Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumamosi, 2 Aprili 2016

IPTL yakanusha Tuhuma za Rushwa na Taarifa za Uongo Zilizochapishwa na Gazeti la MwanaHALISI

pap
Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited  (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited Bwn. Joseph O. R. Makandege (katikati), akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu taarifa ya upotoshaji iliyochapishwa na gazeti la MwanaHALISI ikihusisha IPTL kutoa rushwa kwa viongozi waandamizi wa ikulu na watendaji waandamizi wengine serikalini. Kulia ni Mkurugenzi wa uendeshaji wa IPTL Bwn. Parthiban Chandrasakaran na kushoto ni msaidizi wa mwenyekiti mtendaji Bwn. Rajiv Bhesania. Picha na mpiga picha wetu.
……………………………………………………………………………………………..
Makampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan Africa Power Solutions (T) Limited (PAP), tumesononeshwa sana na taarifa iliyochapishwa na gazeti la kila wiki la MwanaHALISI katika toleo namba 332 la tarehe 28 Machi 2016 lenye kichwa cha habari, “Siri za Kikwete, IPTL zafichuka ”; iliyoambatana na nukuu katika ukurasa wake wa mbele inayosomeka “…hadi ndani ya jumba jeupe (Ikulu kwenyewe), Singasinga alitembeza mlungula.
Taarifa hiyo iliyojaa uongo pamoja na kashfa nzito ya rushwa kwa IPTL/PAP na kwa viongozi waandamizi wa serikali ya awamu ya nne na wengine ambao bado wamo katika serikali hii ya awamu ya tano, imediriki kudai kwa kunukuu maneno yafuatayo,….. “Sethi alitoa rushwa kila mahali, ikiwamo Ikulu, ili kufanikisha mpango wake huo….Alihonga kila mtu. Alitoa rushwa kwa kila aliyeona faili la Escrow. Hadi maofisa wa Ikulu na viongozi waandamizi kutoka wizara ya fedha……..hadi ndani ya jumba jeupe (Ikulu kwenyewe), Singasinga alitembeza mlungula. Ni BoT pekee, ambako hakuhonga au kuombwa rushwa.”
Tungependa kukanusha taarifa hizi za shutuma ya rushwa ambazo ni za uongo na uzushi mtupu wenye lengo la kuichafua IPTL na wamiliki wake akiwemo Mwenyekiti Mtendaji, Bw. Harbinder Singh Sethi. Taarifa hizi zisizo na chembe ya ukweli ndani yake zinalenga kuchafua sifa ya Ikulu ambayo ni taasisi nyeti hapa nchini kwa kuihusisha na upokeaji rushwa ambayo ni kosa la jinai kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yetu.
Isitoshe taarifa hizi zimejaa habari za uongo zilizobuniwa kwa nia na madhumuni maovu ya kuichafua sifa za kampuni za IPTL/PAP na mwenyekiti wake Bw. Harbinder Singh Sethi pamoja na kuwachonganisha dhidi ya wananchi wa Tanzania kwa kuwahadaa na kuwaaminisha Watanzania kuwa IPTL/PAP inaendeshwa kwa misingi ya rushwa na udanganyifu, hivyo basi haistahili kufanya biashara hapa nchini.
Awali ya yote, tungependa kuutarifu umma wa Watanzania kwamba tuhuma za rushwa ni tuhuma nzito na wala siyo za kunyamaziwa kabisa. Rushwa ni moja kati ya makosa makubwa ya kijinai ambayo vyombo vya dola vinatilia maanani sana. Hivyo basi, kampuni ya IPTL/PAP haiwezi kukaa kimya wakati tuhuma kama hizi zikiendelea kuchapishwa dhidi yake, huku ikiwahusisha viongozi waandamizi wa serikali, bila ya gazeti husika pamoja na mwandishi wa taarifa hizo kutoa udhibitisho wowote wa tuhuma hizo.
IPTL/PAP tunaamini kwamba taratibu zote za kukabidhiwa kampuni ya IPTL (ikiwemo mali na madeni halali) zilifuatwa. Tunaamini katika utawala wa sheria ambayo inazingatia haki za kila mtu. Hivyo basi, haitakuwa busara kuendelea kunyamazia vitendo vya kiovu vya kuichafua kampuni yetu vinavyofanywa na baadhi ya vyombo vya habari kwa kisingizio cha “uhuru wa kutoa maoni” au “uhuru wa vyombo vya habari”. Kama vyombo vya habari walivyo na uhuru wao, vivyo hivyo IPTL/PAP kama kampuni ina uhuru wa kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria za nchi bila ya kubughudhiwa. Kwa kutuhumu IPTL/PAP au viongozi wake kutoa rushwa, bila kuthibitisha, ni kuihujumu kampuni ili isiweze kutekeleza majukumu yake ya kuchangia ukuwaji wa uchumi wa nchi yetu.
Joseph O. R. Makandege (ADVOCATE)
(Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria)
KAIMU MWENYEKITI MTENDAJI
Independent Power Tanzania Limited / Pan African Power Solutions (T) Limited.

UTAFITI WA MAJI CHINI YA ARDHI, DAR TANGA VINARA UCHIMBAJI VISIMA BILA VIBALI






MIKOA ya Dar es Salaam na Arusha imeelezwa kuongoza kwa uchimbaji wa visima vya maji ya chini ya ardhi usiozingatia sheria na kanuni za sera ya maji ya mwaka 2002 ambayo pia imelalamikiwa na wadau kupitwa na wakati.
Akizungumza na wanahabari mjini Iringa jana katika mkutano uliozungumzia mradi wa utafiti wa hali ya maji chini ya ardhi, Mkurugenzi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji anayeshughulikia rasilimali za maji, Hamza Sadick alisema baadhi ya watu katika mikoa hiyo na mingine yote nchini wamekuwa wakichimba visima bila vibali.
Alisema pamoja na sera hiyo kulalamikiwa, kwa kupitia sheria namba 11 ya mwaka 2009 ya usimamizi wa raslimali za maji kuna kanuni zinazozungumzia taratibu zinazopaswa kufuatwa ili mchakato mzima wa kutafuta na kutumia maji ya ardhini usiwe na dosari.
Alisema kwa mujibu wa sheria hiyo ni kosa kwa mtu au taasisi kuchimba maji ya ardhini bila kibali au kampuni kufanya kazi hiyo bila kuwa na leseni na kibali cha kazi hiyo.
“Nikiri kwamba kuna tatizo kubwa la kufuatilia utekelezaji wa kanuni na sheria hiyo. Udhaifu huo umewafanya baadhi ya wadau wazalishe na kutumia maji ya ardhini bila kufuata taratibu zinazotakiwa kwa mujibu wa sheria hiyo,” alisema.
Mkuu wa mradi huo wa utafiti, Profesa Japhet Kashaigili alisema ongezeko la matumizi ya maji ya chini ya ardhi nchini limechochewa kwa kiwango kikubwa na kupungua kwa maji ya juu ya ardhi kunakosababishwa na ongezeko la watu na shughuli za kibinadamu.
“Mradi huu wa utafiti utatuwezesha kujua kiasi cha maji yaliyopo ardhini, sehemu yanapoingilia, yapo kiasi gani, yanatosheleza watu kiasi gani na kwa muda gani,” alisema.
“Tusipokuwa makini, maji ya ardhini yataathiriwa na shughuli za binadamu na kuongeza mgogoro wa maji nchini. Kuna haja ya kufahamu namna visima vinavyochimbwa, vinavyojengwa na taratibu zingine zote zitakazoyafanya maji hayo yawe ni kwa matumizi endelevu,” alisema.
Utakapokamilika, Profesa Kashaigili alisema mradi huo wa miaka minne, ulioanza kutekelezwa mwaka jana, utasaidia kukuza msingi, taratibu na usimamizi shirikishi kwa njia za kisayansi ambazo rasilimali za maji ya chini ya ardhi zinaweza kutumika kwa uendelevu na hivyo kupunguza umasikini katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuna changamoto kubwa sana ya mgawanyo wa maji jambo linalosababisha rasilimali hiyo isababishe migogoro katika maeneo mbalimbali nchini.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mku wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, RC Masenza alisema mbali na ongezeko la watu, shughuli za kibinadamu na mabadiliko ya tabianchi, kwa pamoja yamesababisha upungufu wa maji.
 
 

 

FEDHA ZA TASAF KILOLO KUWATOKEA PUANI WANAOZITUMIA KWA ULEVI





HALMASHAURI ya wilaya ya Kilolo imezinyoshea kidole kaya zinazonuifaka na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ikiahidi kuziondoa zile zinazotumia kwa ulevi na matumizi mengineyo yasiyokubalika, fedha wanazopewa kwa ajili kugharamia mahitaji ya msingi ikiwemo elimu, afya na maji.
Jumla ya kaya masikini 6,464 za halmashauri hiyo zinanufaika na fedha za mpango huo zinazotolewa kila baada ya miezi miwili kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Kilolo, Venance Mwaikambo alisema; “halmashauri yetu ilianza kunufaika na mpango huo toka Julai mwaka jana na hadi mwezi Machi mwaka huu kaya hizo zilikuwa zimepata malipo ya tano ya zaidi ya Sh Milioni 198 kwa ajili ya mwezi Machi na April.”
Wakati kaya hizo zikijipatia kati ya Sh 20,000 na Sh 70,000 kila baada ya miezi miwili, Mwaikambo alisema zipo taarifa zinazoendelea kuchunguzwa zikihusisha baadhi yao kuzitumia fedha hizo kununua pombe na matumizi ya starehe na michango isiyo ya lazima.
“Serikali haijaleta fedha hizi kama zawadi, inataka ziwatoe kutoka hatua moja hadi nyingine,” alisema huku baadhi ya kaya zikikiri kuanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji na kilimo, kuwapeleka na kuwanunua watoto mahitaji ya shule na kugharamia huduma za afya.
Mwaikambo alisema serikali haiwezi kukubali kuendelea kutoa fedha kwa watu wanaozitumia kwa pombe na wamekwishapeleka maombi TASAF ya kuwaondoa na kuziingiza kwenye mpango kaya nyingine mpya.
Afisa ushauri na ufuatiliaji wa mpango huo wa TASAF wilayani Kilolo, Happy Mpuya alisema serikali kwa kupitia mpango huo inatoa ruzuku ya msingi na ya masharti nafuu kwa kaya masikini ili kugharamia mahitaji ya msingi ikiwemo elimu, afya na maji.

Mpuya alisema ruzuku ya msingi inatolewa kwa kila kaya iliyoandiskishwa kwenye mpango ili kugharamia mahitaji hayo ya msingi na ruzuku ya masharti nafuu inatolewa kwa kaya masikini zenye watoto wenye umri wa kwenda shule na kliniki.
“Msije mkashangaa fedha mnazopata zinapungua kwasababu ya mahudhurio hafifu ya watoto wenu shuleni na wale ambao wanatakiwa kupelekwa kliniki hawapelekwi. Nataka mjue tuna utaratibu wa kufuatilia taarifa zenu za jinsi fedha hizo zinavyowanufaisha,” alisema.


Alisema kaya zitakazobainika kuzitumia fedha hizo kinyume na malengo hayo zitaondolewa katika mpango kama masharti ya mpango yanavyotaka fedha hizo zisitumike kwa shughuli nyingine tofauti na za mpango.

Mmoja wa wanufaika wa mpango huo, Upendo Geufeni wa kijiji cha Itunda aliyepata jumla ya Sh 100,000 toka Julai mwaka jana alisema; “fedha hizo zinamsaidia kwa matibabu na akiba ndogo anayojiwekea imemuwezesha kufuga kuku.” alisema.

Dada huyo mlemavu aliiomba serikali kuboresha mpango huo kwa kutoa msaada utakaowawezesha kujenga nyumba bora.

Ijumaa, 1 Aprili 2016

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) MKOA WA IRINGA UMEWATAKA WAZAZI KUWAINGIZA WATOTO KATIKA MPANGO MPYA WA HUDUMA YA MATIBABU




Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Iringa umewataka wazazi
na walezi kuwaingiza watoto wao katika  mpango mpya wa huduma za
matibabu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18) unajulikana kwa jina
la “Toto Afya Kadi” kwa lengo la kuwawezesha watoto kuwa na uhakika wa
kupata matibabu wakati wote.

Kauli hiyo imetolewa na meneja wa bima ya afya mkoa wa Iringa dk
Mohamed Kilolile  mapema leo hii wakati akizungumza na mtandao huu wa habari ofisini kwake ,alisema kuwa katika jitihada za kufikia lengo la afya
bora kwa watu wote ,Mfuko wa bima ya afya (NHIF)umetanua wigo wake na
sasa unasajili watoto katika huduma zake ili nao wapate huduma zao
pindi wanapokubwa na matatizo ya ugonjwa.

Alisema kuwa mara nyingi wazazi wamekuwa wakitumia garama kubwa katika
kuwahudumia watoto wao katika swala la afya na wakati mwingine kukosa
fedha kwa ajili ya kuwatibu watoto  wao jambo linoloweza wakati
mwingine  kusababisha kupoteza maisha  lakini kwa kupitia huduma ya
toto afya kadi mtoto atatibiwa kwa mwaka mzima kwa shilingi 50,400/=
sehemu yoyote atakayopenda mwanachama .

Kiholile alisema kuwa hii ni fursaa nyingine  ambayo imetolewa kwa
wazazi na walezi ambao ni wanachama wa mfuko lakini  watoto wao
hawakusajiliwa kutokana na ufinyu wa nafasi za utegemezi kuwa ni
chache kwani mara nyingine mwanachama ana watoto sita lakini nafasi
zilizopo ni 4 hivyo wanapaswa kutumia fursa hiyo kusajili watoto wao
.

Alisema kuwa hii ni fursa ya kipekee pia  kwa Watoto wanaoishi katika
mazingira magumu kupata Bima ya afya kupitia wafadhili na wahisani
mbalimbali ambao wangependa kuwasaidia ili pindi wanapopata matatizo
wawe na sehemu ya kupata Matibabu katika vituo Zaidi ya 600 nchi nzima

 Kiholile alisema kuwa walengwa katika huduma hii ni watoto kuanzia
umri wa mika (18) kushuka chini kutoka katika makundi mbalimbali kama
watoto wote wa shule za awali, msingi na sekondari, Watoto wa kutoka
vituo vya kulea watoto yatima na wasiojiweza  ,Watoto waishio na
wazazi/walezi bila kujali uhusiano walionao na kama wanasoma shule, au
hawasomi

Hata hivyo aliwataka wakazi wote wa mkoa wa Iringa kuchangamkia fursa
hiyo ya kipeke waliyokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu kwa kuwandikisha
watoto wao ili wanufaike kwa pamoja na huduma hiyo .

CHAMA cha mpira wa miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) kimetauwa kamati ya uchaguzi



CHAMA cha mpira wa miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) kimetauwa  kamati ya
uchaguzi  itakayohakikisha  inasimamia chaguzi mbalimbali mkoani  Iringa .

Uteuzi wa kamati hiyo unaelezwa kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa
kumaliza migogoro iliyoko ndani ya vilabu pindi wanachama wake
wanapotaka kuitisha uchaguzi lakini kunatokea migongano kati ya
wanachama na viongozi wao .

Akizungumza na mtandao huu wa kali ya Habari ofisini kwake Kaimu Katibu Mkuu wa
IRFA,Ramadhani Mahano alisema kuwa walifikia maamuzi hayo  ya kuunda
kamati  hiyo katika kikao cha wadau kilichoitishwa na mwenyekiti wake
Cypriyan Kuyava kilichofanyika juzi ili kumaliza migogangano ndani ya
vilabu  .

Mahano alisema kamati hiyo itaongozwa na mwenyekiti wake  ambaye ni
GasterMdegela na makamu mwenyekiti akiwa ni Jakson Chaula .
Alisema kuwa kamati hiyo pia itakuwa na wajumbe sita ambao ni Lupyana
Masawa ,Willy Chikweo,Shemu Mhen pamoja na Happness Nduguru

Hata hivyo Mahano alibaimisha kuwa kamati hiyo pia itangozwa na
wanasheria wawili na wajumbe wake ni wanafamilia na wapenzi wa soka na
kamati hiyo itaanza kazi mara moja baada ya uteuzi wake .

Alisema licha ya kuunda kamati hiyo ya uchaguzi hapo awali  chama
chake kililazimika kuunda kamati sita ikiwemo kamati ya Ligi na
Mashindano ambayo mwenyekiti wake atakuwa David Mwamalekela makamu
atakuwa Pascal Bella ambapo wajumbe watakuwa Carlo Mbinda, Gutram
Kawonga, Cletus Kifyoga, Nikolina Sanga, July Sawani na
Isiaka Majaliwa.

Mahano alisema kuwa Kamati ya Waamuzi itaongozwa na David Lugenge
akiawa na wajumbe Julias Mkomwa, Mwanaheri Kalolo, Abuu Yunus na
Atilio Mnyeke.

Alisema kwa upande wa Kamati ya Mipango na Uchumi mwenyekiti atakuwa
Stanford Mwakasala na wajumbe wa kamati hiyo watakuwa Abdallah
Kiyumbo, William Kessy, David Wapalila, Jonnie Nkoma, Daniel Kindole,
Rukia Muwango, Musa Kamtande na Victor Chakudika.


Alisema kuwa Kamati ya Maendeleo wanawake na  Vijana, Mwenyekiti wake
ni Maulidy Toffy, huku wajumbe wakiwa ni Coster Magolosa, Tigana
Lukinja,Gift Mwachang’a,Edina Ndelwa,Thadeo Lukosina Haruna Mduda.

Mahano aliongeza kuwa kamati ya Nidhamu na Usuluhishi mwenyekiti
atakuwa ni Ignas Seboa Lutalemwa akifanya kazi na wajumbe Stanslaus
Matutu, Devotha Chaula na Fredrick Amando

Aliyewakinga wakristo kutoka kwa al shabab atuzwa

Marehemu mwalimu aliyepigwa risasi akiwakinga wakristo wasiuawe na magaidi wa Al Shabab ametuzwa medali ya juu zaidi na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais Kenyatta alipokuwa akihutubia taifa alisema kuwa wale wakenya wachache wanaoonesha ujasiri wa kukabiliana dhidi ya al shabab watatuzwa.

Na hivyo akasema kuwa Mwalimu Farah ametuzwa heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi.
Marehemu Salah Farah alikuwa katika basi lililokuwa likiwasafirisha abiria kutoka mji mkuu wa Nairobi kuelekea Mandera walipotekwa na wapiganaji wa Al shabab.
Image copyrightPSCU Kenya
Image captionRais Kenyatta amemtuza Mwalimu Farah heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi.
Punde wapiganaji hao wakaanza kuwagawanya waislamu na wale wasio waislamu.
Hapo ndipo Mwalimu Farah na abiria wengine waislamu waliponga'amua nia ya wapiganaji hao ilikuwa ni kuua wakristu , waliibua mbinu ya kuwakinga abiria wakristo miongoni mwao ilikuokoa maisha yao.
Farah na wenzake wawili walijeruhiwa vibaya baada ya kukataa kugawanywa kwa makundi.
Image captionMuislamu aliyewaokoa wakristo waliotekwa na Alshabab atuzwa
Kwa bahati mbata Mwalimu Farah alifariki mwezi Januari baada ya kuuguza majeraha ya risasi kwa takriban mwezi mmoja.
Tukio hilo la kijasiri lilichochea umoja miongoni mwa wakenya ambao wameshambuliwa mara kadhaa na magaidi wa Al Shabab.
Hiyo ilikuwa ni mara ya pili basi la kampuni hiyo ya Makkah kutekwa.
Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa waislamu.
Kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili mwaka uliopita lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa.

Hotuba ya Rais Kenyatta yavurugwa


Hotuba ya taifa ya rais wa kenya Uhuru Kenyatta, imetatizwa kwa muda bungeni baada ya wabuge kadha wa upinzani kupuliza firimbi.
Wabunge hao walianza kupuliza firimbi na kuvuruga hotuba ya rais punde tu alipoanza kuitoa.

Image captionMmoja wa wabunge akizindikizwa nje
Ilimbidi spika wa bunge kuwasihi wabunge ambao walionekana kuendelea kupuliza firimbi.
Hata hivyo utulivu ulirejea baada ya spika kuwatupa nje wabunge waliokua wakizipuliza hizo firimbi, na rais akaendelea kutoa hotuba yake kwa taifa.