Jumatano, 17 Mei 2017

SERIKALI YAIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO MKOANI IRINGA

Posted by Esta Malibiche on MEI 17,2017 IN NEWS


Naibu waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo akisalimiana na wakuu wa Idara mara baada ya kuwasili katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya kilolo mkoani Iringa ,ikiwa ni moja ya ziara yake aliyoifanya jana
 
Naibu waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo akielekea kukagua ujenzi unaoendelea katika jengo la Hospitali ya wilaya ya kilolo Mkoani Iringa,katika moja ya ziara yake aliyoifanya jana.PICHA NA ESTA MALIBICHE
Na Esta Malibiche
KILOLO

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipongeza Halmsahauri ya wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa kwa utendaji wake mzuri  katika kutekeleza na kukamilisha shughuli za Maendeleo   kwa wakati,kuendana na fedha zilizotumika.

Pongezi hizo zimetolewa kutokana  na ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya kilolo unaoendelea kujengwa kwa kasi,ambayo mpaka kukamilika kwake kunatarajia kugharimu kiasi cha shilingi Billion 12.

Akizungumza  mapema leo hii[jana]mara baada ya kutembelea na kukagua  ujenzi huo namna unavyoendelea,Naibu waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa[ TAMISEMI]Suleiman Jaffo alilidhishwa jinsi ujenzi huo unavyoendelea kujengwa katika kiwango cha hali ya juu na kuahidi kuwa,serikali iko tayari  kutoa kiasi cha fedha kilichobakia ili mradi huo uweze kukamilika kuanza kutoa huduma mara moja.

Jaffo alisema kuwa pamoja na kuridhishwa na kazi ya ujenzi huo,serikali inataka kuona ujenzi huo ukikamilika kwa wakati ili kupunguza msongamano kwenye Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.

''Nimefurahishwa na kasi hii ya ujenzi na ubora wa jengo lenyewe.Hivi ndivyo serikali inataka miradi ijengwe,kwa usimamizi huu na uaminifu mliouonyesha nitahakikisha namshauri Mh. Rais ili fedha iliyobaki kukamilisha iweze kutengwa na hatimae tukamilishe kwa wakati ili iweze kuanza kutumiaka.''Alisema Jaffo

Awali akisoma taarifa  ya ujenzi wa mradi huo,Afisa mipango wa Halmashauri ya kilolo Josephine Mukungu,alisema  ujenzi wa Hospitali hiyo unaoendelea umelenga kuboresha huduma za Afya kwenye wilaya hiyo na kupunguza changamoto za kusafirisha wagonjwa wa Rufaa umbali mrefu,pia kupunguza vifo vya akina mama na watoto waliochini ya miaka mitano.

Mukungu alisema lengo kuu la ujenzi wa Hospital hiyo  ni kusogeza huduma za Afya karibu na jamii ikiwa ni utekelezaji wa sera ya Afya ya mwaka 2009 na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama  Tawala ya mwaka 2015na kusema kuwa Mradi huo ukikamilika utawezakuwanufaisha wananchi zaidi ya 222,146,kutokana na  kasi ya ukuaji wa watu unaolkadiliwa kuwa 1.7%  kwa mwaka kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012.

''Kwa kuzingatia ramani uya wizara ya Afya,waanawake,wazee,jinsia na watoto ili kukamilisha miundombinu yote,zaidi ya tssh. 12,000,000,000 zinahitajika.Hivyo kwa hatua za awali ili Hospitali iweze kufanya kazi kiasi cha Tsh. 4,200,000,000 zinahitajika''alisema Mukungu

Alisema kutokana na andiko lililowasilishwa wizara ya fedha na mipango,Halmashauri imekwisha pokea kiasi cha Tsh. 1,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo muhimu,ambapo kwa kuanzia Halmashauri hiyo imeanza kujenga majengo  matano ya ghorofa moja moja  kati ya majengo saba yatakayokamilisha Hospitali hiyo.

''Katika kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa ufanisi na kuendana na thanmani ya fedha kwa kiwango kinachohitajika,Halmashauri imetoa zabuni kwa wakandarasi watatu chini ya usimamizi wa wakala wa majengo Tanzania[TBA]  kujenga miundombinu ya awali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jingo la mionzi na umalizaji wa jingo la opd,ambao upo chini mkandarasi pancha building Construction ambae ameingia mkataba na Halmashauri kwa kaisi cha Tsh.1,199,255,387.50.Kati ya fedha hizo Tsh.292,345,00 kwa ajili ya ukamilishaji wa jingo la opd na kiasi cha Ts.906,910,387.5 ni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mionzi'''Alisema Mukungu

''Ujenzi wa jengo la OPD umefikia hatua ya kuzekwa,kupigwa lipu,kuweka dari,mifumo ya umeme na ujenzi unaendelea.Jumla ya Tsh. 277,324,000.80 zimelipwa kati ya Tsh.1,199,255,387.5 kutoka mkataba Namba LGA\027\LGDG\SP\201\2017\W\01’’’’alisema Mukungu.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliishukuru serikali ya awamu ya tano jinsi inavyoijali jamii kwa kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wananchi ikiwa nipamoja na ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Kilolo.

Asia alimshukuru Naibu waziri Suleiman Jaffo kwa kutekeleza ahadi yake aliyowaaahidi wananchi katika moja ya ziara yake aliyoifanya mwaka jana  kuwa,serikali itahakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati,kuendeleza ujenzi wa Hospitali hiyo na kuhakikisha anasimami.

Nae Mbunge wa jimbo la Kilolo Venus Mwamoto alisemani  zaidi ya miaka  kumi  sasa imepita toka kuanzishwa kwa wilaya hiyo  lakini,kwa muda wote huo hakukuwa na Hospitali ya wilaya,hivyo mara ujenzi huo ukikamilika wananchi watapata matibabu kwa wakati na haraka tofauti na ilivyokuwa hapo awali wakitumia umbali mrefu kusafiri.







0 maoni:

Chapisha Maoni