Posted by Esta Malibiche on MEI 18,2017 IN NEWS
Mkuu
wa Wilaya Ikungi Miraji Mtaturu katikati akiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya ns viongozi wa halmashauri
baada ya kumaliza kikao nao.
Mjumbe
mwakilishi wa madhehebu ya dini sheikh Salum Ngaa akichangia hoja
wakati wa kikao kilichoongozwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji
Mtaturu pichani wakiwa na wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya.
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Haika Massawe akichangia
hoja wakati wa kikao cha wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akitoa maelekezo wakati alipokutana na kamati ya mfuko wa elimu ya wilaya.
……………………………..
MKUU
wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu amekutana na kamati ya
mfuko wa elimu wilaya na kuwaomba kuwa wazalendo katika kutafuta njia
za kutatua changamoto za elimu wilayani humo.
Mfuko huo umeundwa baada ya uanzishwaji wake kuridhiwa na kikao cha baraza la madiwani kilichoketi hivi karibuni.
Akizungumza
katika kikao cha kuwapatia majukumu yao Mtaturu amesema mfuko huo
utakuwa na jukumu la kuratibu masuala yote yatakayosaidia kuboresha
utoaji wa elimu katika shule za msingi na sekondari.
“nawapongezeni
kwa heshima mliyopewa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa kamati hii,naimani
kuwa mtafanya kazi kwa uzalendo mkubwa ili matunda ya uwepo wenu
yaonekane kwa kuitoa elimu yetu hapa ilipo na kuipeleka mbali
zaidi,”alisema Mtaturu.
Alisema
wakifanikiwa kuondoa changamoto zilizopo watakuwa wameboresha mazingira
ya utoaji elimu na kuongeza ufaulu wa watoto jambo ambalo waliazimia
walipokutana wadau wa elimu.
Akitoa
taarifa kwenye kikao hicho katibu wa mfuko huo Salum Athuman alisema
ili kutatua changamoto za elimu zilizopo katika wilaya hiyo zinahitajika
jumla ya shilingi bilioni 26 kwa ajili ya miundombinu ya elimu ikiwemo
ujenzi wa vyumba vya madarasa,nyumba za walimu,maabara,matundu ya vyoo
na mabweni.
Aidha
mwenyekiti wa kamati hiyo Hamis Maulid kwa niaba ya wajumbe alisema
wamepokea kazi hiyo na wataifanya kwa uadilifu mkubwa ili malengo
yaliyokusudiwa yatimie.
Disemba
mwaka jana mkuu wa wilaya huyo alikutana na wadau wa elimu ili kubaini
changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ambapo waliweka maazimio
yapatayo 37 yenyek ulenga kuboresha elimu wilayani humo na moja ya
mkakati waliouweka ndio umezaa wazo la kuanzishwa kwa mfuko huo wenye
wajumbe 15 ambao wameanza kazi rasmi ili kutafuta njia ya kutatua
changamoto za elimu wilayani humo.
Wilaya hiyo ina jumla ya shule za sekondari 30 ikiwemo za kidato cha sita 3 na shule za msingi 108.
0 maoni:
Chapisha Maoni