Alhamisi, 28 Septemba 2017

MVUA YALETA MAAFA MULEBA

Posted by Esta Malibiche on Sept.28,2017 IN NEWS

Moja ya Nyumba kati ya 18 zilizobomolewa na Mvua iliyonyesha jana wilayani Muleba Mkoa wa Kagera na kuziacha familia zikiwa hazina makazi.
Na Junior Mwemezi Azam News Kagera.
 WILAYA  ya Muleba iliyopo mkoani Kagera, imekumbwa na maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa ya upepo na mawe, iliyonyesha jana Jumanne, saa saba mchana na kusababisha athari katika kata tatu.

Maeneo yaliyoathirika ni kama yanavyoonekana katika mabano: Kata ya Mubunda, (nyumba moja), (mazao ya mihogo) na (migomba), kata ya Buganguzi (nyumba 18) na chumba kimoja cha darasa la sekondari ya Rukindo, kimeezuliwa.

Eneo jingine ni kata ya Ibuga ambapo nyumba, shule ya msingi Ruzinga, chumba kimoja cha darasa kimeezuliwa, pamoja na choo na jiko.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa Azam TV, Junior Mwemezi, aliyepo mkoani Kagera, wanafunzi wawili wamejeruhiwa na kupelekwa kituo cha afya cha Kamachumu (Kabanga).

 Taarifa hizo ni za awali tu, kwani tathmini halisi bado inaendelea kufanyika katika maeneo hayo yaliyoathirika











0 maoni:

Chapisha Maoni