibu na kuhakikisha kuwa maeneo ya kufanyia bishara kwa wamachinga yanatengwa na Halmashauri ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa utaratibu bila kuvunja sheria za nchi. 

Aliongeza kuwa wamachinga ni watu muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania kwa kuwa wafanyabiashara wadogo ndio wanaoleta muunganiko wa watu katika kada mbalimbali wakiwemo wasomi wenye shahada, astashaada, kidato cha sita, kidato cha nne, darasa la saba na wasiosoma kabisa wote huunganika na kufanyabiashara kama wamachinga.

Alisema kati ya watanzania milioni 50, walioajiriwa serikalini na sekta ya umma ni 520,000, hivyo kundi kubwa ni la watu ambao ama wamejiajiri au wameajiriwa katika sekta binafsi. 

“Lakini kundi kubwa ni wale watu wanaojishughulisha kwa kutafuta riziki zao wenyewe ambao watu hao ndio unapata asilimia kubwa wako katika kundi la wamachinga,” alisema Mhe.Jafo na kuongeza:

“Utakuta mtu anafanyabishara katika mazingira magumu ambayo yanamfanya kila wakati kutokuwa na uhakika wa kupata kipato cha siku jambo ambalo linaathiri familia yake na kuongeza umaskini nchini, hivyo ifike mahali wakuu wa Wilaya waweke mikakati ya kuhakikisha wamachinga wote wanapatiwa maeneo bora ya kufanyia biashara ili wajikwamue kiuchumi,  “alisisitiza Waziri 

Aliongeza kuwa Serikali imejiwekea mkakati wa kutengeneza masoko mazuri na ya kisasa kwa kuweza kuweka mazingira bora kwa wamachinga kufanya biashara zao katika maeneo stahiki.

Aidha Waziri Jafo alisema kuwa Viongozi wanatakiwa kutafakari na kutatua kero ya maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara wamachinga, hivyo serikali imeanza mpango mkakati  wa ujenzi wa masoko mazuri ya kisasa ili wafanyabishara waweze kufanya kazi katika mazingira bora na tayari imetenga shilingi bilioni 149 kwa ajili ya ujenzi wa masoko, stendi za kisasa na viwanda vidogo.

 “Nimetoa maagizo soko lolote litakalojengwa lazima mustakabali wa wafanyabiashara wadogo wadogo waliokuwepo awali umejulikana na kuwa kipaumbele kwa kupatiwa maeneo ya kufanyia biashara pindi majengo hayo yanapokamilika hivyo viongozi wa halmashauri wahakikishe wanatoa kipaumbele kwa wafanyabiashara waliokuwepo awali,” alisema Jafo.

Alisema kuwa Serikali imekuwa ikiwekeza katika miradi mikubwa ikidhani inawagusa maskini lakini kwa bahati mbaya masoko mengi yanayojengwa wanaonufaika ni watu wenye fedha na kuwaacha wafanyabiashara waliokuwepo awali kabla soko kujengwa. 

Hivyo nawaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wananchi masikini wanapatiwa nafasi katika masoko hayo ili waweze kujiongezea kipato.

Amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri wote nchini kuhakikisha kuwa kabla soko halijaanza kujengwa kufanyike tathmini ya wafanyabishara waliokuwepo awali ili wawe kipaumbele pale soko linapokamilika.

Wakati huohuo Mhe. Jafo amewataka wamachinga nchini kuhakikisha wanajiunga na bima iliyoboreshwa ili iwawezeshe kuwasaidia pale wanapokuwa wagonjwa wao na familia zao kwa kuwa afya ni uhai.

Jumatatu, 28 Mei 2018

MWENGE WA UHURU WABARIKI KIWANDA CHA NEW FOREST

Posted by Esta Malibiche on MEI 25,018 IN NEWS

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Charles Kabeho akiweka jiwe la Msingi katika kiwanda  cha kuandaa na kutengeneza nguzo, kinachomilikiwa na  kampuni ya New Forest, kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha nguzo 800 kwa mzunguko mmoja na 1,600 kwa mizunguko miwili kwa siku pindi kitakapokamilika mwezi ujao.











KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Charles Kabeho mapema leo ameweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kuandaa na kutengeneza nguzo, mali ya kampuni ya New Forest, kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha nguzo 800 kwa mzunguko mmoja na 1,600 kwa mizunguko miwili kwa siku pindi kitakapokamilika mwezi ujao.

Kujengwa kwa kiwanda hicho kumedhihirisha juhudi za wilaya hiyo chini ya mkuu wake wa wilaya, Asiah Abdalla za kutekeleza kwa vitendo mkakati wa mkoa wa Iringa wa ujenzi wa viwanda 100 ifikapo Desemba mwaka huu.
  
Ujenzi wa kiwanda hicho kinachojengwa kwa zaidi ya Sh Bilioni 1.7 katika kijiji cha Lundamatwe wilayani humo ulianza Januari mwaka huu.

Akitoa taarifa ya ujenzi kwa kiongozi huyo, mwakilishi wa kampuni ambaye pia ni Afisa Mahusiano na Maendeleo ya Jamii wa kampuni hiyo, Robert Nyachia alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kutaifanya kampuni yao iwe na uwezo wa kuzalisha nguzo 180,000 kwa mwaka na kutoa ajira zaidi ya 100 wakati wote wa uzalishaji.

“Lakini pia kitatoa hamasa ya uhifadhi wa mazingira kupitia kilimo cha miti katika maeneo yaliyo wazi ambayo hayatumiki kwa kilimo na ufugaji na kutoa soko la uhakika la miti yote itakayokidhi vigezo vya ubora toka kwa wananchi,” alisema.

Pamoja na ujenzi wa kiwanda hicho, Nyachia alisema kampuni yao ina miliki kisheria shamba la ekari 5,000 za miti wilayani Kilolo ambazo kati yake ekari 2,400 zimepandwa miti aina ya milingoti ambayo ni malighafi ya kuzalisha nguzo na ekari 2,600 za miti aina ya misindano.

Kwa ufadhili wa serikali ya Finland na Mfuko wa Misitu Tanzania, alisema kampuni hiyo imewawezesha pia wakulima zaidi ya 1,200 kupanda miti zaidi ya 2,400,000 wilayani humo.

Akizungumzia mahusiano ya kampuni na jamii inayozunguka miradi yao, alisema kampuni imetumia zaidi ya Sh Bilioni 2.2 kuchangia shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii ya wilaya hiyo.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa zahanati tatu, nyumba mbili za waganga, nyumba moja ya mwalimu, wodi ya wajawazito na wagonjwa, vyumba vinne vya madarasa, mabweni ya wasichana na ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule mbalimbali za msingi za wilaya hiyo.

Akiipongeza kampuni hiyo, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru aliwataka wazalishaji wa nguzo hizo nchini kuzalisha kwa wingi ili kufikia mahitaji ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

“Nchi ina malighafi za kutosha ambayo ni miti ya kuwezesha uzalishaji wa nguzo hizo kwa wingi. Serikali haina sababu ya kuagiza nguzo toka nje ya nchi kama viwanda vya ndani vinaweza kukidhi mahitaji ya soko kubwa la Tanesco na masoko mengine,” Kabeho alisema.

Taarifa ya Tanesco iliyotolewa mjini Iringa mwaka jana na Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji wa Huduma kwa Wateja, Joyce Ngayhoma inaonesha Tanesco pekee yake inahitaji nguzo zaidi ya 500,000 kila mwaka, kiasi ambacho soko la ndani limeshindwa kutosheleza.

“Kuna wakati tulilazimika kuagiza nguzo kutoka nje ya nchi kwasababu ya changamoto hiyo; wito wetu kwa wazalishaji wa ndani, waongeze uzalishaji ili kutosheleza mahitaji na wazingatie ubora unaotakiwa na shirika,” alisema.

Alisema shirika limejiwekea lengo la kuunganisha wateja wapya zaidi ya 250,000 kila mwaka na kwa hesabu hiyo mahitaji ni makubwa kwasababu wengine wanahitaji nguzo zaidi ya moja ili wafikiwe na huduma.

“Na ikumbukwe tumeingia awamu ya tatu ya miradi ya REA, lengo la serikali ni kuona ifikapo mwaka 2025 vijiji vyote nchini vinakuwa na umeme,” alisema

MATUKIO KATIKA PICHA :MWENGE WA UHURU UKIZINDUA,KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA

Posted by Esta Malibiche on MEI 28,2018

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Charles Kabeho akimtwika kichwani ndoo ya maji,Bi.Anna Kyando mara mkazi wa mtaa wa Tanganyika,mara baada ya kuzindua Tanki la Maji lenye ujazo wa lita  laki tano(5)lililojengwa kwa gharama ya  mill. 407.6      katika mtaa wa Tanganyika  kata ya Kinyanambo Halmashauri ya Mji wa Mafinga.  .PICHA NA ESTA MALIBICHE.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Charles Kabeho akimtwika kichwani ndoo ya maji,BiGrace John  mkazi wa Mtaa wa Tanganyika mara baada ya kuzindua mradi huo.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaiafa Charles Francis Kabeho akizindua mnara wa kumbukumbu ya wakimbiza Mwenge  kitaifa 2018 uliojengwa katika Shule ya Sekondari J  J  Mungai .





Club ya kupambana na shule katika Shule ya Sekondari JJ Mungai ikizinduliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Charles Kabeho.



Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaiafa Charles Francis Kabeho akiweka jiwe la Msingi katika vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Ihongole.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaiafa Charles Francis Kabeho,akiweka jiwe la Msingi katika  mradi wa Kilimo bora cha maparachichi katika mtaa wa ndolezi  ,uliopo kijijji cha kiterewasi kata ya boma,lenye ukubwa wa  ekari 16.5 lilopandwa miche 1,031.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaiafa Charles Francis Kabeho akizindua bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Mwinyigumba.










































Jumamosi, 26 Mei 2018

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 28 WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TANZANIA

Posted by Esta Malibiche on MEI 26,2018 IN KITAIFA

15 14
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake TANZANIA(TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa TAWLA Bi. Athanasia Soka wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake TANZANIA(TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
11
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akihutubia kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano mkuu wa 28 wa TAWLA .
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kufanya hima maana Serikali iko katika hatua za mwisho za kuanza kufanya mageuzi makubwa katika eneo la mazingira ya biashara kama ilivyobainishwa hivi karibuni na Waziri wa Viwanda na Biashara.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) unaotanguliwa na mafunzo endelevu ya Sheria.
“Nawapongeza TAWLA kwa namna ya kipekee sana kwa kutimiza miaka 28 ya uhai wake. Ni miaka 28 ya mafanikio makubwa sana. Nawapongeza  kwa sababu, katika miaka 28 ya uhai wenu, hamjawahi kuyumba wala kutoka nje ya lengo la kuanzishwa kwenu, ambalo ni kutumia taaluma ya sheria kuwasaidia wanawake wasio na uwezo kupata msaada wa kisheria na haki zao.” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesema anatambua na kuguswa na kazi nzuri inayofanywa na Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) hapa nchini ya kupigania haki za wanawake kwa kutumia taaluma ya sheria.
Mkutano huo wa mwaka huu ambao umebeba  kauli mbiu ya “Uwekezaji Wenye Tija; Kufungua Fursa kwa Mitaji ya Sekta Binafsi na Umma Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi”
Makamu wa Rais amewataka Chama Cha Wanasheria Wanawake wawasaidie wanawake wajasiriamali kujua sheria,  “Sisi kama wanawake kwanza ni kumnyanyua mwanamke, Ukimnyanyua Mwanamke umeinyanyua Tanzania”
Makamu wa Rais aliwahakikishia TAWLA kuwa Serikali haina upungufu wa dhamira. “ Serikali yenu inajali na inao utashi wa kumkomboa mwanamke kiuchumi”
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano maana maslahi ya TAWLA na ya Serikali yanakutana katikati katika suala hili.
Akimkaribisha Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Afya, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile amewataka TAWLA kutumia maendeleo ya kiteknolojia kujitangaza ili wanawake wengi zaidi wapate taarifa zao na kuweza kupata msaada wa kisheria.
Nae, Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka amesema TAWLA inapenda kuona mtoto wa kike na mwanamke anaendelea kupewa kipaumbele katika maendeleo ya Tanzania.

Ijumaa, 25 Mei 2018

JUMLA YA MIRADI 8 YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA BILL.6 YAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU WILAYANI KILOLO

Posted by Esta Malibiche on Mei 26,2018 IN NEWS
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asiah Abdala.Makabidhiano hayo yamefanyika katika kijiji cha Viwengi ,mpakani mwa Kilolo na Iringa vijijini.PICHA NA ESTA MALIBICHE.

Mkuu wa wilaya ya KiloloAsiah Abdala akipokea Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili jana wilayani kilolo.
.Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Charles Kabeho akiweka jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji uliopo katika kijiji cha Ilundamatwe kata ya Irole Wilayani kilolo.Mradi huo mapaka kukamilika kwake utagharimu kiasi cha Mill.700.PICHA NA ESTA MALIBICHE.
.Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Charles Kabeho akiweka jiwe la Msingi katika Mradi wa  mtambo wa kutibu nguzo za umeme [New forest ]uliopo kata ya  lundamatwe wilayani Kilolo. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Asiah Abdalah,akimsalimia kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Caharles Kabeho.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Asiah Abdalah,akikaribisha wilayani Kilolo  kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Caharles Kabeho
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Asiah Abdalah,akimkaribisha wilayani Kilolo Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Issa 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Aloyce Kwezi akisamilimana na Kiongozi wa Mio za Mwenge kitaifa Charles Kabeho.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Aloyce  Kwezi akimkaribisha  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru  kitaifa Charles Kabeho

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kilolo akimkaribisha kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Charles Kabeho.
Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kilolo akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Charlse Kabeho
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kilolo akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Charlse Kabeho
Mbunge wa Jimbo la Kilolo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,Venansi Mwamoto akisalimiana na kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa
































































NA ESTA MALIBICHE

KILOLO

MKIMBIZA   Mwenge wa Uhuru kitaifa  Ipyana Alinuswe amewataka wazazi na walezi   Nchini kuhakikisha wanawekeza katika elimu kwa kugharamia mahitaji muhimu ya Watoto wao, kama mavazi, viatu, Madaftari sanjari na kuchangia mchango wa Chakula cha mchana kwa wanafunzi wa kutwa chini ya ujumbe mkuu wa mbio za Mwenge 2018 unaosema “ELimu ni Ufunguo wa Maisha Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu”
Hayo ameyasema jana wakati akizungumza na wananachi pamoja na wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Ilula iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, wakati akitoa ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 chini ya ujumbe mkuu unaosema “ELimu ni Ufunguo wa Maisha Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu”
Alinuswe alisema kuwa Serikali ya awamu ya tanao imejipanga kuhakikisha  mitaara ya Elimu inazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuiboresha  mitaara  ili iweze kuzalisha rasilimali watu ambao wataweza kuliletea Taifa Maendeleo.
Akizungumzia utoro mashuleni alisema kuwa swala la utoro kwa wananafunzi linachangiakwa kiasi kikubwa  kuathiri sekata ya Elimu nchini,hivyo ni jukumu la kila mzazi au mlezi kufuatilia maendeleo ya mtoto wake na siyo kuwaachia walimu peke.
Aidha aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo ikiwa nipamoja na kusoma kwa bidii huku ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
‘Ninawaomba wanafunzi kote nchini msijihusishe na mambo ambayo yanaweza kukatisha ndoto zenu katika masomo.Zingatien masomo mnayofundishwa na walimu wenu,epukeni vishawishi vinavyoweza kuwasababaishia kupata ujauzito’.
Nae kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Charles Kabeho akiwa katika mradi wa nyumba ya walimu uliopo katika kijiji cha Msosa  kata ya Ruaha Mbuyuni,alikataa kuweka jiwe la msingi katika  ujenzi wa nyumba ya walimu iliyojengwa chini ya kiwango ukilinganisha na kiasi cha fedha,ambazo ni Mill.90 zilizotumika kugharimu mradi huo mpaka kukamilika kwake.
‘Kutokana na Mradi huu kukosa sifa kutoana na kujengwa chini ya kiwango,pia kutokana na mradi huu kutoendana na thamani ya fedha,Mwenge wa uhuru hautaweza kuweka jiwe la msingi  katika jingo hili,hakikisheni mnawachukulia hatua ya kinidhamu wale wote waliohusika kukwamisha mradi huu kwa namna moja au nyingine’Alisema Kabeho.
 Aidha Kabeho aliwataka  watendaji kufanya kazi kwa makini huku wakizingatia viwango na ubora katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili kuendana na kiasi cha fedha kinachotolewa .

 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asiah Abdalah akisoma taarifa ya miradi ya maendeleo iliyotembelewa na Mwenge wa uhuru,kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Iringa Mjini, alisema alisema  Wilaya yake itaendelea kutekeleza Maagizo mbalimbali yaliyotolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kuhusu uboreshaji wa mradi wa nyumba ya walimu iliyopo katika Kijiji cha Ruaha Mbuyuni uliojengwa chini ya kiwango ukilinganisha na fedha zilizotolewa.Pia alimsimamisha kazi mkandarasi aliyejenga chini ya kiwango mradi wa nyumba ya walimu.
‘Kuanzia sasa namsimamisha kazi  mkandarasi na ninaamuru vyombo vya usalama vifanye uchunguzi haraka iwezekananvyo,mpaka kufikia Mei.30 2018 ripoti  ya uchunguzi nipatiwe’Alisema Asiah.
Aidha alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani kilolo ulizindua, kuwekewa mawe ya msingi pamoja na kukaguliwa miradi ya Maendeleo 8 yenye thamani ya shilingi bilioni 6.
Ndugu kiongozi wa Mbio za wa Uhuru kitaifa,Mwenge wa uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo umeweza  kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji uliopo katika kijiji cha  kitelewasi kata ya Irole, ulizindua mradi wa barabara  ya rami Ilula –Uhambingeto, uliweka jiwe la Msingi katika kiwanda cha kuchakata nguzo za umeme, ,ulizindua maabara za sayansi katika shule ya Sekondari  Kiheka,Ulikagua shuhuli za uzalishaji wa vifaranga vya samaki pia uliweka jiwe la msingi katika mradi wa chumba cha upasuaji katika kituo  cha Afya  mtandika’Alisema Asiah