Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro aipongeza Taasisi ya Foundation
For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhamasisha maswala ya
elimu katika Mkoa wa Arusha awataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano
huo’ aliyasema hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi
Levolosi jijini hapa, ambapo Taasisi hiyo iliandaa Tuzo maalumu kwa
mwalimu bora(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu
Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza
katika hafla hiyo ,iliyofanyika hivi karibuni katika shule ya Levolosi
jijini hapa,ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa wameaanda Tuzo
hiyo kwa shule za msingi jiji la Arusha na Meru kwa walimu 20
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel
Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya sombetini,Caroline Kiyoja cheti
cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha
kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo
maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Sinoni,Dorice Mhina cheti
cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha
kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo
maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Levolosi,Elizabeth Minja cheti
cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha
kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo
maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Uhuru,Jane Mkomwa cheti
cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha
kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo
maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Lucky Vicent Julius Saunyi cheti
cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha
kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo
maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Daraja mbili Leah Mshana cheti
cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha
kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo
maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Waalimu
kutoka shule za msingi jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na
mgeni rasmi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya cheti pamoja na kiasi
cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja Tuzo hiyo maalumu iliandaliwa
na shirika la Foundation For Tomorrow kwaajili ya waalimu waliobainika kufanya kazi zao kwa umahiri mkubwa
Na Pamela Mollel,Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro ameipongeza Taasisi ya Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhamasisha maswala ya elimu katika Mkoa wa Arusha .
Aliyasema
hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini
hapa ambapo alisema shirika hilo limekuwa bega kwa bega katika
kuhamasisha maswala mbalimbali ya Elimu na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo
“Foundation
for Tomorrow wamekuwa mstari wa mbele sana katika maswala ya elimu
mfano mzuri leo wameanda Tuzo maalumu kwa mwalimu bora ambaye amekuwa
akifanya kazi zake kwa umahiri mkubwa”alisema Daqarro
Kwa upande wake Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa lengo la Tuzo hiyo ni kutia hamasa miongoni mwa walimu waliobainika kufanya kazi zao kwa bidii na umahiri mkubwa
Alisema
kuwa katika zoezi hilo la kumsaka mwalimu bora limezingatia vigezo
vyote ikiwemo uwezo wa kuhamasisha ufikiri wa kina miongoni mwa
wanafunzi,uwezo wa kutengeneza mazingira ya kushiriki na mazingira
rafiki ya kujifunza,uvumbuzi na ubunifu katika swala zima la ufundishaji
na utekelezaji wa mtaala
Kayanda
aliongeza kuwa vigezo vingine ni pamoja na kujikita katika kusaidia
watoto wenye changamoto za kujifunza pamoja na uzoefu wa kujifunza
Alisema
kuwa katika Tuzo hiyo ya mwalimu bora kila mwalimu atapewa zawadi ya
cheti pamoja na kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja