Jumatano, 27 Septemba 2017

MAANDALIZI YA MAONESHO YA UTALII KARIBU KUSINI YAPAMBA MOTO

Posted by Esta Malibiche on Sept.27,2017  IN Utalii

ZAIDI ya wajasiriamali 350 wamejitokeza kushiriki maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayoanza rasmi leo,ambayo yatafunguliwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa Kasimu hapo tarehe 29,9,2017  hadi Oktoba 2 katika viwanja vya Kichangani mjini Iringa.

Maonesho hayo yameandaliwa na mikoa ya nyanda za juu kusini kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii,  shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido) na wadau mbalimbali ukiwemo Mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST).



























Endelea kutembelea mtandao huu wa habari ili uweze kupata matukio mbalimbali yatakayoendelea katika maonesho ya utalii karibu kusini.

0 maoni:

Chapisha Maoni