Jumamosi, 9 Septemba 2017

DC NACHINGWEA AWATAKA WAGANGA WA JADI KUFUATA SHERIA ZILIZOWEKWA NA SERIKALI

Posted by Esta Malibiche on Sept.9,2017  IN NEWS

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi,Rukia Muwango
akizungumza na waganga wa jadi na tiba mbadala katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, .Rukia Muwango amewataka wanganga wa jadi wilayani humo kufanya kazi kwa kufuata kanuni,  taratibu na Sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na kusajiliwa katika baraza la waganga wa jadi na tiba Mbadala la Taifa.

Agizo hilo amelitoa mapema jana wakati akizungumza na wanganga wa jadi na tiba mbadala katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.

Katika hotuba yake alimwagiza mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kupitia Mratibu wa waganga wa jadi awasaidie kufutilia vibali katika wizara ya Afya na ustawi wa jamii ili wawwze kupata kwa wakati.

Aidha aliwaasa waganga hao,wawe na umoja wao ambao utakuwa ni chombo cha kurahisisha mawasiliano na serikali na taasisi mbalimbali.

Rukia alisema kuwa kujiunga katika  umoja kuna faida nyingi ikiwemo swala zima la kusaidiana, pamoja na kufahamiana na kusaidiana.
Pia aliwaaihi  Kutopiga ramri, Kuzingatia kanuni za afya na usafi ili kuepuka kuambukizana wao kwa wao  na  Kuwashauri wagonjwa wakapime Afya zao Hosp ili kujua wanasumbuliwa na ugonjwa gani kabla ya kuanza kutoa tiba.
Pia aliwaaiaitiza kuhusu suala ya ulinzi na usalama kwa kuwataka kushiriki kikamilifu kawasabau suala la ulinzi na usalama ni wajibu wa kila mmoja wao.


0 maoni:

Chapisha Maoni