Alhamisi, 4 Mei 2017

DC IRINGA RICHARD KASESELA AWATAKA WATENDAJI KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI

Posted by Esta Malibiche on Mei 5 2017 in NEWS 

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wananchi wa kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa.Picha na Davi.
​Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela amewataka watendaji wa kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa kuhakikisha wanawasomea wananchi mapato na matumizi.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika moja ziara yake aliyoifanya ikiwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi,huku akiambatana na Mkurugenzi wa Manispaa ya  Iringa Dr.Willium Mafwele,Naibu Meya Nzala Lyata,Mbumge wa Viti maalum mkoa wa Iringa Ritha Kabati,Diwani wa kata ya Mlandege Mwamwindi,maafisa Tarafa pamoja na watendaji.

Kasesela alipokea kero mbalibali kutoka kwa wananchi ikiwa ni pamoja na Mgogoronwa ardhi,
unyanyasaji wa kijinsia,ulinzi na usalama pamoja na kutosoma mapato na matumizi jambo ambalo lilisababisha Mkuu wa wilaya kukasirishwa na  hatimae kutoa tamko kwa watendaji hao ndani ya wiki mbili wawe wameshawasomea wananchi mapato  na matumizi laasivyo waachie ngazi.

Katika mkutano huo  liliibuka swala la ujenzi wa soko ambalo limechukua karibu miaka miwili kuanza,ambapo Mkuu wa wilaya alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kuhakikisha soko hilonlimaanza mara moja.


Katika hotuba yake mkuu wa Wilaya alisema kuwa huu ni wakati wa kufanya kazi kwa kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi ccm.

"Ninawaomba tufanye kazi,huu siyo muda wa kupiga siasa bali ni muda wa kuwaletea maendeleo wananchi.Tutete wanyonge ili waweze kujikomboa katika lindi la umasikini"" Alisema Kasesela na kuongeza kuwa
"" Sisi sote titapimwa 2020,hivyo ninawaomba tuweke itokadi zetu pembeni na tufanye kazi huu si muda wa siasa."Alisema Kasesela.

0 maoni:

Chapisha Maoni