Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumatano, 27 Julai 2016

TANZANIA YAENDELEA KUPATA MAFANIKIO KATIKA KUKABILIANA NA UGONJWA WA VIKOPE (TRACHOMA).


Postedy by Esta Malibicheon July 27, 2016 in JAMII with No comments
VIKO1Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Neema Rusibamayila akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano uliowahusiaha  Wadau wa Wizara hiyo na washirika wa maendeleo Maendeleo kutoka Mfuko wa Malkia Elizabeth unaojihusisha na utokomezaji wa Ugonjwa wa Vikope na wale wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DFID).
VIKO3Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Malkia wa Uingereza unaojihusisha na utokomezaji wa ugonjwa wa Vikope katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania Dk. Aristid Bonifield akieleza namna Mfuko huo utavyoendelea  kuisaidia Tanzania kwa kuwa inafanya vizuri katika kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa nchini leo jijini Dar es salaam.
VIKO4Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo nchini Tanzania (DFID) Vel Gnanendra akifafanua namna wadau wa maendeleo walivyojipanga kuiunga mkono Tanzania kwa kuhakikisha ugonjwa wa vikope (Trachoma) unatokomezwa nchini.
VIKO5Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele,   Upendo John Mwingira akizungumza wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
VIKO6Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sightsavers kutoka Uingereza Dk. Caroline Harper akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa kutokomeza ugonjwa wa Vikope leo jijini Dar es salaam.
VIKO7Washiriki wa Mkutano wa Kutokomeza Ugonjwa wa Vikope kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto  na Wale wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika picha ya Pamoja leo jijini Dar es salaam.
Picha/Aron Msigwa – MAELEZO.
………………………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
 Dar es salaam.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeeleza kuwa licha ya Tanzania kuendelea kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Vikope (Trachoma) jamii bado inalojukumu la kuendelea kuzingatia na kufuata kanuni za afya kwa kufanya usafi wa mwili na mazingira ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Wadau wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele,  Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Neema Rusibamayila amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupunguza ugonjwa huo ikishirikiana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesema kupitia idadi ya wagonjwa wanaougua vikope imeendelea kupungua mwaka hadi mwaka kupitia afua mbalimbali chini mpango ujulikanao kama “SAFEambao unahusisha huduma za Upasuaji,utoaji wa dawa za Antibayotiki, kuosha  pamoja na usafi wa mazingira
Ameongeza wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweza kufanikisha upunguzaji wa ugonjwa huo kwa kutoa dawa/tiba kinga kwa wananchi katika maeneo yaliyoathirika ambapo amesema kufuatia utafiti uliofanyika mpaka sasa wilaya 22 ugonjwa huo umepungua sana kiasi cha wananchi wa maeneo hayo kutohitaji dawa za tiba kinga.

Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali awataka wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa

chp1Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)  rangi sahihi zinazotakiwa kutumika katika bendera ya Taifa wakati akielezea umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi, kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari (Maelezo) Bw. Frank Shija.
chp2Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi, kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Nyamagori Omari
chp3Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (katikati) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)  baadhi ya vielelezo sahihi vya Taifa vinavyotakiwa kutumiwa na wananchi wakati alipokuwa akielezea umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi mapema hii leo Jijini Dare s Salaam kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari (Maelezo) Bw. Frank Shija na kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Nyamagori Omari.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo

BENDI 10 MAARUFU ZA MUZIKI WA DANSI KUWASHA MOTO JUMAMOSI VIWANJA VYA LEADERS

 Mwanamuzi wa mziki wa dansi, Ali Choki akiwaongoza wenzake kutoa burudani mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda walipofika ofisini kwake leo, kuzungumzia Tamasha la muziki huo litakalofanyika Jumamosi  Viwanja vya Leaders ambalo litashirikisha bendi 10 maarufu za hapa nchini.
 Baadhi wa wadau wa muziki wa dansi na wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Mdau wa muziki wa dansi, Asha Baraka akizungumza katika mkutano huo kuhusu tamasha hilo la kukata na shoka ambalo alijawahi kufanyika hapa nchini.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda akizungumza na wanamuziki hao kuhusu tamasha hilo la muziki wa dansi nchini.
 Mkutano ukiendelea.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wa dansi baada ya kuzungumza nao ofisi kwake.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-)

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, DK ANGELINA MABULA AAGIZA HALMASHAURI YA UYUI KUKAMILISHA UNUNUZI WA NYUMBA ZA NHC UYUI

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akitembelea nyumba za gharama nafuu Uyui zilizopo Isikizya wilayani Uyui, Tabora ambapo ameiagiza Halmashauri ya Uyui kulipia nyumba zilizojengwa na NHC ili watumishi wake waweze kuhamia. Kushoto kwake ni Meneja wa NHC mkoani Tabora, Dickson Ngonde.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tabora muda mfupi baada ya kutembelea nyumba za gharama nafuu Uyui ambapo ameiagiza Halmashauri ya Uyui kulipia nyumba zilizojengwa na NHC ili watumishi wake waweze kuhamia. PICHA ZOTE ZA KITENGO CHA MAWASILIANO KWA UMMA NA HUDUMA KWA JAMII CHA NHC.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisikiliza taarifa kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora, Bw. Biseko Musiba wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika mkoa wa Tabora na kujione hali ya maendeleo ya sekta ya ardhi mkoani humo pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo ya taasisi zake.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akimsikiliza Kamishna Msaidzi wa Kanda ya Magharibi, Dorothy Wanzala wakati akikagua masjala ya ardhi ya Tabora. 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisoma mojawapo ya mafaili yaliyopo katika masjala ya Ardhi huku Kamishna Msaidizi wa Kanda ya Magharibi, Dorothy Wanzala akishuhudia. 
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tabora muda mfupi baada ya kufika katika ofisi hizo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akizungumza na watumishi mbalimbali wa sekta ya ardhi mkoani Tabora.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tabora muda mfupi baada ya kufika katika ofisi hizo.

MKATABA KATI YA TTCL NA BHART AIRTEL WAISHA RASMI

TT1Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL), jinsi ya mfumo wa kutoa taarifa kwa wafanyakazi unavyofanya kazi wakati alipotembelea ofisini hiyo jijini Dar es salaam.
TT2Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni  ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt . Kamugisha Kazaura akisoma taarifa ya utendaji kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Hayupo pichani) wakati alipoongea na uongozi wa kampuni hiyo, jijini Dar es salaam.
TT3Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Profesa Tolly Mbwete akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati Waziri alipotembelea ofisi hiyo, jijini Dar es salaam.
TT4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na Uongozi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakati alipotembelea kampuni hiyo, Jijini Dar es salaam.
TT5Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni  ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt . Kamugisha Kazaura akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipofanya mazungumzo na wafanyakazi wa kampuni hiyo,jijini Dar es salaam.
TT6Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Jijini Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA BENJAMINI SAWE -MAELEZO
…………………………………………………………………………………………………..
Serikali imehitimisha ubia kati ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), na Kampuni ya Bhart Airtel ya India kwa kuilipa kampuni hiyo Shilingi Bilioni 14.9 na hivyo kuirudisha TTCL mikononi mwa Serikali kwa asilimia miamoja.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hatua hiyo ni mkakati wa Serikali wa kuiwezesha TTCL kujitegemea ili kuzalisha faida, Kuimarisha Miundombinu yake, na kutoa gawio Serikalini.
“Tunawataka TTCL mjipange vizuri mjitangaze ili muwe kampuni kubwa na bora ya mawasiliano hapa nchini”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa amesema katika kuiongezea nguvu TTCL Serikali itawapa kituo cha  Kutunza Taarifa cha Kijitonyama (Internet Data Center) ili ikisimamie na hivyo kujipatia mapato kupitia gharama za uendeshaji na usimamizi wa kituo hicho.
Amewataka wafanyakazi wa TTCL kufanya kazi kwa bidii, kasi, uaminifu, ubunifu na kuulinda Mkongo wa Taifa ili uwawezeshe kuwa na huduma bora na za uhakika wakati wote.
“Tumetumia fedha za mkongo wa taifa kumlipa mbia mwenzenu bhart airtel ili kuiwezesha TTCL kumilikiwa na Serikali kwa asilimia miamoja hivyo changamoto inayowakabili sasa ni kufanya mabadiliko makubwa katika upande wa kutafuta masoko ili kuweza kuongeza idadi ya wateja na kufanya kazi kwa faida”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Aidha Prof Mbarawa amesema katika kuijali TTCL, Serikali imeipa masafa ya 1800 na masafa ya 2100 na itawaongezea masafa ya 800 yatakayowawezesha kuwa na huduma ya 4G LTE yenye  mtandao wenye kasi na hivyo kuiongezea wateja hususani katika huduma za data.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL,  Profesa Tolly Mbwete amesema TTCL imejipanga kutoa huduma zake katika maduka makubwa, hospitali, stesheni za treni, mabasi ya mwendokasi na viwanja vya ndege katika jiji la Dar es salaam na Miji mikubwa ili kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma za mtandao na data wakati wote.
Naye,  Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura, ameishukuru Serikali kwa fursa mbalimbali inazoipa kampuni hiyo na kumhakikishia Waziri Prof Mbarawa kuwa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo matokeo ya mkakati wa mabadiliko ya kibiashara yataanza kuonekana.
Dkt. Kazaura amesema kuwa tayari watumishi wenye mtazamo wa mabadiliko ya kiteknolojia wameajiriwa na wengine watapewa mafunzo ili kuhimili soko la kibiashara na kuiwezesha TTCL kunufaika na miundombinu yake iliyopo nchi nzima.
Waziri Prof. Mbarawa alikuwa akizungumza na Menejimenti na wafanyakazi wa TTCL ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kuzungumza na wafanyakazi na taasisi zilizopo chini ya Wizara yake.

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA JUMAMOSI 30 JULAI 2016 STUTTGART,UJERUMANI

indexBaada ya kuwadatisha washabiki katika maonyesho mawili makubwa kule bayreuth na tubingen sasa kamanda Ras Makunja anakipeleka kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni katika onyesho kubwa la XXL Afro Summer Jam mjini Stuttgart nchini ujerumani,onyesho hilo litafanyika siku ya jumamosi 30 Julai 2016 katika ukumbi mkubwa Kulturhaus
Arena,uliopo Ulmer Str. 241, 70327 Stuttgart,ujerumani,akiongea na vyombo vya habari kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja alisema Ngoma Africa band ni mali ya washabiki na ina kazi moja tu nayo kudatisha washabiki katika kila onyesho bila kuremba remba , bendi hiyo iliyojizolea umaarufu na maelfu ya washabiki kila kona duniani
imejiwekea rekodi ya aina yake kuwa ni bendi ya mwanzo ya kiafrika kuimiri vishindo,na kudumu kwa miaka 23 ughaibuni na kufanikiwa kuwanasa washabiki wa kimataifa.
ungana nao at www.ngoma-africa.com




SERIKALI YATANGAZA MAOMBI RUZUKU AWAMU III

indexNa Asteria Muhozya, DSM
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ambayo inatekeleza Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) imetoa taarifa ya kukaribisha maombi ya Ruzuku Awamu ya Tatu kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini.
Akizungumza katika Kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa, TBC1, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe alisema kuwa, kiasi cha ruzuku kilichotengwa kwa shughuli hiyo ni Dola za Marekani Milioni Tatu.
Profesa Mdoe alisema kuwa, taratibu zote za kupata washindi wa ruzuku hiyo zitafanyika kwa uwazi huku zikishirikisha Vyama vya Wachimbaji vya Mikoa (REMA), lengo likiwa ni kupata walengwa stahiki kutokana na kuwa, vyama hivyo vinawatambua wanachama wao.
“Mbali na vyama vya wachimbaji, pia Serikali itashiriki kupitia ofisi zetu za Kanda zilizoko katika Mikoa yote kabla ya kufikishwa katika ngazi ya Wizara ambapo pia kutakuwa na Kamati Maalum ya kushughulikia suala hilo,”alisisitiza Prof. Mdoe.
Akizungumzia lengo la utoaji ruzuku hiyo alisema kuwa, ni kukuza mitaji ya wachimbaji wadogo na kuongeza kuwa, tayari Serikali imekwisha toa ruzuku hiyo katika Awamu Mbili, ambapo katika Awamu ya Kwanza kwa mwaka wa fedha 2013/14, Serikali ilitenga kiasi cha Dola Laki Tano (US $ 500,000), ambapo jumla ya vikundi 11 vya wachimbaji vilinufaika na kila kikundi au mchimbaji walipata kilipata wastani wa Dola Elfu Hamsini (US $ 50,000).
Akizungumzia ruzuku Awamu ya Pili alieleza kuwa, kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Serikali ilitenga takriban shilingi Bilioni 7.2, ambapo wanufaika 111 walishinda kati ya waombaji 720.
“Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao ndani ya siku 21 kuanzia tarehe 20 Julai, 2016. Mwombaji anatakiwa kujaza nakala Tatu (3) za fomu za maombi na kuziwasilisha katika Ofisi ya madini ambapo wahusika wanafanya shughuli zao,” alisema Prof. Mdoe.
Pia alizitaja nyaraka ambazo mwombaji anatakiwa kuambatisha na maombi yake kuwa ni pamoja na;  Nakala ya leseni ya uchimbaji au biashara ya madini au leseni ya biashara iliyothibitishwa na Kamishna wa viapo;  Nakala ya Cheti na Katiba ya kuandikishwa kwa kampuni au ushirika.
Aidha, alisema nyaraka nyingine ni pamoja na Nakala za stakabadhi za malipo ya Serikali ya ada za mwaka, mrabaha na kodi; Nakala ya Cheti cha Mlipa Kodi (TIN); Mpango wa Utunzaji Mazingira (EPP) ulioidhinishwa na Afisa Madini Kanda ikiwemo taarifa ya uzalishaji kwa kipindi kisichopungua miezi sita.
Yapo mafanikio ambayo yamepatikana kufuatia Serikali kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo. Baadhi ya  mafanikio ya wanufaika wa ruzuku Awamu ya kwanza ni pamoja na Kikundi cha Itandura Miners Cooperation Society cha Nyamongo  kilichoongeza uzalishaji wa dhahabu, kampuni ya Precious Decor ya Tanga inayomilikiwa na Mwanamama  inayochimba madini ya stone  ambayo sasa ni maarufu jijini Dar Es Salaam kwa kurembesha kuta .
Aidha, mbali na utoaji ruzuku, Serikali imefanya jitihada kadhaa za kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini na kuhakikisha kuwa, uchimbaji mdogo unakuwa endelevu na unakua kutoka uchimbaji mdogo kwenda uchimbaji  wa Kati hatimaye mkubwa.
Kufuatia malengo hayo, tayari Serikali imetenga maeneo 35 kwa wachimbaji wadogo yenye jumla ya hekta 242,400.81 sehemu mbalimbali Tanzania Bara.
Pia, Serikali imepanga kujenga vituo saba vya mfano katika maeneo ambayo kuna uchimbaji mwingi wa madini, ambapo vituo hivyo vinatarajiwa kujengwa kati ya mwaka 2016 hadi 2018. Aidha, vituo hivyo, vitaitwa centres of excellence ambapo migodi ya mfano itajengwa na mitambo ya uchenjuaji itasimikwa ili wachimbaji wapate huduma ya kuchenjuliwa madini yao kwa gharama nafuu.
Aidha, ili kuhakikisha madini ya vito yanayochimbwa nchini yanaongezwa thamani, Serikali imefungua Kituo cha mafunzo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kilichopo Mkoani Arusha kwa ajili ya kufundisha uchongaji na ukataji wa madini hayo ili kuyaongezea thamani.
Pia, Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), linatoa huduma ya mafunzo ya kitaalamu ya nadharia na vitendo kwa wachimbaji wadogo wa madini na kuwapatia miongozo ili kuboresha shughuli zao.
Miradi inayoweza kupewa ruzuku katika awamu ya III ni kama ifuatavyo:
 NA AINA YA MIRADI KIWANGO CHA JUU CHA RUZUKU (USD)
1 Miradi ya kuendeleza, kuboresha na kupanua uchimbaji madini au kurekebisha mazingira yaliyotokana na shughuli hizo. 100,000
2 Miradi ya kupanua na kuboresha uchenjuaji madini au kurekebisha mazingira yaliyotokana na shughuli hizo. 100,000
3 Miradi ya kuboresha teknolojia ya uchimbaji madini, uongezaji thamani au uchenjuaji usiotumia zebaki. 100,000
4 Miradi ya uongezaji thamani hususani ukataji na uchongaji madini / mawe. 100,000
5 Miradi ya wakina mama katika maeneo ya uchimbaji mdogo yenye lengo la kutoa huduma kwa wachimbaji wadogo. 15,000