Jumatano, 25 Julai 2018

WANAUME MKOANI IRINGA WATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMA VVU

Posted by Esta Malibiche on Julai 25,2018
Mkuu wa wilaya ya mufindi Jamhuri Wiliam akizindua rasmi kampeni ya 'FURAHA YANGU' pima,jitambue,ishi Mkoani Iringa.Uzinduzi huo ulifanyika jana katika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa ikiwa na  lengo la kuhamasisha wannachi hususani wanaume kupima vvu.picha na Esta Malibiche.


WANAUME  mkoani Iringa wametakiwa kujitokeza kwa wingi  kupima ili kujua Afya zao na kuanza dawa mapema  ili  kupimguza maambukizi mapaya.

Iringa ina jumla ya watu wapatao 18,000 wanaoishi na maambukizi ya VVU na wengi wao ni wanaume ambao hadi sasa hawajui hali zao za maambukizi.
Akizungumza jana na wananchi wa mkoa  wa Iringa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘furaha yangu’pima,jitambue,ishi iliyofanyika katika viwanja vya mwembetogwa Manispa ya Iringa, mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Iringa,ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William alisema kuwa takwimu zilizofanyika mwaka 2017 zinaonesha Iringa inakadiriwa kuwa na watu 72,000 wanaoishi na maambukizi ya vvu na kati ya hao hadi kufikia Juni 30 ,2018 watu 54,000 walikuwa wamejiunga na huduma za tiba na matunzo wengi wao wakiwa ni wanawake.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa Christopher Magala akipima maambukizi ya vvu katika Uzinduzi wa kampeni ya" Furaha yangu" pima,jitambue,ishi iliyozinduliwa jana mkoani Iringa.Picha na Esta Malibiche
Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe ambae pia ni Diwani wa kata ya Isakalilo [CHADEMA] akipima maambukizi ya vvu katika Uzinduzi wa kampeni ya" Furaha yangu" pima,jitambue,ishi iliyozinduliwa jana mkoani Iringa.Picha na Esta Malibiche.



0 maoni:

Chapisha Maoni