Jumatano, 25 Julai 2018

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MKOANI SONGWE-ILEJE

Posted by Esta Malibiche on JULY 25,2018 IN KITAIFA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele mara baada ya kuzindua
shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbuge wa Jimbo la Ileje Mhe. Janeth Mbene mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais)



  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya shamba la Misitu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mipango-Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais)



 Kikundi cha Ngoma cha Sange kikitumbuiza ngoma ya Ling'oma wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia  wakazi wa kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais)

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  amezindua shamba la miti katika hifadhi ya Misitu Iyondo Mswima lililopo Katengele wilayani Ileje mkoani Songwe ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.

Shamba hilo lililo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni moja kati ya mashamba mapya yakiwemo Biharamulo (Chato Geita), Buhigwe (Kigoma) na Mpepo (Mbinga, Ruvuma).
Akisoma taarifa ya Shamba hilo kwa Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Mipango –Wakala wa Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo amesema kuwa mpaka shamba la miti la Iyondo Mswima limeweza kutoa ajira kwa wananchi 400 katika msimu wa kupanda miti, pia shamba limetoa ajira zingine 200 wakati huu wa maandalizi ya bustani ya miti, hekta 201 zimepandwa miti kama sehemu ya upanuzi wa mashamba ya miti ya Serikali ambapo bustani yenye jumla ya miche 430,000 kwa ajili ya upandaji miti wa mwaka 2018/2019.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele ambapo shamba la misitu la Serikali Iyondo Mswima limezinduliwa, Makamu wa Rais amewataka wananchi hao kutunza na kuyalinda mazingira kwa kupanda miti kwa wingi ambapo kila mwaka wananchi watapewa miche 50,000 na Wakala wa Huduma za Misitu wa Serikali.
Makamu wa Rais pia alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Sange ambapo aliwaambia wananchi wa kijiji hicho kuwa Mungu amewapa rasilimali nzuri sana hivyo hawana budi kuyatunza.
Makamu wa Rais amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje kuhakikisha Maafisa Ugani wanashuka kwa wananchi na kutoa ushauri namna ya kufanya shughuli za kilimo vizuri.
Makamu wa Rais amesema Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1.5 katika bajeti mwaka huu iliyopita kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya ya Ileje.

0 maoni:

Chapisha Maoni