Posted by Esta Malibiche on MEI 18,2017 IN NEWS
Kushoto
ni Jamali Juma afisa mradi wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za
Mazingira kwa vitendo (LEAT) akifuatiwa na Afisa habari wa LEAT Edina
Tibaijuka pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha kibada Philipo Nyavili wakati wa mkutamo wa hadhara wa kijiji cha kibada ukiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha kibada
Hawa
ni baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo wa hadhara wenye
lengo la kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na Maliasili za
kijijiNa Fredy Mgunda, Iringa.
Ili kuongoza au kusimamia jamii ni lazima kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kuondoa migogoro mbalimbali inajitokeza na itakayo kujitokeza kwa sababu ya kuzivunja sheria na taratibu hizo.
Hayo
yamesemwa na Afisa mradi wa Mradi wa timu ya wanasheria watetezi wa
haki za Mazingira Jamali Juma wakati wa mkutano wa kijiji cha kibada
kilichopo kata ya sadani wilayani Mufindi Mkoani Iringa kwa kuwataka
viongozi na wananchi kutimiza wajibu na haki ili kukifanya kijiji kiwe
na maendeleo.
Juma
alisema kuwa sheria na taratibu zilizopo hapa kijiji zitanatakiwa
kufuatwa kwa ajili ya manufaa ya sasa na ya kizazi kichacho lakini pia
inajenga imani na amani ya kijiji.
"Leo
hii usipofuata sheria na taratibu za kijiji lakina utakwazana na
viongozi au wananchi na kupelekea migogoro ndani ya kijiji kwa kuwa
sheria zinakuwa zimekiukwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977" alisema Juma
Aidha
Juma aliwataka viongozi wa kijiji cha kibada kuitisha mikutano ya
hadhara na kuwasomea mapato na matumizi ili wananchi wajue wapi kijiji
kimetoka kimaendeleo na ipi mikakati ya kimaendeleo kijiji.
"Ukipita
vijiji vingi unakuta migogoro mingi inayotokana na kutosomewa mapato na
matumizi kwa sababu binafsi za viongozi husika hivyo ni lazima viongozi
wa vijiji kuongoza vijiji kwa kufuata sheria na taratibu za
kijiji"alisema Juma
Lakini
Juma aliwataka wananchi wa kijiji cha kibada kutunza na kuvilinda
vyanzo vya maji na Maliasili walizonazo na kuacha kuishi kwa mazoea ili
kuboresha Mazingira ili yarudi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa kulima
kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia.
"Jamani
kuna njia nyingi za kulima mboga mboga kwa njia ya kisasa kwa mfano
unaweza kuchukua gunia au sarufeti na kuuweka mchanga kisha kupanda
mbegu za mboga na kumwagilia maji machafu unayokuwa unayatumia nyumbani
kwao na kuvifanya vyanzo vya maji kuwa salama" alisema Juma
Fadinard
yilikwipande,Shauri na Stephano waliitaka serikali kuanga upya sheria
za kilimo cha mboga mboga kilinacholimwa kwenye utongo mnyevumnye au
karibu na vyanzo vya maji kwa akili ya kilimo changu kwa ajili ya
kujiongezea kipato chao.
"Sisi
tunalima kwenye vijaruba vidogo vidogo tu maarufu kama vinyungu wala
hatuleti madhara yoyote ya uharibifu wa vyanzo vya maji na mbona miaka
yote tulikuwa tunalima bila kuharibu Mazingira na serikali itambue kuwa
Kilimo hiki ni cha kitamaduni sasa inatakiwa kutofautisha sheria za
mambo ya asili au ya kitammaduni"walisema wananchi wa kibada
Kwa
upande wake Afisa habari wa timu ya wanasheria watetezi wa haki za
Mazingira kwa vitendo (LEAT) Edina Tibaijuka aliwashauri wananchi na
viongozi wa kijiji cha kibada kuzifuata sheria walizoletewa za kulinda
Mazingira na vyanzo vya maji hadi pale serikali itakapoa tamko liingine
kuhusu hiyo sheria.
"Jamani
sheria ni msumeno hivyo mnapaswa kuzifuata kwa kuwa msipozifuta mtatiwa
nguvuni na kupelekwa mahakama hivyo itakuwa inawapunguzia nguvu kazi
yenu na kupelekea Msumbufu kwa familia zenu,Mimi nawaomba tiini sheria
bila shuruti ili kuepukana na hayo matatizo" alisema Tibaijuka
Tibaijuka
aliwashauri wananchi na viongozi wa kijiji cha kibada kupelekea
malalamiko yao kwa viongozi wa serikali, madiwani na wabunge wao ili
kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo la sheria hiyo mpya iliyokuja
baada makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Samia Suluhu
la kukataza Kilimo chochote kile kwenye vyanzo vya maji.
Naye
Mwenyekiti wa kijiji cha kibada Philipo Nyavili aliwaomba viongozi wa
serikali kuifikiria upya sheria waliyoitunga juu ya matumizi ya vyanzo
vya maji kwa kuangalia utamaduni wa watu Vijijini hasa kwenye swala la
Kilimo cha kipindi cha kiangazi maeneo ya mabondeni kwa kuwa wananchi wa
Vijijini wantegemea kilimo hicho.
"Hivi
kama huku wilaya ya Mufindi wakulima wanategemea Kilimo cha kulima
kwenye mabonde maarufu kama Kilimo cha kwenye vinyungu kwa kupanda mboga
mboga pamoja na mahindi ya msimu wa kiangazi"alisema Nyavili
0 maoni:
Chapisha Maoni