Jumatano, 25 Julai 2018

SERIKALI YAAGIZA UANZISHWAJI WA MABARAZA YA WAZEE NCHINI.


  Posted by Esta Malibiche on Julai 25,2018 IN NEWS


Pix 1 (1)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akifungua jengo jipya la Wazee na wasiojiweza  Kolandoto lililopo mkoani Shinyanga.
Pix 2 (1)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi vifaa na mahitaji kwa ajili ya wazee na wasiojiweza mara baada ya kufungua jengo jipya la Makazi hayo ya  Kolandoto lililopo mkoani Shinyanga.
Pix 5
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na Mwenyekiti wa wazee waishio katika makazi ya Kolandoto Mzee Somolo Shija mara baada ya kufungua jengo jipya la Wazee na wasiojiweza  Kolandoto lililopo mkoani Shinyanga.
Pix 3
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wazee na wananchi wa Kolandoto wakati wa uzinduzi wa  jengo jipya la Wazee na wasiojiweza la Kolandoto Mkoani Shinyanga.
Pix 4
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo la wazee na wasiojiweza la Kolandoto lililopo Mkoani Shinyanga kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kabla ya uzinduzi wa jengo hilo .
NA WAMJW, SHNYANGA
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezitaka Mamlaka za Mikoa na Wilaya kuanzisha Mabaraza ya Wazee katika mikoa na Halmashauri nchini.
Agizo hilo limetolewa mkoani Shinyanga na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akizindua jengo la makazi ya kulea Wazee na wasiojiweza ya Kolandoto yaliyopo mkoani Shinyanga.
Akizungumza na wazee na wanachi wa eneo la Kolandoto Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wazee ni tunu kwa taifa na jamii imeaswa kuwatunza na kuewaenzi kwa utumishi na mambo makubwa waliyofanya katika taifa letu.
Ameongeza kuwa Serikali ipo katika mpango wa kuendelea kukarabati makazi mengine 16 yaliyopo sehemu nyingine nchini.
” Niseme tu Serikali inawajali Wazee kwa kiasi kikubwa na itahakikisha inawatunza wale Wazee wote wasio na ndugu wa kuwalea”.
Dkt Ndugulile amewaasa wazazi na jamii kupambana na mimba na ndoa za utotoni na kuwaomba Wazee nchini wawe washauri na walezi wazuri kwa wajukuu zao katika kuzuia mimba na ndoa za utotoni.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro amesema kuwa Serikali ya Wilaya itaendelea kuwalinda na kuwatunza Wazee kwani ni sehemu pekee ya kuchota busara ili kuwezesha Jamii kuishi katika maadili mema.
“Sisi kama Wilaya tutalisimamia suala la kuwalea Wazee hawa ambao ni tunu ya taifa” alisisitiza Mhe. Josephine.
Akito taarifa ya ujenzi wa jengo hilo Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa makazi hayo yamegharimu jumla ya Tsh . Millioni 138 mpaka kukamilika kwake.
Bibi. Sihaba ameongeza kuwa ujenzi huo umetokana na uchakavu wa majengo yaliyokuwepo hivyo kuwapa mazingira salama Wazee waishio katika makazi hayo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wazee wa Makazi hayo Mwenyekiti wa Makazi Mzee Somolo Shija ameishukuru Serikali ya Awamu ya tano kwa kuwawezesha kupata makazi mapya kwani walikuwa wakiishi katika majengo chakavu.
“Tunaishukuru Serikali yetu kwa kutujali wazee” alisisitiza Mzee Shija.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014 kuna jumla ya wazee 4,14,382 sawa na asilimia 5.6 ya watanzania wote ambapo ndugu na Serikali wanajukumu la kuwalea na kuwatunza katika kaya zao.

0 maoni:

Chapisha Maoni